TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 22, 2013

Bunduki yatumika kuombea rushwa *Wananchi walalamika kubambikiwa kesi na polisi *Viongozi CCM wataka iundwe tume kuchunguza Papa asimikwa,atoa ujumbe mzito Kikwete aomboleza kifo cha trafiki Hukumu wafuasi a ponda Kituo kikubwa cha kuzalisha gesi kujengwa nchini KATUNI

MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:



Posted: 19 Mar 2013 11:41 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Tabora

BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora, wamelalamikia kitendo cha baadhi ya askari wa vituo vya polisi Usinge na Kaliua, kuomba rushwa kwa mtutu wa bunduki.
Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wamemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kusikiliza kilio chao na wachukulia hatua baadhi ya askari wanaofanya vitendo hivyo ili waweze kuishi kwa uhuru na amani.
Wananchi hao kutoka Vijiji vya Ugansa, Shela, Kombe, Maboha na Usinge, walitoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Usinge, Bw. Titus Kilomba.

Mkutano huo ulifanyika hivi karibuni kwenye Kijiji cha Ugansa, ambapo wananchi hao walidai kuwa, mbali ya kutishiwa kwa silaha ili kutyoa rushwa pia wamekuwa wakibambikiziwa kesi na askari.
“Tunamuomba Dkt. Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, atusaidie kutatua mgogoro kati ya askari na wananchi ambao umeanza kuvunja mahusiano wetu,” walisema.
Walidai kwamba askari hao wamekuwa wakiwanyanyasa wananchi hususani jamii ya wafugaji kwa kuwabambikia kesi kubwa kwa lengo la kutaka wapewe rushwa.
Mkazi wa Kijiji hicho, Bw. Ngidingi Lusumisha (67), alidai yeye walimbambikia fuvu la kichwa cha mtu na askari aliowataja katika mkutano huo (majina tunayo), ambao walikwenda nyumbani kwake na kudai wanamtilia shaka kuwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.
“Siku hiyo ilikuwa asubuhi, askari walikuja nyumbani kwangu wakaniambia nipo chini ya ulinzi wakidai wan mashaka na mimi hivyo wanahitaji kufanya upekuzi.

“Wakati wakiendelea kunihoji, kuna mtu ambaye nadhani alikujana na fuvu la kichwa cha mtu na kukiweka katika zizi langu la ngo’mbe ambapo wakati wakiendelea kunihoji, askari mmoja alitokea zizini akiwa na kichwa fuvu hilo na kudai nimekitoa wapi,” alisema.
Alisema askari hao walianza kumtisha na kumwambia “Wewe mzee sasa utaozea jela maana adhabu ya kukutwa na fuvu la binadamu mahakamani ni kunyongwa hivyo kama nina sh. milioni tano, wamuachie kwani kesi yake ni nzito sana.
Aliongeza kuwa, kutokana na maelezo ya askari hao aliogopa sana hadi kulazimika kuwalilia wakamshawishi awape sh. 200,000. ambazo alizito na kuwapa.

Hata hivyo, Bw. Lusumisha alidai kumshukuru Mwenyekiti wake wa Kijiji cha Shela, Bw. Martin Juma kwa kumshauri alifikishe suala hilo kwa Bw. Kilomba ili aweze kulifuatilia zaidi.
Kwa upande wake, Bw. Kilomba alisema, amekuwa akipokea malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu
vitendo askari wa Kituo cha Polisi Kata ya Usinge ambao
wanadaiwa kuwanyanyasa raia na kuwalazimisha kutoa
rushwa kwa mtutu wa bunduki.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Kombe, wilayani humo, Bw. Ikungile Mwandu, alidai mtoto wake Bw. John Ikungile (25), alipigwa risasi na askari wa Kituo cha Kaliua, kwa madai ya kuchunga ng'ombe katika shamba la jirani la kusababisha hasara ya sh. milioni 150.

Alisema baada ya askari hao kufika nyumbani kwake, walimuweka mtoto wake chini ya ulinzi, kumfunga pingu ambapo wakiwa njiani kumpeleka Kituo cha Polisi, walimtaka anyooshe mikono juu na kumpiga risasi katika mkono wake wa kulia.

Akizungumzia mkasa huo, Bw. Ikungile alisema “walinipiga risasi katika mkono wa kulia, baada ya kuanguka na kutowa damu nyingi walinifungua pingu na kukimbia wakiwa na pikipiki.

“Baba aliporudi alinipeleka polisi ili tukachukue PF3 ili niweze kwenda kutibiwa hospitali lakini baada ya kufika kituoni hapo, waliniambia tukienda hospitali nisiseme kuwa nimepigwa risasi eti, niwaambie nimechomwa na kitu chenye ncha kali,” alisema.

