TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 10, 2012

MAANDALIZI MASHUJAA MUSICA SIKU YA IJUMAA YAPAMBA MOTO

 Rais wa Bendi ya Mashujaa Muzika, Kajo Litungu,
 Kutoka kulia ni wacheza shoo wa Mashujaa Musica, Jack Spoila, Baby White, Salma Mwiba, Salma Teketeke, Suzy Mashujaa, na Aisha Twiga, wakati wa maandalizi na mpambano wa siku ya Ijumaa dhidi ya maasimu wao wakuu Mapacha watatu na Extra Bongo, katika Ukumbi wa Bussiness, Barabara ya Mwenge Victoria.
 Baadhi ya wanamuziki wa Mashujaa Musica
 Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Kajo Litunguru(kushoto) akiongoza wenzake Jado Fid(Jembe) kulia, Pasia Budansi Black Bell wa pili kulia na Raja Radha, wakati wa mazoezi leo
 Wacheza Shoo wa Mawashujaa Musica, Juma Nyamwela(kushoto),Mpasi M-Pesa, na Kelvini Sayona Kill kuu
 Mcheza shoo wa Mashujaa Musica, Salma Teketeke(Mjukuu wa Babu)
 Wapiga Ngoma wa Mashujaa Musica, Sele Kadanse(kulia) na Dulla Ngoma
 Mpiga Kinanda wa Mashujaa Musica, Fredy Manzaka(Picha Zote na Shaaban Mpalule)

-WANAMUZIKI WAKESHA MAZOEZI KUJINDA DHIDI YA WAPINZANI WAO MAPACHA WATATU/EXRABONGO.

-JADO FID (JEMBE), ASEMA LENGO  LIMETIMIA

Aliyekuwa Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica ,Jado Fid(Jembe)aliyejiudhuru wadhifa huo wa Madaraka baada ya kumalizika mwaka 2011, amesema kwamba, ameamua kupisha nafasi hiyo ili kuweza kutoa changamoto kwa wanamuziki wengine kupata uzoefu katika idara ya Uongozi kwenye Muziki.
Jado ambaye amekuwa Raisi wa Bendi hiyo tangu alipovuliwa Urais, Eliston Angai, mwaka juzi, ni kati ya wanamuziki wanaotakiwa kuigwa kutokana na Moyo wake wa Ujasiri na Utekelezaji wa Maadili ya Uongozi kwa wanamuziki, baada ya kuitoa katika hali ngumu na yenye misukosuko mingi bendi hiyo hadi alipoamua kustaafu ngazi ya juu ya Uongozi katika bendi hiyo.
"kwa ujuma nimeamua kuwapisha wengine pia ili kuwepo na mabadiliko kimziki, maana uongozi ni sawa na jalala la takataka, watu wengine wakisikia mtu ni kiongozi bila shaka wanadhani kwamba yupo katika hali ya furaha, amani, na hata kuwa mkamilifu kwa kila jambo, kiukweli uongozi ni mzigo, tena unapoona mtu kakaa kwa kipindi kirefu katika kuongoza anatakiwa kuhesimiwa sana, maana hakuna kazi ngumu kama kuongoza binadamu, tena watu wazima, hakika baada ya kusimamishwa Alistoni kwa wakati huo na kisha kubebeshwa nafasi kama ile, ilibidi nifanye kazi ya ziada, ukizingatia ndo tulikuwa katika kutengeneza nyimbo na Albamu za Bendi, so kiukweli namshukuru Mungu, aliweza kuniongoza vizuri hata kuweza kuelewana na kila mmoja wetu wakati wote wa Uongozi wangu, alisema Jado
Ukumbuke kwamba kati ya Nyimbo zinazovuma kwenye kundi la Mashujaa ni ule wa Safari ya Vikwazo, ambao ndiyo unabeba Ujumbe katika Albamu hiyo, Mtunzi ni Jado Fid, ambaye kwa sasa Mashabiki wamempachika jina la JEMBE au Mkapa, na kwa sasa akiendelea kutesa na nyimbo katika baadhi ya Vituo vya Radio na TV, Ukumu ya Mnafiki.
Siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Business uliopo eneo la Victoria, kutawashwa moto kutokana na Bendi tatu kubwa kuwasha moto ndani ya jukwaa moja, yaani MASHUJAA MUSICA, EXTRABONGO,na MAPACHA WATATU.
AKIZUNGUMZIA onyesho hilo, Rais Mteule wa Bendi hiyo, Kajo Litungu, alisema maandalizi yanakwenda vizuri ambapo wanategemea kuwasha moto mkubwa kwa lengo la kuwapa raha mashabiki wao kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
kundi hilo linaundwa na wacheza shoo, Jack Spoila, Baby White, Salma Mwiba, Suzy Joshua, Aisha Twiga, Juma Nyamwela, Mpasi M-Pesa, Kelvini Sayona Kill kuu, Sweety Baby, wapiga vyombo, Fredy Manzaka(Kinanda), Sele Kadanse(Ngoma), Dulla Ngoma, Amosi Nabii Sollo, Profa Kariakoo(Sollo)Baba Isaya Sharobaro(Risimu), Tonton Drama, Kamode Besi na Kassimu Bezi
Waimbaji wanaowakilisha kundi hilo nji pamoja na Jado Fid(Jembe), Kajo Litungu Dasia, Pasia Budansi Black Bell, Raja Radha, Jimmy Adori, Masudi Namba ya Mwisho, Salasini na Tatu, na upande wa Malapa ni pamoja na Ibrahimu Milinda Nyeusi, Yaniki Noha(Sauti ya Radi), na  Zidane Taarifa ya Habari.
chini ya Uongozi wao Makini ukiongozwa na Meneja Hamisi Promota, pamoja na jopo la kamati ya Ufundi, Makala Mbage (Mwanashinyanga)Prince Twalib,Yohana Malasusa na  Mamaaa Sakina,
Kiingilio katika Onyesho hilo kwa mujibu wa Kajo itakuwa shilingi Elfu saba 7,000/= mlangoni.

