Posted: 06 Feb 2013 01:27 AM PST
Mchuuzi
wa Samaki, Bw. Aloyce Sebastian akimfunga samaki na mpira (rubber band)
ili maji yasiingie katika mapezi, kama alivyokutwa kwenye Soko la
Samaki la Kimataifa Feri, Dar es Salaam hivi karibuni. Wateja wengi
huamini samaki mwenye mapezi mekundu kuwa ni salama kwa kitoweo. (Picha
na Asia Mbwana) 
|
|
Posted: 06 Feb 2013 01:24 AM PST
Na Goodluck Hongo
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amesema chama hicho kitatumia ngumu ya umma kupeleka hoja zote za wabunge zilizokataliwa bungeni kwa wananchi. Dkt. Slaa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, hakuna mahakama nyingine za
kuwashtaki Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda na Naibu wake, Bw. Job
Ndugai. “Hakuna mahakama yoyote ya wananchi iliyowahi kushindwa,
nasi tutapeleka hoja zote zilizozimwa na bungeni na Spika Makina pamoja
na Naibu wake Ndugai kwa wananchi,” alisema Alisema chama hicho kilishatangaza mwaka huu ni wa nguvu ya umma hivyo kitendo cha Spika na Naibu wake kushindwa kuliongoza Bunge ambalo ndiyo linaisimamia Serikali kwakuzima hoja muhimu kwa masilahi ya nchi na Watanzania,wananchi watatoa hukumu kwa Serikali na CCM. “Wananchi
wanashindwa kupata haki zao mahakamani, polisi na sehemu zingine na
hivi sasa vitendo hivi vimehamia bungeni kwa kuzima haki za wananchi.“Ipo siku uvumilivu utakwisha na kujua kwa nini nchi za Rwanda na Burundi waliingia vitani...nchi hizi hazijaingia katika vurugu kwa kupenda bali kutokana na ukandamizaji kama huu,” alisema. Alisema
mwaka 2011, aliwahi kusema Tanzania haitatawalika na kuitwa mchochezi
lakini leo maamuzi ya Spika ni ya kukandamiza wananchi kwani hoja
zilizozimwa ni kwa manufaa ya Watanzania ambapo Spika na Naibu wake,
wanaongoza Bunge kwa chuki. Aliongeza kuwa, kutokana na hilo
amewaagiza wabunge wote wa CHADEMA kutokwenda kwenye Kamati ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge hadi Spika atakapoweka wazi rufaa 10
zilizokatwa na wabunge hao. Aliwataka wajumbe wote ambao
watakwenda katika mabaraza ya kutoa maoni ya Katiba Mpya, watoe mani ya
kutaka Spika na Naibu wake wasitokane na chama chochote cha siasa ili
Bunge liweze kufanya kazi kwa niaba ya wananchi si kwa matakwa ya CCM. Dkt.
Slaa alisema, hivi sasa viongozi wanaoliongoza Bunge hilo, wameshindwa
kutekeleza wajibu wao kwa kupindisha kanuni za Bunge wazi wazi na kama
zingefuatwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru
Kawambwa, angejiuzulu. “Samuel Sitta (Mbunge wa Urambo, mkoani
Tbaora na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki), aliongoza Bunge
kwa aibu pale alipotaka kupindisha sheria lakini Spika wa sasa na Naibu
wake ni balaa zaidi,” alisema Dkt. Slaa. Alisema cham hicho kinawapongeza wabunge wote wa upinzania waliosimama bungeni kupinga maamuzi ya Spika na hiyo ndio njia pekee ya kutafuta haki za Watanzania.
|
Posted: 06 Feb 2013 01:23 AM PST
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaaam, Machi 11 mwaka huu, inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa zaidi ya sh. milioni 100, inayowakabili vigogo wa Shirika la VUKA-Tanzania, linalohusika kuendesha miradi ya UKIMWI.Washtakiwa
hao ni Mwenyekiti wa shirika hilo Bw. Adolf Mrema, Mkuu wa Kitengo cha
Fedha na Utawala, Bi. Hilda Urassa pamoja na mshauri Bw. Straton Simon,
ambao wanadaiwa kutumia fedha za miradi ya UKIMWI. Jana kesi hiyo ililetwa mahakamani hapo kwa ajili ya utetezi ambapo washtakiwa hao, walijitetea mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kufunga ushahidi wao.Wakitoa utetezi wao, washtakiwa hao walikana kutumia isivyo halali fedha hizo kutoka Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na Shirika la SAT-Tanzania. Kwa
nyakati tofauti, washtakiwa hao walidai fedha hizo walizitumia kwa
ajili ya matumizi ya ofisi kama dawa kwa ajili ya waathirika wa VVU,
kuendesha semina na kulipa mishahara ya wafanyakazi wao. Hata
hivyo, washtakiwa hao hawakuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi ya
fedha hizo na kudai kuwa, nyaraka hizo zilichomwa moto na mwenye nyumba
aliyewapangisha ofisi kwa kuwa waliifunga.Walidai mwenye nyumba
baada ya kuona wamefunga osifi, aliamua kumpangisha mtu mwingine hivyo
kutoa vitu vyao na kusababisha nyaraka zao kupotea na nyingine kuchomwa
moto kama uchafu. Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 37 likiwemo la kugushi, wizi na matumizi mabaya ya fedha.Inadaiwa kuwa, washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Juni11,2006 hadi Desemba 2007, Temeke, Dar es Salaam.