Mkuu wa Mkoa huo, Bi. Fatuma Mwassa, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alikiri kupokea malalamiko hayo na kuwa, tayari amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Anthony Rutta ashughulikie suala hilo ili wahusika waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kijeshi.

“Taarifa hiyo ninayo...tayari nilishamwagiza RPC awachukulie hatua askari wote wanaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo,” alisema.

Naye Kamanda Rutta alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo alidai kuwa, hana taarifa yoyote kuhusu hivyo kupingana maelezo ya Bi. Mwassa ambaye alisema tayari alishampa maagizo.

“Nani kakuambia taarifa hizo...mimi sifahamu chochote kuhusu jambo hilo ndio kwanza unanipa taarifa ngoja nizifanyie kazi” alisema Kamanda Rutta.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo, Bw. Iddy Amme, alisema chama hicho hakiwezi kuvumilia vitendo vya aina hiyo vinavyofanywa na askari wanaokiuka madili ya kazi zao.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, alishituka sana na kuahidi kulifikisha suala hilo katika uongozi wa CCM Taifa ili liweze kushughulikiwa kikamilifu.

Katibu wa CCM wilayani Kaliua, Bw. Simon Yaawo, alipendekeza iundwe tume ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo kwa wahusika.

“Mimi nipo tayari kutoa ushahidi sehemu yoyote kama nitahitajika maana tumechoka na matukio kama haya, mimi mwenyewe nilimuona yule kijana aliyepigwa risasi (Ikungile).
Posted: 19 Mar 2013 11:35 PM PDT
ROME, Italia

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I, jana amesimikwa rasmi kutumikia wadhifa huo na kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi mbalimbali, kuwalinda wanyonge na masikini.

Papa Francis I, alitoa wito huo katika misa maalumu iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma ambapo katika misa hiyo, alivalishwa pete ikiashiria sasa amekuwa Baba Mtakatifu wa 266.

Kwa mujibu wa Kituo cha Utangazaji cha CNN, Papa Francis I, alizunguka katika viwanja hivyo akiwa kwenye gari la wazi na baada ya kuteremka, aliwabariki mahujaji mbalimbali.

Hata hivyo, inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.6  waliudhuria sherehe hiyo huku mamilioni wakiifuatilia kupitia vyombo vya habari wakiwemo viongozi 130 kutoka duniani kote.

Papa huyo alichaguliwa na Mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo Februari 28, mwaka huu.

Papa Benedict XVI alikuwa papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya kanisa hilo akidai umri wake wa miaka 85, asingeweza kutekeleza kikamilifu majukumu yake.

Katika hatua nyingine, Papa Francis I, anaonekana kuwa na mtazamo tofauti na watangulizi wake.
Posted: 19 Mar 2013 11:34 PM PDT
Na Jesca Kileo

RAIS Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, kuomboleza kifo cha askari WP 2494 Koplo Elikiza ambaye amepoteza maisha kwa kugongwa na gari juzi mchana katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam.

Koplo Elikiza aligongwa wakati akimsimamisha dereva gari ambalo alijiunga na msafara wa Rais Kikwete na kupewa amri ya kusimama badala yake akamgonga na kusababisha kifo chake.

“Nimepokea taarifa za kifo hiki kwa mshtuko na huzuni nyingi, nimejulishwa kuwa aligongwa na gari akiwa kazini katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam, wakati akiongoza msafara rasmi.

“Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kwa Koplo Elikiza kupoteza maisha akiwa kazini kwenye utumishi wa jeshi lake
na nchi yake wakati Taifa bado linaendelea kuhitaji sana
nguvu kazi yake,” alisema Rais Kikwete.

Alimtaka IGP Mwema kumfikishia salamu zake kwa familia ya marehemu kuwa yupo pamoja nao.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema bado linaendelea kumsaka dereva aliyesababisha kifo cha askari huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Posted: 19 Mar 2013 11:32 PM PDT
Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kesho inatarajia kutoa hukumu ya washtakiwa wa kesi ya kufanya maandamano haramu kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), inayowakabili wafuasi 53 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Sundi Fimbo, anayesikiliza ambapo upande wa mashtaka ulikuwa ukiwakilishwa na wakili wa Serikali, Bernad Kongola, wakati upande wa utetezi unawakilishwa na wakili Mohamed Tibanyendela.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi saba na vielelezo mbalimbali ambapo upande wa utetezi, washtakiwa hao walijitetea wenyewe.

Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya maandamano haramu Februari 15 mwaka huu kwenda kwa DPP, licha ya Jeshi la Polisi kukataza kufanyika kwa maandamano hayo.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa hao wanadaiwa kufanya maandamano haramu kwenda katika Ofisi ya DPP ili kumshinikiza atoe dhamana kwa Shekhe Ponda na mwenzake Shekhe Mukadamu Swalehe.