Monday, January 9, 2012

meli ya mizigo NZ Rena splits baada ya kupata dholuba baharini Safi-up






pwani katika New Zealand baada ya meli ya mizigo kuzama katika pwani stranded  ambapo mgawanyiko wa vipande wiliwi ulitokea. na inakadiliwa na Maritime New Zealand  kwamba vyombo mbali mbali vya na contena zilizokuwa ndani ya meli hiyo inayofikia 150 na watu wengi inasadikiwa  kuzama.
Kuosha vyombo wameanza ashore

Nigeria mgomo wa mafuta na kizaazaa na maandamano







Mgomo nchini Nigeria juu ya kuondolewa kwa ruzuku na kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli huleta uchumi kusimama, na kusababisha vifo vya watu tatu katika mapigano na polisi.

MATUKIO YA PICHA KATIKA MCHEZO WA MAN U DHIDI YA MAN CITY

 Wachezaji wa MAN -U, Wakishangilia Ushindi dhidi ya Man City wa 3-2
 Mchezaji wa Man City, akijaribu Kumzuia Mchezaji wa Man U, nani
 Wachezaji wa West Hamu wakitazama kama kuna dalili zozote za Mpira kutinga wavuni
 Mwamuzi alikuwa na wakati Mgumu wakati wa kuamua tukio, wakati Mchezaji wa Chelsea akionyesha tendo la kushangilia mpira huo

Mchezaji wa Chelsea (TORES) chini akijaribu kulalamika baada ya kuchezewa faulo
Wachezaji wa Man U, Paul Scholes wakifanya mabadiliko dhidi yake ya Nani, wakati wa mchezo dhidi ya Man City.

Henry Awahamasisha wachezaji wa Arsenal kushinda kombe la FA

Thierry Henry aonyesha ushujaa katika mchezo wake wa kwanza baada ya kurejea Arsenal katika mechi zake saba anazotarajiwa kucheza, ambapo leo kafanikiwa kuifunga timu ya Leeds katika Kombe la FA raundi ya tatu kwenye Uwanja wa Emirates 1-0
Thierry Henry made the perfect return to Arsenal when he emerged as a substitute to score a late winner in the FA Cup third-round tie against Leeds United.

