Chuo Kikuu cha Dar es salaam ni
miongoni mwa taasisi mbalimbali nchini zilizoitikia wito wa kudhamini fainali
za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 ikiwa ni baada ya kupata taarifa ya kuwapo
kwa mapungufu mbalimbali ambayo yamepelekea kusogezwa mbele fainali zake kutokana
na upungufu na ufinyu wa bajeti kiasi cha shilingi milioni 170 zilizotokana na
kushindwa kwa baadhi ya wadhamini kutimiza ahadi zao.
udhamini huo ambao unalenga moja
kwa moja kwa washindi, ni pamoja na kulipiwa gharama za ada ya masomo katika
musimu wa 2013/14 kozi ya uandishi wa
habari katika chuo kikuu cha dar es
salaam ,school of journalism and mass communication( sjmc).
akizungumza jijini dar es salaam
kuhusu udhamini huo , rais wa miss utalii tanzania, gideon chipungahelo alisema
kwamba ni jambo la kupendeza kwa kuwa kuna
ufinyu wa bajeti katika kukamilisha fainali za taifa za miss utalii
tanzania.
“tunashukuru kuona taasisi kama
chuo kikuu cha dar es salaam kinajitokeza kuunga mkono juhudi za miss utalii
tanzania katika harakati za kufanikisha fainali za taifa za miss utalii
tanzania 2012/13 ambazo zinalenga kuutangaza utalii wa tanzania, ikiwa ni
pamoja na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho kina historia ukilinganisha na
vyuo vingine katika ukanda wa afrika mashariki na kati, hivyo nazidi kusisitiza
kwa wadau, taasisi na makampuni binafsi kujitokeza kuunga na kusaidia juhudi
hizi ili fainali za mwaka huu ziwe tofauti na fainali za miaka ya nyuma”
alisema chipungahelo
Na
kuongza kwamba ahadi kwa wadau na wapenzi wa mashindano haya iko pale pale, kwa
kuwa dhamira ipo na nia ya kulifanya shindano la Miss Utalii Tanzania kuendelea
kuwa bora na lenye mafanikio makubwa kuliko jingine lolote nchini na afrika iko
pale pale, na hili litadhihirika wakati wa fainali kuu ya mashindano mwishoni mwa mwezi huu, hivyo wadau,wafanyabiashara,
makampuni binafsi na ya umma, hasa ya kizalendo watakaojitokeza siku hiyo watashuhudia
burudani ya aina yake kutoka kwa Warembo mbalimbali wanaowakilisha Mikoa yao,na
wawakilishi wa Kanda za Vyuo Vikuu Tanzania bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment