Posted: 20 Jun 2012 11:02 PM PDT
Na Halfan Diyu
KATIBA muongozo ambao taifa lolote limejiwekea jinsi ya kuendesha shughuli za kila siku za taifa lao. Taifa linakuwa imara linapokuwa na katiba imara na viongozi bora, wenye maono ya kuwaletea maendeleo wananchi wao. Taifa
lazima lisimamie misingi ya haki na ianishwe katika katiba kwani ni
haki pekee huleta watu pamoja na kiondoa misingi yote ya unyonyaji. Pia, ndio sheria mama nchini na katiba zote zinazotengenezwa na taasisi au vyama vya siasa zinapaswa kuakisi yale yote yaliyopo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si kupingana, kinyume na hapo itakuwa batili. Maendeleo
ya nchi nyingi zilizoendelea yamechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na
katiba imara na inayokidhi mahitaji ya sekta mbalimbali kama za elimu,
afya, utamaduni, uchumi, siasa, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa
wananchi kuzungumza au kutoa maoni yake. Hakuna ubishi kuwa nchi
ya Marekani ni moja ya mataifa ambayo yamekuwa na katiba imara inayogusa
sekta zote nilizotaja hapo juu na ambayo imedumu kwa muda mrefu bila kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara. Matokeo yake tunashuhudia Taifa hilo likisimama kwa muda mrefu kwa kuwa na uchumi imara duniani. Nchini
baada ya kuundwa kwa katiba mwaka 1977, tayari yameshafanyika
marekebisho kumi na nne hadi mwaka 2005, ambapo ya kwanza yalifanyika
mwaka 1979. Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini, Bw.Deus
Kibamba anasema marekebisho ya kwanza ya mwaka 1979 yaliingiza moja ya
mambo muhimu katika taifa letu, ambapo ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Rufaa. Mwaka
1980 yalifanyika tena marekebisho katika Katiba na moja ya marekebisho
hayo ni kuingizwa kwa katiba ya Zanzibar katika Katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania. Mwaka 1982 yalifanyika marekebisho ya mfumo
mpya wa kuchagua wakuu wa mikoa, mwaka 1984 marekebisho bora ambayo
yalizingatia maoni ya wananchi ambapo suala la haki za binadamu
liliingizwa katika katiba. Hayo ni baadhi ya marekebisho machache
tu ambayo yalifanyika katika hiyo miaka niliyoitaja hapo juu na kufikia
hadi mwaka 2005 jumla ya mabadiliko kumi na nne yalifanyika na mengi
yaligusa masuala ya siasa na muungano, achilia machache kama ya haki za
binadamu ambayo yanagusa jamii yote bila kubagua. Vilevile ubora
na uimara wa katiba mpya ijayo uende sambamba na kudumu kwa miongo mingi
na si kufanya marekebisho ya mara kwa mara ambayo yanagharimu fedha
nyingi za walipa kodi. Katika kipindi hiki Taifa lipo katika
vuguvugu la kuanza mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya, ambapo
ifikapo tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 2014 Katiba hiyo inatakiwa iwe imekamilika. Wananchi
waelimishwe umuhimu wa kuchangia maoni ya masuala mbalimbali yanayogusa
maisha yao ya kila siku na si kuwa na mawazo mgando ya kuchangia katika
masuala ya muungano na siasa tu, ingawa pia yana umuhimu katika mustakabali wa Taifa. Nionavyo
jamii inatakiwa kupata uelewa na nafasi ya kuchangia maoni yao ili
kupatikana kwa katiba bora, imara itakayogusa sekta zote kwa ajili ya
maendeleo ya Taifa.
|
Posted: 20 Jun 2012 11:00 PM PDT
|
Posted: 20 Jun 2012 10:59 PM PDT
Na Mwandishi Wetu
BENDI
ya muziki wa dansi ya Mashujaa 'Wana Kibega', inatarajia kufanya ziara
maalumu kwa mashabiki wake wa Kanda Ziwa mwishoni mwa wiki. Akizungumza
Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter alisema
onesho la kwanza litafanyika Ijumaa mjini Kahama, mkoani Shinyanga. Alisema Jumamosi watatoa burudani mjini Geita na Jumapili watakuwa jijini Mwanza. Meneja
huyo alisema wameandaa shoo ya nguvu kwa wapenzi wa mikoa hiyo
ikiongozwa na Lilian Internert, akiwa na wengine ambao wataonesha shoo
zao mpya zilizoundwa hivi karibuni. Sospeter alisema katika
maonesho hayo nyimbo zao zote zitapigwa, ikiwa pamoja na zilizokuwa
hazijawahi kusikika kwenye vyombo vya habari. "Kuna nyimbo mpya
ambazo zitaanza kusikika huko huko, tunafanya kama kuwatambulisha
wapenzi wa Kanda ya Ziwa waone mambo mapya ya Mashujaa," alisema
Sospeter. Alisema bendi hiyo itarejea Dar es Salaam Jumatatu na
kuendelea na ratiba yake ya kila wiki, huku ikiandaa ziara yake ya mikoa
ya Kusini ambayo itafanyika mwezi ujao.