Henry, back in Arsenal colours for the first time since he left for Barcelona in 2007, scored his 227th goal for the club with 12 minutes remaining amid emotional scenes at the Emirates.
The 34-year-old - back at the club where he was recently honoured with a statue on a two-month loan from New York Red Bulls - had only been on 10 minutes when the magical moment arrived.
Henry took a pass from Alex Song in his stride in the area before steering a composed, angled, right-footed finished tantalisingly out of the reach of Leeds United keeper Andy Lonergan.
It finally broke the stubborn resistance of Leeds and was the signal for an outpouring of emotion as Henry pumped his chest in celebration after racing to hug his mentor Arsene Wenger on the touchline.
Arsenal keeper Wojciech Szczesny raced the length of the field to join the celebrations while Henry later indulged in a spot of impromptu cheerleading as he urged the supporters who worship him to even greater backing for Arsenal in the closing stages.
It was the perfectly scripted finale to a contest that needed Henry's Midas touch against a Leeds side who battled in a manner that did manager Simon Grayson and their magnificent travelling support great credit.
At the final whistle, with the first task of his temporary return to the club completed, Henry raised his arms to the heavens before falling into the arms of his Arsenal colleagues and taking the acclaim of an elated crowd.
Henry's presence, even on the bench, enlivened the stadium when he came out to warm up and later when his name was announced to rapturous applause.
And the 45 minutes that followed only increased the appetite and anticipation for his return as Arsenal dominated but failed to breach a resilient and well-organised Leeds defence.
With leading scorer and captain Robin van Persie rested, attacking duties fell to Andrey Arshavin and Marouane Chamakh, the pair combining in the opening moments only for the Russian to fire wildly over the top.
Sebastien Squillaci then headed narrowly wide and Aaron Ramsey was unable to navigate a way around Lonergan after he was played into the area by Arshavin.
Leeds United's big chance, in a half they spent mainly on the retreat, came when Luciano Becchio found space in the box but shot wastefully off target.
Arsenal's defensive resources have thinned out in the face of mounting injuries - and they were depleted further before the interval when Francis Coquelin pulled up with a hamstring problem and was replaced by Nico Yennaris.
The momentum remained with Arsenal after the break as Lonergan saved well low to his left from Mikel Arteta after the Spaniard was set up by Chamakh, and Arshavin fired across the face of goal after picking up Zac Thompson's misplaced pass.
Henry's increasingly energetic sprinting along the touchline drew a loud reaction from Arsenal's fans and he was finally introduced with 22 minutes left, replacing Chamakh. Theo Walcott also came on for Alex Oxlade-Chamberlain.
Henry was given a hero's welcome as he set about the business of attempting to break down a Leeds side proving as stubborn as they had been here at the same stage of the FA Cup last season.
And the moment Arsenal had been waiting for came with 12 minutes left as Henry gathered Song's pass in his stride before sparking scenes of ecstasy on and off the pitch with a perfect finish.
Leeds refused to be distracted by the euphoria and almost snatched a replay in the closing stages as Szczesny saved well from substitute Mikael Forssell.
This, however, was Henry's night and Henry's story. Now Arsenal fans will hope he can write fresh chapters before returning to the United States.
 



Mashabiki wa Manchester United katika kusherehekea ushindi wakati wa kufuta majeraha ya kufungwa na Manchester City. Picha: PA


Mchezaji Scholes aliyeingia dakika za kipindi cha pili, alitajwa kwenye benchi kwa ajili ya mchezo dhidi ya City.
 
 

WHITE BAD THE KILLER -MBIONI KUKAMILIKA

Msanii wa Filamu za Kitanzania(Shabani Swarehe)maarufu kama SHABAX analotumia kwenye sanaa,(kulia), akiwa na msanii mwenzake (Zainabu Mohame) maarufu kama TINA, wakionyesha hali ya kutoelewana wakati wa Mazoezi ya Kundi hilo Lenye Makazi yake Tabata Liwiti, jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Shaaban Mpalule).
Filamu ya kitanzania yenye Mandhali ya kutisha na yenye mauaji yanayosisimua, Jambazi mkubwa ambaye ni msanii wa maigizo ya kuchekesha(Comed), Pembe, na wengine chipukizi , Dulla Nguvu, Moko , Shabax ambaye ambaye ameigiza kama jini muua wenye kudhulumu, wenye kuua watu, mlipa kisasi mtetezi wa Watu, na wengine wengi.
akizungumzia Filamu hiyo msanii Shabax, amesema kuwa filamu hii ni nzuri, Baada ya kucheza filamu ya Maisha ya Damu ambayo iko sokoni muda mrefu, baada ya kucheza kama jambazi(Iddi), "kikubwa ndugu yangu mwandishi, ninawambia watu wakae mkao wa kupata madhali ya kusisimua kutokana na filamu hii kuwa bora na iliyoandaliwa kimataifa, ukilinganisha na filamu zingine zinazotolewa na wasanii wa hapa nchini Tanzania" alisema Shabax
hata hivyo baadhi ya watu ambao walikuwa awadhanii kama msanii mwenzao Shabax anaweza kuigiza kwa kiwango cha hali ya juu wameshangazwa kutokana na ushirikiano baina yake na Msaanii wa COMEDI,  Pembe kuwa wa hali ya juu.
Filamu hiyo ambayo imehekitiwa sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam, ikiwemo Maeneo  ya Tabata, Vingunguti, Segerea, Banana, imenakishiwa madhali ya kuvutia kitendo kinachoionyesha kana kwamba imeratibiwa na kuhekitiwa nje ya nchi.

