Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote,mara baada ya kuifungua semina ya siku moja iliyofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani |
WEMA SEPETU KUMSHUSHA NYOTA WA FILAMU OMOTOLA JALADE KUTOKA NIGERIA
Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade katika pozi matata |
Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jaladekatika kivazi cha ofisini |
Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade katika kivazi cha kutokea |
MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, anatarajia kumdondosha nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade hapa nchini.
Wema Sepetu, ambaye kwa sasa anatamba kwenye tasnia ya filamu anatarajia kumleta Omotola kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo Super Star.
Filamu hiyo ya Super Star, inazungumzia maisha ya Wema kuanzia utotoni kushiriki kwake Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss Tanzania hadi kuingia kwenye filamu.
Kwenye filamu hiyo Wema ameshirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo mwimbaji wa Machozi Band, aitwaye Mwinyi.
Omotola, ambaye atatua Tanzania wiki hii, alianza kutamba kwenye tasnia hiyo baada ya kutoka na filamu iitwayo Iva mwaka 1993.
Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52, zikiwemo, Ties That Bind (2011), A Private Storm
Ije (2010), My Last Ambition (2009), Beyonce & Rihanna (2008), Temple of Justice (2008), Tomorrow Must Wait (2008) na nyingine nyingi.
Wema Sepetu, ambaye kwa sasa anatamba kwenye tasnia ya filamu anatarajia kumleta Omotola kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo Super Star.
Filamu hiyo ya Super Star, inazungumzia maisha ya Wema kuanzia utotoni kushiriki kwake Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss Tanzania hadi kuingia kwenye filamu.
Kwenye filamu hiyo Wema ameshirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo mwimbaji wa Machozi Band, aitwaye Mwinyi.
Omotola, ambaye atatua Tanzania wiki hii, alianza kutamba kwenye tasnia hiyo baada ya kutoka na filamu iitwayo Iva mwaka 1993.
Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52, zikiwemo, Ties That Bind (2011), A Private Storm
Ije (2010), My Last Ambition (2009), Beyonce & Rihanna (2008), Temple of Justice (2008), Tomorrow Must Wait (2008) na nyingine nyingi.
Wakazi wa arusha waipokea kwa shangwe huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5
Sehemu ya Wakazi wa Arusha wakishangilia ujio wa huduma mpya ya Airtel Supa5 |
Wakazi wa jiji la Arusha wakiendelea kuhamia na kujiunga kwa wingi na Airtel. |
.Sehemu ya Wakazi wa Arusha wakishangilia ujio wa huduma mpya ya Airtel Supa5 |
WAKALI DANCERS WASHEREHEKEA MIAKA 4 DAR LIVE MBAGALA
SHEREHE za miaka minne ya kundi la Wakali Dancers jana zilifana ndani ya
ukumbi wa kisasa wa burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, jijini
Dar. Vikundi vya taarab vya Kings, Coast Modern na Kidumbaki kutoka
Zanzibar pamoja na Talent Band vilifanya ‘bonge la kufuru’ kwa mashabiki
waliofika katika ukumbi huo kwa ajili ya kuburudika wikiendi.
Wakali Dancer wakiwa na bendera yenye nembo yao wakati wakisherehekea miaka 4 ya kuanzishwa kundi lao.
...wakizidi kunogesha sherehe hizo.
...wakicheza wimbo wa Thriller ulioimbwa na Michael Jackson.
...wakizidi kupagawisha.
MMOJA MBARONI KWA MAUAJI, HUKU AJALI KUSABABISHA KIFO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa DODOMA, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen akisani taarifa kwa ajili ya
vyombo vya habari(Press Release)
Na. Luppy Kung’alo,wa Jeshi la Polisi Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la RAMADHANI S/O AMIR Mwenye umri wa miaka 24, Mkulima na Mkazi wa Pahi wilayani Kondoa kwa tuhuma za
mauaji.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alisema tukio hilo la mauaji lilitokea tarehe 17/06/2012 majira ya saa
17:15 jioni katika kitongoji cha Lusangi Kijiji na Tarafa ya Pahi Wilaya ya
Kondoa Mkoani Dodom.