Katika maelezo ya awali, washtakiwa hao walidaiwa kuwa awali polisi walitoa zuio la maandamano hayo lakini walikaidi ambapo siku ya tukio, polisi waliwaamuru kutawanyika katika mikusanyiko waliyokuwa wakiifanya na kukaidi ndipo wakakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Katika maelezo hayo, mshtakiwa wa kwanza Bw. Salum Makame, alikiri kukutwa na kisu na kipaza sauti lakini akakana kuwa hakuwa mfuasi wa Shekhe Ponda.

Posted: 19 Mar 2013 11:31 PM PDT

OSLO, Norway

KAMPUNI za Statoil na BG Group, zinatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 10 kujenga kituo cha kuzalisha na kusafisha
gesi ya asili nchini Tanzania ili kuiuza Asia.


Hatua hiyo inatokana na Kampuni ya Statoil kutoka nchini Norway, kugundua uwepo wa gesi nyingi Pwani mwa Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Uchimbaji wa kampuni hiyo, Bw. Tim Dodson, aliyasema hayo juzi kutokana na utafiti waliofganya kwenye Bahari ya Hadi na kugundua uwepo wa gesi yenye
ujazo wa trilioni nne hadi sita.

“Tunafanya kazi na BG ili kuja na makubaliano ambayo yataweka mambo sawa katika maeneo husika, tunapaswa kukubaliana na mamlaka husika nchini Tanzania wakati tunaingia katika hatua
ya pili,” alisema Bw. Dodson wakati akizungumza na Shirika
la Habari Reuters.

Aliongeza kuwa, gesi waliyoigundua katika bahari hiyo huenda ikawa na ongezeko kubwa kwani rasilimali hiyo inaonekana ni nyingi nchini Tanzania ambapo kwa mujibu wa Reuters, BG imevutiwa na ushirikiano uliopo kati ya kampuni hiyo na nyingine ya Ophir Energy.

Mwanzoni mwa wiki hii, Kampuni ya BG ilitangaza utafiti wake umefikia katika hatua nzuri za uchimbaji wa gesi Tanzania.

Katika hatua nyingine, Wanajeolojia kutoka nchini Marekani wanadai gesi ya asili inapatikana kwa wingi katika mwambao wa Tanzania, Kenya na Msumbiji kuliko Nigeria ambayo ni nchi kubwa kwa uzalishaji wa nishati ya mafuta.

Reuters liliongeza kuwa, Afrika Mashariki imeanza kuvutia watu katika sekta ya mafuta kutokana na uhitaji mkubwa wa gesi katika Asia.

“Statoil na BG katika ujenzi wa kiwanda hicho, tutakuwa tunapitia japo hatua mbili, kwanza kuiandaa gesi katika kitalu namba mbili kinachosimamiwa na Statoil na kitalu namba moja cha BG kwa nyongeza kutokana na ujazo wa 10-13 (tcf) ambao tunao.

“Kama ujazo huo utafikia 20 (tcf), wataangalia nini kifanyike ili
gesi hiyo iweze kuandaliwa vizuri, kiasi hicho cha fedha kitatumika katika shughuli hiyo na uwekezaji utafanyika ndani ya miaka mitatu, kabla ya mwaka 2016,” alisema Bw. Dodson.

Wakati huo huo, Mwandishi Peter Mwenda anaripoti kuwa, Wizara ya Nishati na Madini, imeingia mkataba wa utafiti wa gesi, mafuta na Kampuni ya JACKA Resources Ltd ya Australia.

Waziri wa Wazara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa, watafiti hao wameingia mkataba wa miaka 11 ambao umegawanyika sehemu tatu.

Alisema utafiti  huo utafanyika katika eneo la Ruhuhu mkoani Ruvuma, Njombe na utakuwa wa miaka minne kwa kila awamu.

Aliongeza kuwa, awamu ya kwanza ya mradi huo kama mafuta na gesi itagundulika, kampuni hiyo itachukua asilimia 50 ya mapato na serikali ya Tanzania asilimia 50.

Alifafanua kuwa, baada ya hapo Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania nchini (TPDC), nayo italipa kodi asilimia 30 na kampuni hiyo italipa asilimia 30 ambazo zitatokana na mapato yao ya asilimia 50.

Awali akizungumza katika mkataba huo, Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Scott Spencer, alisema wao ni wazoefu katika kazi hiyo kwani waliwahi kufanya utafiti katika Bara la Afrika na kufanikiwa kugundua mafuta ya petrol kwenye Ziwa Albart nchini Uganda.

Alisema mradi huo utagharimu dola milioni 20 hadi 50 ambazo ni sawa na fedha za Tanzania sh. bilioni 80.
Posted: 19 Mar 2013 11:29 PM PDT

No comments:

Post a Comment