Serikali leo imetoa tamko la hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi 2011,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo,(kulia) akifafanua jambo kuhusu Tamko la Serikali juu ya Hatma ya Wanafunzi waliofutiwa Matokeo ya Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2011, kushoto ni  Kaimu Kamishina na Mkuu wa Idara ya Sekondari, Charles Philemoni, iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Elimu Dar es Salaam leo.(Picha na Shaaban Mpalule).

Serikali leo imetoa tamko la hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi 2011, iliyofanyika makao makuu ya wizara ya Elimu Dar es Salaam leo, akizungumzia sakata hilo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema kuwa kati ya wanafunzi 983 545 ya waliofanya mitihani, 567,767 sawa na asilimia 58.28 wamefaulu mtihani huo, na kwamba kati ya wanafunzi 9,736 wamefutiwa matokeo kutokana na kubainika kufanya udanganyifu



Monday, January 2, 2012

Youssou N'dour atangaza kuwania urais

Mwanamuziki mashuhuri wa Senegal Youssou N'dour atangaza kugombea urais dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade. 

Msimamo wa Ligi Kuu ya England

MTGPNT
1Man City193745
2Man Utd193245
3Tottenham181539
4Chelsea201437

5Arsenal20836

6Liverpool19934
7Newcastle19130
8Stoke20-929
9Norwich20-525
10Everton18-124
11Swansea20-323
12Aston Villa20-423
13Fulham20-423
14West Brom19-822
15Sunderland19121
16Wolves20-1417
17QPR20-1617

18Wigan19-2015
19Blackburn20-1414
20Bolton19-1913

SHEREHE ZA MWAKA MPYA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE

 
Usiku wa kuamkia tarehe 1 Januari 2012, Jumuiya ya Watanzania, maafisa wa Ubalozi pamoja na waalikwa kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Balozi wa Malawi na Balozi wa Ethiopia nchini Zimbabwe walihudhuria hafla ya kukaribisha mwaka mpya.
katika picha ya juu Mhe. Balozi Adadi akishereheka na watanzania.Mhe. Balozi Adadi akiteta jambo na wageni wake ambao ni Balozi wa Malawi na Balozi wa Ethiopia.
Watanzania na waalikwa wengine wakipata chakula sambamba na kuukaribisha mwaka mpya. katika Ubalozi wa Tanzania Harare

Waziri Dk Mwinyihaji Makame akutana na wabunge wa Afrika Mashariki

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na menyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame,alipokuwa kaizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,walipofika ofisini kwake Ikulu Mjini Zanzibar jana,Wabunge hao walisisitiza juu ya wananchi kupewa elimu ya kutosha kuhusu Jumuiya hiyo na shuhuli zake kwa wajumbe,(kutoka Kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Uhaibuni,Khamis Ali,Mbunge Dk Said Kharib Bilal na Mbunge Bi Septuu Mohamed. (02/1/2012)
(Picha na Ramadhan Othman Ikulu).

MATUMLA AMGALAGAZA CHEKA KWA POINTI

Mohamed Matumla Kushoto na Cosmas Cheka wakioneshana uwezo wa kutupa Masumbwi jana huko mkoani Morogoro
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akikingiana ngumi na Rais Wa PST Emanuel Mlundwa kabla ya kuanza kwa mpambano jana
kutoka kushoto ni Rashid Matumla,Mohamedi Matumla,Mbwana Matumla na Mkwanda Matumla (picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

FAMILIA TANO ZAWAKAMBIA MORANI, ZAOGOPA KUTEMBEZWA MITAANI UCHI

Familia tano zenye watoto zaidi ya ishirini zimelazimika kukimbia makazi yao ya kudumu kwa kipindi cha wiki tano sasa kwa kuhofia kutembezwa uchi na kupigwa na vijana wa kabila la kimasai”Morani”mara baaada ya kufanya ibada sanjari na kufanya tohara kwa njia za kisasa zaidi
Familia hizo zimelazamika kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao pamoja na maisha ya watoto wao ambapo kundi kubwa la vijana wa kimasai wanawatafuta kwa makosa ya kuharibu na kuvunja mila zao kwa njia ya Sala pamoja na Kufanya tohara Mahospitalini.
Hayo yametokea katika eneo la Oljoro Mkoani hapa ambapo kwa muda wa wiki tano familia hizo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuhofia kutembezwa mitaani Uchi, pamoja na kupigwa kipigo kikali.
Akiongea na WAANDISHI WA HABARI mmoja wa wanafamilia waliolazimika kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kutembezwa mitaani Uchi Bw Korduni Wilson, alisema kuwa Morani hao wamekuwa wakifanya vibaya sana kwa kuwa mila wanazozitaka zina madhara sana.
Bw Korduni alieleza kuwa wameamua kufikia uamuzi huo wa kukimbia nyumba zao kwa kuwa wao tayari wameshajua na kufahamu madhara ya kufanya tohara kwa njia ya kienyeji sanjari na kuabudu mila ambazo Morani hao wanazitaka.
“kati ya hizi familia tano nyinginezo hazijakimbia kwa kuwa wamefanya tohara kwa watoto wao bali Morani hao wamekuwa wakidai kuwa wanaharibiwa mambo ya Kimila hasa pale wanaposali kwa maana hiyo wanakataa hata makanisa kwa kuhofia Matambiko, na Mila”aliongeza Bw Korduni.
  
Pia aliongeza kuwa mara baada ya Morani hao kuona kuwa Kanisa linakubali na kusisitiza waumini wake kufanya Tohara kwa njia ya kisasa sanjari na kukataa Mila ambazo zina madhara kwa Mtanzania Morani hao waliktaa amri hiyo na kuvunja Kanisa la T.A.G oljoro hali ambayo ilisababisha hasara kubwa sana.
Katika hatua nyingine Msimamizi na Muangalizi wa makanisa ya T.A.G mkoani hapa Bw Simion Vomo alisema kuwa wao kama kanisa hawataweza kuwasikiliza Morani hao kwa kuwa madai yao hayana Msingi Kisheria
Aliongeza kuwa Kanisa litalazimika kuchukua hatua kali na za kisheria,kwa kuwa Morani hao wanasababisha amani ndani ya miji na Maboma ya wananchi kukosekana hali ambayo kama haitaweza kuchukuliwa tahadhari basi itazaa matatizo makubwa sana katika jamii.
Awali Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Bw. Akili Mpwapwa alisema kuwa bado polisi wanaendelea na Upelelezi,hivyo familia hizo tano ambazo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuwahofia Morani hao, wanatakiwa kutoa Taarifa ili Sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa wanachokifanya Morani hao ni Makosa.(Na:Shaaban Mpalule)

Shule ya kufundishia mpira yapata msaada wa vifaa vya michezo.

Na Gladness mushi , Arusha. SHULE ya kufundisha mpira wa miguu ijulikanayo kama Future Stars Academy iliyopo jijini hapa imenufaika na msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shs, 4.5 milion. Msaada huo umetolewa na wafadhili kutoka chama cha mpira cha vijana jimbo la Florida Marekani ikiwa ni njia mojawapo ya kuchangia swala zima la michezo kwa shule hiyo. Akizungumzia kuhusiana na shule hiyo , Mkurugenzi wake, Alfred Itaeli alisema kuwa, lengo la shule hiyo ni kufundisha michezo kwa wanafunzi waliopo mashuleni ambapo wanafunzi zaidi ya 152 kutoka shule mbali mbali za mkoa wa Arusha wanafundishwa michezo katika shule hiyo. Alisema kuwa, shule hiyo iliazishwa kwa lengo la kuinua vipaji vya michezo kwa wanafunzi ambapo hadi sasa wana jumla ya timu sita kuanzia umri wa miaka 11 hadi 17 . Itaeli alisema kuwa, shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009 likiwa na lengo la kuwaweka wanafunzi pamoja ambapo wanajifunza mpira wa miguu . Ambapo mwaka jana wanafunzi hao wamefanikiwa kushiriki mchezo wa kikombe cha ligi ya Afrika Mashariki ambapo mchezo huo ulifanyikia Nairobi na ilizishirikisha jumla ya timu 94 ambapo timu hiyo ya Future stars Academy ilifanikiwa kushinda nusu fainali ambapo lengo lao ni kuchukua kombe . ‘pamoja na kuwa sisi tunajitahidi sana kuleta maendeleo ya michezo katika jamii yetu kwa ujumla bado changamoto ni nyingi sana zinazotukabili ,hivyo tunaomba watu binafsi na mashirika wajitokeze kwa wingi kuchangia vifaa mbalimbali vya michezo kwani hivi bado havitoshelezi ikilinganishwa na kuwa uhitaji ni mkubwa sana’alisema Itaeli. Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni apmoja na ukosefu wa viwanja vya michezo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza vijana hao kwani michezo imeweza kwa kiasi kikubwa sana kuwaondoa katika changamoto mbalimbali zikiwemo za kuondokana na makundi yasiyofaa(Na :Mwandishi Wetu)

MDAU WA WWW.ELIMUBORA.COM AMALIZA KOZI YA WEB DESIGN

Evance ambae anaratibu website ya www.elimubora.com akiwa anapokea cheti baada ya kuhitimu kozi fupi nchini India. Amewataka watanzania hususan wadau wa masuala ya IT kufuatilia udhamini mbalimbali wa kozi fupi utolewao na chuo hicho kwa taarifa zaidi ingia katika libeneke lake la www.elimubora.com

RAIS JAKAYA AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAWILI NA NAIBU KATIBU MKUU MMOJA IKULU DAR LEO

Rais Jakaya Kikwete aklimwapisha Mh Eliakim C. Maswi kuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini katika hafla iliyofanyika Iukulu leo jijini Dar es salaam. (PICHA ZOTE NA IKULU) Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliackim Chacha, baada ya kuapishwa leo Ikulu Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Paul, Katibu Mkuu Ikulu, Peter Alanambula Ilomo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Chacha, kabla ya kuapishwa wakati Makamu akiingia katika Ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa makatibu hao walipokuwa wakisubiri kuapishwa rasmi kushika nafasi hizo Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa leo Januari 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo.
Rais Jakaya kikwete akimwapisha Mh Peter Ilomo kuwa Katibu Mkuu Ikulu PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi PICHA NA IKULU
Rais Dk. Jakaya Kikwete wa pili wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa rais Dk. Gharib Bilal wa pili kutoka kushoto na makatibu walioapishwa leo kutoka kulia ni Mh Peter Ilomo Katibu Mkuu Ikulu, Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi,Balozi Ombeni Sefue katibu mkuu kiongozi na mwisho kushoto ni Mh Eliakim C. Maswi Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini (Mwandishi Wetu).

UWF yatoa msada kwa familia iliothirika na mafuriko huko kigogo mji mpya

Mwenyekiti wa UWF - Unity Of Women Friends,Mwate Madinda akikabidhi kiasi cha fedha taslim kwa familia ya Mzee Shaaban Mkana,ambao walithirika na mafuriko huko Kigogo mji mpya,jijini Dar,pamoja na kukabidhi kiasi cha fedha pia UWF walitoa msaada wa vifaa, chakula na vitu mbalimbali,mwishoni mwa wiki,Kushoto kwa Mwenyekiti ni Mwenyekiti wa mradi wa SOMKI (somesha mtoto wa kike),Maryam Shamo pamoja na mwanachama wa UWF,Bi.Galina Ajmy.
UWF - Unity Of Women Friends wakijumuika na marafiki wa karibu na kukabidhi misaada ya vifaa, chakula na fedha taslim kwa familia ya mzee Shaaban Mkana ambao waliathirika na mafuriko huko Kigogo mji mpya,mwishoni mwa wiki.
Kikundi cha UWF kimejikita katika kuwakomboa watoto wa kike wasio na uwezo katika kupata elimu kupitia mradi wao wa SOMESHA MTOTO WA KIKE (SOMKI), pia wamejiwekea utamadumuni wa kutembelea vituo mbali mbali kama hospitali, vituo vya kulelea watoto n.k. kuwafariji wakati wa sikukuu mbali mbali.Ukitaka kuona kazi mbalimbali zilizowahi kufanywa na UWF,(Mwandishi Wetu)