Akizungumzia
tukio hilo alisema kwamba mtuhumiwa huyo alimshambulia na kumpiga bwana MOHAMED S/O IBRAHIM Mwenye umri wa miaka 60,
Mkulima na Mkazi wa Lusangi kwa kumpiga
na kipande cha kuni kichwani na kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani.
“Marehemu
alikuwa nyumbani kwake na mara ghafla akatokea mtuhumiwa huyo na kuanza kumpiga
na kumshambulia.” Alisema Kamanda Zelothe Stephen
Bw. Zelothe
alisema kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa
na majirani wa eneo hilo walidai kwamba mtuhumiwa ni mgonjwa wa akili, hata hivyo mtuhumiwa
amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mkuu huyo wa
Polisi Mkoa wa Dodoma alisema Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
BODI YA UTALII TANZANIA YAPONGEZWA KWA KAZI NZURI
Na: Geofrey Tengeneza
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imepongezwa kwa kazi nzuri inayofanya
katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na jukumu kubwa
la kuitangaza Tanzania kama eneo bora lenye vivutio vingi vya kitalii
duniani pamoja na ushindani mkubwa kutoka nchi nyingine na hivyo kufanya
idadi ya watalii wanotembelea nchi yetu kuendelea kuongezeka mwaka hadi
mwaka sambamba na kuongezeka kwa pato la Taifa litokanalo na sekta ya
utalii.
Akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii
hivi karibuni katika ukumbi wa Mikutano wa chuo cha Utalii jijini Dar
es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna
Tarish amesema Bodi ya Utalii imeendelea kutekeleza vema majukumu yake
na kwamba wafanyakazi wa taasisi wana kila sababu ya kujivunia mafanikio
haya kwa kuwa kila mmoja kwa nafasi yake amechangia katika mafanikio
hayo. Amewataka wafanyakazi kuendelea kuwa wabunifu zaidi
kwa kuibua mawazo mapya yatakayosaidia kuboresha utendaji wa Bodi siku
hadi siku na kujipima kwa matokeo ya kazi na mipango wanayojiwekea.
“Nawaomba sambamba na kuwa na mipango ya kazi mfanye kazi kwa matokeo
na kuwa wabunifu kadri iwezekanavyo kwa kila mfanyakazi kujitahidi kuwa
na mawazo mapya ambayo yatasaidia shirika kuboresha utekelezji wa majukumu
majukumu yake” alisema Bibi Maimuna.
Akizungumzia mikutano ya Baraza la Wafanyakazi sehemu za kazi Katibu
Mkuu huyo amesema jambo muhimu sana katika kutatua baadhi ya matatizo
yanayoikabili taasisi husika kwa kuwa mikutano hiyo ndicho chombo cha
juu kabisa ambacho wafanyakazi kupitia wawakilishi na viongozi wao wa
vyama vya wafanyakazi na Menejimenti wanapata fursa ya kukaa pamoja
na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu taasisi na wafanyakazi kwa
ujumla. Amesema kwa kufanya hivyo ni kutekeleza kwa vitendo agizo la
serikali linalolenga katika kuendeleza na kudumisha utawala bora jambo
ambalo linadumisha umoja na mshikamano baina ya wafanyakazi.
Baraza hili jipya la wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania pamoja
na mambo mengine kadhaa katika kikao chake hicho cha siku mbili lilipokea
na kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya Bodi katika kipindi cha
mwaka 2012/2013, na taarifa ya utekelezaji wa mipango na kazi
mbali mbali za Bodi katika kipindi cha Julai 2011 hadi Machi 2012.
