TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 9, 2013

IBF YAAWAALIKA WAFANYABISHARA WA KITANZANIA BERLIN, UJERUMANI

 


Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati linawaalika wafanyabishara wa kitanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe Mei 21-25th, 2013.
 Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200 duniani watahudhuria.
 Hii ni fursa pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huu kutangaza biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii, TEHAMA, usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini.
 Mkutano wa mwaka wa IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta mbalimbaki za kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao mzuri wa biashara.
 Rais wa Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi anawahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hizi ili waweze kufaidika kiuchumi,
 Aidha, Ngowi anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya shughuli za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia fursa mbalimbali za biashara.
 Ngowi ataongoza ujumbe nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati wakiwamo Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.
 

DK. ABDALLAH KIGODA:MIPAKA YA NCHI LANGO LA BIDHAA FEKI




Na Gladness Mushi,Arusha.
 Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Abdallah  Kagoda amesema kuwa mipaka  ya nchi imekuwa chanzo cha uingizwaji wa bidhaa ambazo ziko chini ya viwango (feki)  hali inayochangia kuleta athari kubwa kiuchumi na afya za watu wanaotumia bidhaa hizo.
Aidha waziri huyo ameeleza kuwa uingizaji wa bidhaa bandia nchini unatokana na taasisi zinazoshughulikia masuala ya viwango vya ubora kutoimarika kiutendaji .
Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha iliyoandaliwa na shirika la dunia linalohusika na mambo ya kuandaa viwango (ISO) wakishirikiana na shirika linaloshughulikia viwango na ubora wa bidhaa nchini (TBS),warsha iliyokuwa ikijadili juu ya mfumo wa uzalishaji kuanzia malighafi,bidhaaa,mtumiaji na taka inayotokana na bidhaa hiyo ilivyo na athari katika mazingira yaani (Life Cycle).
 “Mkutano huu ni muhimu kwa nchi zinazoendelea kushiriki katika kuweka vigezo vya viwango vya ubora na kujiaandaa kuvitimiza ili kuweza kuuza bidhaa katika soko la dunia ili kuondokana na vikwazo katika uingizaji wa bidhaa zao kwenye soko hilo kutokana na bidhaa kutokizi ubora wa kimataifa na teknolojia dhaifu inayotumika  kuanzia malighafi,bidhaa hadi usafirishaji” Waziri Kagoda
 Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBS Bwana Leandri Kinabo amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kuweka mikakati ya viwango,na uzalishaji bora unaozingatia ubora ili kushiriki kikamilifu katika soko la dunia  (WTO) ukizingatia kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa soko hilo .
 Hivyo amewataka wazalishaji   kuzingatia utunzaji wa mazingira katika mfumo mzima wa uzalishaji kuanzia malighafi,bidhaa,usafirishaji na utupaji wa taka inayotokana na bidhaa hiyo (Disposal).
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo ni kutoka nchi za Afrika Mashariki,Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC)  na pia unatarajia kuhudhuriwa na nchi za Malaysia,India,China na Uingereza.