|
Posted: 20 Jun 2012 10:56 PM PDT
Na Heri Shaaban, Pwani
WAZIRI
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenela Mukangara amesema
Mashindano ya Shule za Sekondari (UMISSETA) ya mwaka huu yatatumika
kuunda timu ya pili ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars). Akizungumza
katika ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika juzi mjini Kibaha,
Waziri Fenela alisema haina budi kuunda timu B ya wanawake kwa kutumia
wachezaji watakaopatikana katika michuano hiyo. "Ombi langu la
mapendekezo haya, najua litatekelezwa mara moja ili tuwe na timu mbili
za wanawake za soka ili zije kuwa tishio siku za baadaye. "Nimeshudia
mechi ya mpira miguu ya wanawake kwa timu za Kanda Nyanda za Juu
Kusini, iliyofungwa mabao 10-1 dhidi ya Kanda Mashariki ambazo
zimeonesha mpira mzuri," alisema. Alisema mashindano hayo ni
chachu ya kuibua vipaji vya wanamichezo mbalimbali, ndiyo maana mwaka
huu michezo hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali katika sekta hiyo, ili
waweze kuangalia vijana wenye vipaji. Waziri huyo alisema
michezo ni ajira inatakiwa kutambua mchango wake, hivyo Ofisi ya Waziri
Mkuu TAMISSEMI kwa ushirikiano na Wizara ya Mafunzo ya Ufundi zinatakiwa
kufanikisha mashindano hayo ambayo ndiyo chachu ya kupata wachezaji wa
timu ya Taifa wa baadaye. Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI, Jumanne Sagin amezuia walimu wakuu kuuza maeneo ya viwanja vya
shule badala yake vibaki kwa ajili ya michezo.
|
Posted: 20 Jun 2012 10:37 PM PDT
Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa (AF), Sullivan Benetier (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam juzi,
kuhusu kituo hicho kuandaa Maadhimisho ya Siku ya Muziki Duniani
inayofanyika leo, kwa kushirikisha bendi na vikundi mbalimbali vya
muziki. Kulia ni Kiongozi wa Bendi ya FM Academia Nyoshi Saadat. (Picha
na Charles Lucas)
|
Posted: 20 Jun 2012 10:36 PM PDT
Na Mhaiki Andrew, Songea
WACHEZAJI
20 na viongozi watatu wa timu ya soka ya vijana wenye umri chini ya
miaka 17 ya mkoa wa Ruvuma, imeondoka jana mjini hapa kwenda jijini Dar
es Salaam kushiriki mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2012. Akizungumza
mjini hapa juzi usiku katika halfa ya kuwaaga vijana hao, Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa (FARU) Joseph Mapunda, alisema kazi
iliyokuwa mbele yao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa kombe hilo mwaka
huu. Wachezaji waliondoka pamoja na viongozi wao kuwa ni Joseph
Hilly, Adeligoti Kipipa, Amosi Bandawe, Ramadhan Ramadhan, Peter
Malekoni, Maneno Zuberi na Severin Mkandawile (Mbinga), Panjo Mshindo,
Anthon Heneko, Omari Ally na Shaban Chitete (Tunduru). Wengine ni Edward Songo, Mapunda Sandali, Ebroni Haule, Sunday Kalonga, William John, Juma Said, Ally Abdallah. Aliwataja
wachezaji wengine kuwa ni Shanely Michael na Hamis Yasin kutoka
Manispaa ya Songea na Kocha Mkuu wa timu hiyo Francis Samatta, msaidizi
wake Francis Kasembe na mkuu wa msafara, Emmanuel Kamba. Mapunda
alisema wilaya zingine tatu za Namtumbo, Nyasa na Songea Vijijini
katika wachezaji wake hawakuweza kuteuliwa baada ya kushindwa
kushiriki mashindano hayo.
|
Posted: 20 Jun 2012 10:35 PM PDT
Na Mwandishi Wetu
SIGARA
ya Embassy kupitia chapa yake ya Club E, inakuja na pati ya Hollywood
Glam Night. Pati hiyo itafanyika kesho jijini Dar es Salaam katika
Ukumbi wa Blue Pearl ulioko Ubungo Plaza kuanzia saa 2 usiku. Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam juzi na Tumaini Toroka
ambaye ni Meneja wa Embassy ilieleza kwamba pati hiyo ambayo itakuwa na
maudhui ya Hollywood, ambapo wanachama na wapenzi wa burudani watapata
watashuhudia burudani mbalimbali na vivutio vya Hollywood. Alisema
wanachama wa Club E, wataingia bure kwenye pati hiyo kwa kupitia
mwaliko maalumu na kwa watu wengine ambao si wanachama na wangependa
kuhudhuria, watalipa sh. 30,000. Kiingilio hicho kitajumuisha vinywaji
pamoja na chakula. Alisema kwa miaka mitano iliyopita, Club E
imejijengea jina kwa kufanya pati zenye ubora na hadhi ya hali ya juu
kwa wanachama wake. "Ukiacha suala la kuburudisha wanachama
wake, kwa kipindi cha miaka mitano, Club E pia imeweza kutoa mchango
wake kwa kuinua wanamuziki wetu wa ndani ambao wamepata muda wa kuimba
kwenye jukwaa moja na wasanii mbalimbali wa bara la Afrika na Marekani. Alisema
Club E ilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwaleta pamoja na
kuwaburudisha wanachama wake, ambao ni wavutaji wa sigara ya Embassy. "Tangu
kuanzishwa kwake Club E imefanya pati nyingi na kuwaleta wasanii wengi
wa ndani na nje ya nchi kutumbuiza. Wasanii walioletwa na Club E ni
pamoja na Werrason, Miriam Makeba, Amani, Blue 3, Lady Jay Dee, Mbilia
Bell, Tshalla Muana, JB Mpiana, FM Academia, Chaka Khan na Falii Ipupa,"
alisema.