Utalii nii Sekta ya pili nchini kwa kuchangia katika pato la Taifa
ambapo inachangia kiasi cha asilimia 17.2 baada sekta ya Madini ambayo
ndiyo inaongoza. Aidha kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 idadi ya
watalii waliotembelea Tanzania kutoka nchi mbalimbali duniani iliongezeka
kutoka watalii 782,699 mwaka 2010 hadi watalii 867,994. Nayo mapato
yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Kimarekani 1,254.50
mwaka 2010 hadi ufikia dola za kimarekani 1,348,30
PHILIP GUCHA AKABIDHIWA PIKIPIKI YAKE ALIYOSHINDA KATIKA PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO"
Mkazi wa Iringa Bw.
Philip Gucha akiwa amepanda pikipiki mpya ambayo
amejishindia katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA
SBL, makabidhianoya pikipiki hiyo yalifanyika jana mkoani Iringa mjini.
Kampuni ya Bia ya Serengeti jana
imekabidhi zawadi ya bajaji mpya na pikipiki mpya kabisa kwa washindi wa
zawadi hizo mkoani
Iringa ambapo Bajaji ilikabidhiwa kwa Bw Fadhili Manzi katika mji mdogo
wa Mafinga mkoa humo na pikipiki ilikabidhiwa kwa bw………… mjini Iringa
ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL
inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Ni wiki ya 6 sasa kati ya wiki 16 za
promosheni hiyo ambapo katika droo ya sita iliyochezeshwa hivi karibuni
washindi wawili walipatikana ambao ni bw. Deusdedit Tobias Njau 22
kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya
na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro ambaye
amejinyakulia pikipiki mpya kabisa ambayo naye atakabidhiwa zawadi yake
siku chache zijazo pindi taratibu za usajili zitakapokamilika.
Makabidhiano
hayo yalifanyika jana na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa
vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini huku tukio zima likishuhudiwa
na umati mkubwa wa watu
ambao walitoa maoni mabalimbali juu ya zoezi zima la promosheni hiyo na
kusema SBL inabadilisha maisha ya watanzania wengi hasa vijana jambo
ambalo linapaswa kuigwa na makampuni na mashirika mengine hapa
nchini.Washindi hao wameishukuru SBL nakuitaka iendelee na moto huohuo.
Akiongea na waandishin wa habari wakati
wa kukabidhi zawadi hizo meneja wa masoko SBL mkoa wa Iringa Bw. Philip
Gucha amesema washindi hao walipatikana
kihalali na kwamba kila mtanzania mweneye sifa zilizoainishwa katika
vigezo na masharti ya promosheni hiyo ana haki na uwezo wa kushiriki na
kushinda zawadi mojawapo au zaidi kati ya zawadi zilitajwa katika
promosheni hiyo “leo tunawakabidhi hawa zawadi zao lakini zawadi hizi ni
robot u ya zawadi zite ambazo tunawasubiri ninyi watanzania na wateja
wetu wote kujishindia” alisemaGucha
na kuwataka watanzania wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya
Serengeti waendelee kushiriki kwani batahi ya mtu haiwezi kwenda kwa
mwingine.
Hii ni droo ya sita wiki ya sita
mfululizo ambapo bado takriban wiki 11 sasa ili kuisha kwa promosheni
hiyo ya pekee na ya kwanza kutokea hapa nchini ambapo zaidi ya milioni
780 za kitanzania zinashindaniwa kote nchini
Kwa upande wake mshindi wa bajaj bw. Fadhili Manzi
amesema kwasasa safari ya maisha yake na familia yake itabadilika
kutokana na zawadi hiyo kwani ni sawa na mkulima hodari kuzawadiwa trekta
“Sasa wale vijana wenye uwezo wa kuendesha bajaj walete vyeti na leseni
zao za udereva wa bajaj ili niwape kazi kwani hii bajaj inaanza biashara
haraka iwezekanavyo” alisema Manzi ambaye alionekana kujawa na furaha
ya pekee na kutumia fursa hiyo kuishukuru kampuni ya bia ya Serengeti
kwa kumwezesha kupiga hatua kubwa kimaisha.
