TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 27, 2016

WIZARA YA AFYA YAFANYA UZINDUZI WA MRADI WA SIKU YA KIMATAIFA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA MASHULENI


 Mkurugenzi wa Mtandao wa Mpaluleblogs: Shaaban  akiwa na Wanahabari wakati wa Uzinduzi wa hedhi salama kwa ajili ya wasichana mashuleni


MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI  (SOUTHERN SUN HOTEL) LEO

Naomba urejee kichwa cha habari hapo juu,siku ya Ijumaa leo tarehe 27/Mei/2016  saa 4 kamili  Mkurugenzi wa Chief Promotions Bwana Amon Mkoga  atazungumza na waandishi wa Habari kuhusu Uzinduzi wa mradi wa Hedhi Salama kwa wasichana walipo mashuleni katika wilaya sita 1.Masasi-Mtwara 2.Ruangwa-Lindi 3.Kongwa-Dodoma 4.Uyui-Tabora 5.Kahama-Shinyanga 6.Geita 7.Handeni –Tanga 8.Kasulu-Kigoma .haswa katika kutatua changamoto mbalimbali kama upatikanaji wa pedi,maji,vyoo vya kike na kiume,vyumba mahususi vya kubadilishia nguo kipindi cha hedhi .
Kuelekea siku ya hedhi kitaifa kesho tunaiomba serikali ifute ushuru wa vifaa vya hedhi ili kuweza kushuka bei ambapo kila muhitaji atapata kwa bei rahisi.

Vile vile siku ya kesho Chief Promotions kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama PSI,SNV,EU(Umoja wa Ulaya,Barclays Bank,Makankasha Security,Village Supermarket,Coca Cola,Knight Support,Dr.Amon Mkoga Foundation na Benki ya wanawake wameandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika kesho saa 12 asubuhi kuanzia uwanja wa Biafra mpaka TTCL Kijitonyama Dar es Salaam.

Ripoti ya UNICEF zinasema msichana mmoja kati ya 10 wa kiafrika huacha kwenda shule kwa siku 4 mpaka siku 5 kwa mwezi au kuacha shule kabisa,kutokana na mazingira duni katika kipindi cha Hedhi.
Ninaomba uwepo wa chombo chako cha habari siku na muda  tajwa hapo juu ili muweze kutusadia kuipatia taarifa jamii.

Mgeni Rasmi -mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto

Ujumbe hakuna maisha bila ya Hedhi salama,
Ndimi
Amon Mkoga
Mkurugenzi Mtendaji
Chief Promotions
P.O.Box 78566
Simu: 0755 638 004/0655 638 004
Barua Pepe:dramontz2002@yahoo.com
Tovuti:www.chiefpromotions.or.tz
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment