Aliyekuwa
Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na
uokozi na Bw. Naamini Hendry Sangiwa pamoja na Mkandarasi na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa
leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya
wilaya ya Ilala. Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Hassan.
Washtakiwa tajwa hapo juu walishtakiwa kwa makosa 7 yakiwemo Matumizi
Mabaya ya Madaraka, Kutumia Nyaraka Kumdanganya Mwajiri kinyume na
kifungu cha 22 na 31 mtawalia vya Sheria ya kuzuia na Kupambana na
Rushwa Na.11/2007, Kughushi Nyaraka kinyume na Kifungu cha 333, 335 (d)
(1) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, na kuisababishia
Serikali hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza, Kifungu
cha 57(1) na 60(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200.
Mnamo mwaka 2009 Serikali ilitoa zabuni ya Ujenzi wa uzio wa Chuo cha
Zimamoto na Uokozi kilichopo Mbopo Bunju katika Manispaa ya Kinondoni
Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Kiareni Investment Ltd (Mzabuni), ilipatiwa zabuni hiyo na kulipwa Kiasi cha Shilingi 81, 963, 360/=.
Hata hivyo taratibu za utoaji zabuni hazikufuatwa, na Mzabuni ambaye ni
Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, alifanya kazi yenye thamani ya kiasi
cha Shilingi 13, 784, 652/= tu kati ya fedha yote aliyolipwa.
Ili kuwezesha malipo ya Shilingi 81, 963, 360/= kulipwa pasipo kazi
kukamilika, Washtakiwa walitoa zabuni kwa Mkandarasi pasipo Mkataba
(LPO), na Kughushi Hati ya kuonesha kazi imekamilika (Certificate of
Works Completion).
Washitakiwa wote watatu walifikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwanzoni mwa mwaka 2014 na kusomewa mashtaka
yao Mbele ya Hakimu Mkazi Hassan, ambapo washitakiwa walifunguliwa kesi
ya Uhujumu Uchumi No. 06/2014.
Upande wa Jamhuri katika Kesi
hii uliwakilishwa na Wakili STANLEY HILMAR LUOGA akisaidiana na Wakili
EMMANUEL JACOB, wote waendesha Mashitaka wa TAKUKURU Makao Makuu.
Upande wa washtakiwa wote waliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea MDUMA.
Upande wa Jamhuri uliita Mashahidi 7 na kupeleka vielelezo 21 ili
kuthibitisha kesi dhidi ya washtakiwa. Upande wa washtakiwa hawakuita
shahidi hata mmoja walijitetea wenyewe.
Mshitakiwa wa kwanza
Dotto Salehe Mgogo, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Mafunzo wa Wizara ya
Mambo ya Ndani katika idara ya Jeshi la Zimamoto na Uokozi alifariki
dunia mwaka 2014 baada ya kusomewa mashitaka na hivyo Mashitaka dhidi
yake yalifutwa kwa mujibu wa sheria.
Kufuatia kifo cha
Mshitakiwa wa kwanza, Mshitakiwa wa Pili Bw. Naamini Hendry Sangiwa
ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Katika Jeshi la
Zimamoto na Uokozi alikuwa anakabiliwa na makosa manne (4) ambapo makosa
mawili ni ya Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kughushi na Kuisababishia
Serikali Hasara, ametiwa hatiani katika makosa yote mawili ya Matumizi
ya Madaraka na kupewa adhabu ya kulipa faini ya Tshs.300, 000 kwa kila
kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka kama atashindwa kulipa faini, kwenda
jela miezi 6 kwa kila kosa.
Katika Kosa la Kughushi Nyaraka, Mshtakiwa ametiwa Hatiani na Kuamriwa kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda wa miezi 12.
Mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw. Webu Manoth Masawe, ambaye ni
Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd,
anakabiliwa na Kosa moja la Kuisababishia Serikali Hasara.
Mahakama imemtia hatiani na kumpa adhabu ya kwenda Jela miaka mitatu (3)
pamoja na Kuirudishia Serikali kiasi cha Shilingi 67, 913, 748/= ikiwa
ni hasara aliyoisababishia Serikali.
IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
24 MACHI, 2016
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
24 MACHI, 2016
............Comments.................