WAKUFUNZI WA SENSA WAPIGWA MSASA
Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho akitoa neno la utangulizi kwa wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakati wa mafunzo ya
siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa . Mafunzo
hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) yalianza jana mjini
Dodoma.
|
Shairi kutoka kwa mdau Mroki Mroki:Kapumzike kwa amani Wille wa Ogunde
Kapumzike kwa amani Wille wa Ogunde
Salaamu wasomaji, Moyo naupiga konde,
Sihitaji hata maji, kama viazi mviponde,
Nimejawa na simanzi, Kifo cha kaka Ogunde,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Tusimlaumu Mungu, sote tulio waungwana,
Najua tuna uchungu, yowe ni kwamaulana,
Mola angetupa fungu, kifo siwe cha kijana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Twasema kasitukizwa, Wille kaenda kijana,
Alipo kuja hatukuulizwa, tulimwona tu mvulana,
Mungu we ndo muweza, kifo leo twakimbizana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Mwaka ule 74 machi saba, Wille ukaiona dunia,
Leo amegonga siku ya saba, ukamtwaa hii dunia,
Tena tarehe kumi na saba, Wille kaiga dunia,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Wille ulilia kaka, siku uliyo iona dunia,
Mpalule, Pinto,na Mroki, sasa zamuyetu kulia,
Wengi wanatafuta kichaka, lini nao watatwaliwa,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.
Pigo la wana habari, Tanzania na Afrika pia
Hakika kifo ni bahari, hakuna ajuae ilikoanzia,
Kifo ni jemedari, Wille amesha twalia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Salamu kawape jalia, wote walo kutangulia,
Mwakiteleko alotulia, na wote wana familia,
Wanahabari tunalia, Wille Ogunde kutangulia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Father Kidevu tamatia, nangoja nami kufuatia,
Siku itapo fikia, hakuna atakae bakia,
Kifo kitendawili, Mola ndie atakae kitegua,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.
Mroki Mroki a.k.a Father Kidevu
0717002303/0755 373999
MATUKIO KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZAZNIBAR
Mwakilishi wa Jimbo la Chakechake Omar Ali Sheheakiwa pamoja na
Mwakilishi wa kuteuliwa Panya Othman CCM wakiingia katika Ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi huko Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
Badhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakisikiliza kwa makini hoja
mbalimbali zinazotolewa ndani ya Baraza hilo huko Bweni Nje ya Mji wa
Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
WAFANYAKAZI BENKI YA UBA WAKIJIANDAA KWENDA KATIKA MAZOEZI KIGAMBONI AMBAKO PIA WALITOA MSAADA KITUO CHA HOPE FAMILY
ATCL yajipanga kuendeleza sekta ya usafiri wa anga
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limetangaza mpango
wakuungana na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) ilikutoa mafunzo mbalimbali
yatakayowezesha upatikanaji wa wataalam mbalimbali wa sekta ya anga.
Akizungumza katika sherehe yakuwaga wanafunzi 39 wa Chuo cha
Mafunzo cha Shirika la Ndege la Air Tanzania jijini Dar es Salaam wikiendi hii,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL,
Kapteni Lusajo Lazaro alisema mpango huo ambao utakuwa endelevu umewekwa kwa
makusudi ilikuhakikisha wataalam katika sekta ya usafiri wa anga wanakuwa na
ubora unaostahili hususani wakati huu ambapo sekta ya usafiri wa anga inakuwa
kwa kasi zaidi na kuvutia wawekezaji zaidi.
“Tumeshasaini nyaraka za makubaliano (MOU)na NIT
ilikuwezesha ufanisi wa swala hili. Nimatumaini yetu kuwa mpango huu utasaidia
kupunguza tatizo la upungufu wa wataalam katika sekta ya anga nchini.