|
Posted: 20 Jun 2012 10:34 PM PDT
Baadhi
ya mashabiki wa soka wa klabu za Ligi Kuu ya England, waliojitokeza
kwenye kushiriki mashindano ya kumsaka 'Shabiki Bomba' kwenye Castle
Lager Superfans yaliyofanyika Kimara jijini Dar es Salaa jana (kulia) ni
Msumi Maneno akifanyiwa usaili kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho.
Mshindi wa mashindano hayo atakwenda Afrika ya kusini kushuhudia Fainali
za Mataifa ya Afrika mwakani. (Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 20 Jun 2012 10:31 PM PDT
Na Mhaiki Andrew, Songea
MKUU
wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa filamu ya Adelahida, ambayo imechezwa na waigizaji wazawa wa
mkoa huo. Uzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Songea Klabu, Julai
Mosi mwaka huu.
Akizungumza
mjini hapa jana Mratibu wa filamu hiyo, Shukrani Faraja alisema filamu
hiyo ni muhimu kwa vizazi vya sasa katika kuelewa historia ya zamani ya
mababu.
Alisema filamu hiyo itakapoingiwa sokoni itasaidia
kuelewa mila, desturi na tamaduni za mababu wa mkoa huo ambazo walikuwa
wakiziendekeza ikiwemo kuuwa watoto watakaobainika wamezaliwa mapacha
zaidi ya wawili kwa imani za kutokea mikosi katika ukoo wao.
Faraja
alisema pamoja na filamu hiyo waigizaji wake wameelezea mambo mengi,
huku wakiowanisha na kipindi chote ambacho Tanzania inajitawala.
Mratibu
huyo alisema uzinduzi huo utakwenda sambamba na maigizo mbalimbali
ikiwemo na wasanii wa kizazi kipya, ngoma za asili za makabila ya Mkoa
wa Ruvuma na wazee wa kimila ikiwa ni tambiko lao kabla ya filamu hiyo
kuingia sokoni.
|
Posted: 20 Jun 2012 10:29 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi
WACHEZAJI
wapya wa Yanga, Said Banahuzi na Juma Abdul 'Baba Ubaya', wameanza
mazoezi na timu hiyo yanayoendelea katika Uwanja wa Kaunda, Dar es
Salaam na kufanya timu hiyo kuzidi kuimarika. Wachezaji hao
wamesajiliwa msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar ambapo wameungana na nyota
mwingine, Nizar Khalfan katika kuhakikisha wanaimarisha timu hiyo
inayojiandaa na michuano ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Bara. Gazeti
hili lilishuhudia wachezaji hao wakifanya mazoezi ya pamoja na wenzao
ambao walianza tangu Jumatatu wakiwa chini ya Kocha Msaidizi, Fredy
Felix 'Minziro' huku mashabiki wakionekana kuvutiwa nao. Pamoja
na kufanya mazoezi hayo, lakini kivutio kikubwa kilikuwa kwa Baba Ubaya
ambaye hucheza beki wa kushoto, alikuwa akionesha umahiri wake katika
kuuchezea mpira na kupiga pasi zenye uhakika. Beki huyo ambaye ni
tunda na Kituo cha Michezo cha Tanzania (TSA), baada ya kuonesha uwezo
mkubwa akiwa kituoni hapo ndipo aliposajiliwa na Mtibwa akiichezea timu
ya vijana (U-20) lakini msimu uliopita alipandishwa na kuchezea timu ya
wakubwa. Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Minziro alisema
anapata matumaini mapya baada ya kuona kila kukicha wachezaji
waliosajiliwa na timu yake wanakuja, hivyo ataanza programu ya mazoezi
siku si nyingi. Alisema wachezaji waliokuwa katika timu ya Taifa
(Taifa Stars) bado hawajaanza mazoezi, lakini ana imani baada ya siku
chache za kupumzika watajiunga na wenzao kufanya mazoezi. Timu
hiyo ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, ambalo walilitwaa mwaka
jana chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Sam Timbe lakini baadaye alifukuzwa
na mikoba yake kuchukuliwa na Kostadin Papic.
|
No comments:
Post a Comment