Muddy Muddy Kosa la kughushi lina exception kumbe.ninavyofahamu nikifungo cha miaka saba hiyo hukumu ya kughushi ni JIPU
Kayanda Nurdin komaa komaa,mhe............!!
مجوو سعيد ابراهيم Endelea kuwanyoosha mweshimiwa magu
Abbs Chris Maheri Laki 3 tuu kwa kosa la matumizi mabaya? Afu matumizi hayo yamepelekea hasara ya 67mil.Izi sheria ziangaliwe upya.
Abeid Mbano Adhabu
hazitoshi Hawa mahakim na majaji wanabidi wafatiliwe hata kama sheria
inataka mahakama kuwa huru lakini nivyema kuvunja sheria kwaniaba ya
watanzania walio wengi mfano mtu anaiba billion 10 unaenda kumuhukum
miaka 3 sasa hata mimi ukiniambia unanipa billion 10 halafu nikafungwe
miaka 3 nakubali namaanisha adhabu zinanzotolewa hazitoshi hata kidogo
lazima mtu afungwe miaka 20 au 30 ndio itakua fundisho
Abeid Mbano Naomba nitoe maoni zaidi 0714297033
Ally Khatibu BabaNeyuu Hii.sheria
mbona siielewi mtu anahujumu mabilioni anafunga miaka michache mfano
miaka 3..mwingine kagushi majina hewa ya wanafunzi kaipatia serikali
hasara ya milion 4 kafungwa miaka 23...sielewi
Henry Sufa A
Luta Continua....waliokuwa wanajilipa mishahara hewa warudishe pesa
zetu au kufilisiwa (sijui kama sheria inaruhu) na baada ya hapo
gerezani.
Chande Kijuni dah
mbona adhabu ndogo sana kias hiki? kwa nini lakini? kuisababishia
hasara serikali ni kosa kubwa mno adhabu ndogo hiyo bkra ijengwe tu hiyo
mahakama ya mafisadi
Mnyamani Amiri Serekali
bado muangalia na kesi ya Askari wa Zima moto waliostaafishwa kinyume
cha taratibu. Wale wazee wamefanyiwa figisu, wapewe haki Yao.
Mickah Peter Yule wa milungi kahukumiwa kifungo chamaisha,hyu matumizi mabaya ya ofisi lak 3,anyway kuna siku ambo yatabadilika
Sohail Thakur Very good..wako wengi tu kila kona kama hao..fuatilieni
Agano John Ng'asi Kama
sheria ndivyo zinavyosema ,basi waacheni wapete.pia nadhani adhabu hizo
ziliwekwa na watu ambao walikuwa wanafikiria kuwa nawao yanaweza
kuwakuta so adhabu ziwe ndogo.
Jozee Simba Kama mtu kakamatwa na mirungi huko Kilimanjaro kafungwa maisha je kuhujumu uchumumi inakuwaje? Duuuh Mimi napita tuu
James Bombi angekua mwizi wa cm au tv miaka 5 au 10 jela duh! kwel noma
Izack Musa Sijaridhika, wote walishirikiana kuhujumu nchi, je hukumu si sahihi
Wafungwe kama yule wa ngorongoro
Wafungwe kama yule wa ngorongoro
Deusdedith Rwebangira Pccb
ihundwe upya na kufuta iliyopo imekuwa sehemu ya tatizo kidonda sugu
jamii inakilalamikia hawahfanyi kazi wanaishia vikesi vya watendaji wa
vijiji kifutwe kiundwe upya.
Sadock Mahanga Safi sana kwa kazi nzuri. Ila pia mngewafilisi kabisa iwe fundisho kwa wengine.
Naboth Longo kazi
nzuri ila adhabu ni ndogo sana, tunaomba sheria ziangaliwe upya hasa
wakati wa kuaandaa mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi. adhab
zinatakiwa kuwa kubwa.
George Mzule Upuuz uleule
Samweli Njama Hivi
jamani huo sikutufanya watoto huyu mwenye faini silaki tatu makosa
matatu la tisa sasa kala shiringi ngapi asiweze kutoa faini ahsanteni
sana kwa kutuona wajinga.
No comments:
Post a Comment