”Bila pingamizi lolote kuwa sasa tutahitaji wataalam zaidi
ili kuboresha utoaji wa huduma zetu hususani katika kipindi hiki ambacho tumejikita katika
utekelezaji wa mpango wetu wa maendeleo
wa miaka mitano ambao unalengo la kuongeza safari na ndege nyingine katika miaka
michache ijayo,” alisema.
Lazaro akitoa maoni yake juu ya soko la pamoja la Afrika
Mashariki ambalo limefungua milango kwa biashara huria za bidhaa na huduma
ndani ya nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) alisema kuwa
kampuni yake imejipanga kutumia fursa hiyo ipasavyo.
“Soko hili huria la
pamoja litatengeneza fursa nyingi sana na tayari sisi kama shirika tumejipanga kuchangamkia
na kuzitumiua fursa hizo ipasavyo. Tupo katika mipango ya kuongeza safari zetu
zaidi na pale inapowezekana kutafanyakazi pamoja na mashirika makubwa barani.
Tunahitaji wafanyakazi wenye ujuzi na walio bora ambao watatusaidia kuleta
ushindani kama shirika,” aliongeza.
Kwa upande wake, mhitimu wa Chuo cha Mafunzo cha Mafunzo ya
Anga cha ATCL Yasmin Khanj akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake
waliohitimu alisema kuwa watatumia vizuri ujuzi wote walioupata katika chuo
hicho ilikuchangia maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini.
“Hii ni hatua kubwa
sana katika maisha yetu. Tunaiomba kampuni ya ATCL kutupa fursa ya kupata ujuzi
zaidi kwa kutupatia nafasi kwenye kampuni ili tuweze kupata uzoefu unaohitajika
ili tulete ushindani na kutoa huduma ipasavyo,” alisema.
Aidha, mkuu wa chuo cha mafunzo cha ATCL, Lawrence Mhomwa
alisema kuwa wahitimu hao baada ya kumaliza mafunzo yao yaliyojumuisha mada saba
katika chuo hicho zikiwa pamoja na huduma kwa wateja, usalama katika viwanja
vya ndege, uhudumu ndani ya ndege, usalama ndani ya ndege na mada
nyingine,wahitimu hao sasa wanauwezo wa kufanyakazi katika shirika lolote la ndege
.
Epiq Bongo Star Search yamaliza kazi mkoani Dodoma
Na Mwandishi Wetu Dodoma
PAZIA la shindano la Epiq Bongo Star
Search (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma limefungwa rasmi huku vipaji kibao
vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.
Kilichovutia
zaidi ni washiriki wa miaka 16 ambao walionekana kuimba vema na kuwa
kivutio hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village.
Akizungumzia shindano hilo Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo
Ritha Paulsen alisema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa
hasa idadi ya washiriki wasichana pia.
Alisema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza
kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012
ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji vya washiriki wa umri huo.
Katika
usaili huo kulikuwa na washiriki wa aina mbalimbali wakiwamo wanafunzi,
wafanyabiashara ndogondogo, vijana wa mitaani na wadau wengineo wa
muziki.
Kwa
kuthamini umuhimu wa akina mama na watoto mshiriki aliefika kuonesha
kipaji chake katika ukumbi huo alipewa nafasi ya kuimba ili aweze kuwahi
kuondoka.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla
mbali na kuvutiwa na ushiriki wa vijana waliojitokeza pia alihamasisha
upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa kituo cha damu mkoani Dodoma.
“
Kwa kupitia EBSS 2012 tunataka kuwafikia vijana sio tu katika muziki
bali pia hata katika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama
vile hili la kuchangia damu na mengineo” alisema Awaichi.
Washindi watakaopatikana watatangazwa
baadae katika vyombo vya habari. Baada ya Dodoma kwa sasa inafuata
Zanzibar ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe.
No comments:
Post a Comment