NYANYA
|
Posted: 06 Feb 2013 01:20 AM PST
Dalali
wa nyanya katika Soko la Ilala, Kaniki Ramadhani akiwa ameshikilia
'kitita' cha fedha wakati kifanya hesabu za biashara hiyo, kama
alivyokutwa Dar es Salaam jana. Sanduku moja la nyanya lilikuwa likiuzwa
kwa sh. 18,000. (Picha na Charles Lucas)
|
|
Posted: 06 Feb 2013 01:14 AM PST
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MWENYEKITI
wa Kanisa la Moravian nchini, Jimbo la Kusini, Mchungaji Clement
Mwaitebele, mewataka wachungaji 14 ambao alitangaza kuwafukuza baada ya
kukiuka kiapo chao cha utumishi Misheni ya Dar es salaam, kuondoka
katika nyumba za kanisa.Akizungumza na Majira jana, Mchungaji Mwaitebele ambaye alionesha kukerwa na wachungaji hao kuvuruga amani ndani ya kanisa
hilo kwa kujitangazia Halmashauri Kuu yao kinyume na Katiba, alisema
uongozi wa kanisa umechukua hatua stahiki kwa watumishi hao kwa kuwa
wasaliti katika jimbo mama. Alisema inashangaza wachungaji hao
kudai hawaitambui mamlaka iliyowafukuza badara yake wanasubiri maelekezo
ya uongozi wa Bodi ya Dunia (Unity Bord) ulio na Makao Makuu nchini Ujerumani hali inayoonesha kuwa, pamoja na usomi wao bado wameshindwa kutambua taratibu.“Kwa kuwa wameonesha kiburi cha kutoitambua mamlaka yangu kikatiba, natangaza rasmi kuwa kuanzia leo (jana), nimefuta ujio wa Bodi ya Dunia kuja nchini kuzungumzia tatizo hili kwa sababu tayari limekwisha hawana umuhimu wa kuja,” alisema. Mchungaji Mwaitebele alisema Ofisi la Dunia ni Makao Makuu ya Jumuia ya kanisa hilo kama ilivyo Umoja wa Mataifa ambao hauwezi kuingilia mambo ya ndani nchini Tanzania hadi unapopewa taarifa na uongozi wa nchi. “Sisi
kama viongozi wa jimbo mama, hatuoni umuhimu wa hawa viongozi Bodi ya
Dunia kuja kusikiliza mazungumzo kwa sababu tayari tumemaliza mgogoro
uliokuwepo na taratibu za kisheria zinachukuliwa,” alisema. Aliwataka
wachungaji hao kuhama mara moja katika nyumba za kanisa kwani hivi sasa
si watumishi tena wa kanisa hilo kwa mujibu wa katiba baada ya
kushindwa kulinda kiapo chao kilichowataka kuwa watii uongozi badala
yake wanatumika kuleta mipasuko.Aliongeza kuwa, wao walifuata utaratibu wa kanisa wa kukaa mezani ili kusikiliza matatizo ya Misheni hiyo baada ya Sinodi ya eneo hilo kumuondoa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wao. “Wakati
mazungumzo yakiendelea, Mwenyekiti huyo alitangza Halmashauri Kuu yake
jambo lililoonesha wazi usaliti mkubwa katika kanisa,” alisema Mchungaji
Mwaitebele.Aliwaonya Watunza Hazina wa kanisa hilo kuepuka kushirikiana na wachungaji hao kwa kuchukua fedha za matumizi yao binafsi kwani uongozi wake utawaburuta mahakamani kwa kosa la wizi wa fedha za umma jambo ambalo asingependa litokee. Alisema
Mamlaka iliyowafukuza wachungaji hao ni halali ambayo ilichaguliwa na
Mkutano Mkuu wa Kanisa na hivyo madai kuwa walipaswa kufukuzwa kwa
pendekezo la Askofu ni upotoshaji wawanaoufanya ili kuliyumbisha
kanisa.

|
|
Posted: 06 Feb 2013 01:13 AM PST
Na John Gagarini, Pwani
MABAHARIA sita wanahofiwa kufa maji baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kwenye Habari ya Hindi kuzama.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, alisema mabaharia hao walipanda jahazi la mizigo na walikuwa saba lakini mmoja ameokolewa. Alisema
jahazi hilo linalofahamika kwa jina la Soweto, lilizama katika Visiwa
vya Koma, eneo la Mwamba wa Chokaa, wilayani Mkuranga. “Usajiri wa jahazi hili bado haujafahmika na lilikuwa na shehena ya mbao na mirunda likitokea Kyasi kwenda Zanzibar,” alisema.Aliwataja
baadhi ya mabaharia wanaohofiwa kufa maji kuwa ni Ally Hasan, Hassan
Mamba, Nasoro Isa, Abdala Said na Husein Huku wakati Hasan Rajab,
aliokolewa na wanaendelea kutafutwa.Aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kawa wataziona maiti zinazoelea majini.

|
|
Posted: 06 Feb 2013 12:57 AM PST
Na Godfrey Ismaely, Manyara
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuona matukio ya ujangili nchini yanaongezeka siku hadi siku, muda wowote ataagiza majeshi yote kushirikiana ili kudhibiti matukio hayo.Hatua hiyo inatokana na Serikali ya Tanzania kusaidi dikezo maalumu na Serikali ya Marekani ambalo kushirikiana katika kudhibiti matukio ya ujangili nchini.Balozi Kagasheki aliyasema hayo jana mkoani Manyara katika hafla
maalumu ya uzinduzi wa Kituo cha Mapokezi kwa watalii ambacho kipo
chini ya Jumuiya ya Usimamizi wa Hifadhi ya Wanyapori Burunge (WMA),
Wilaya ya Babati, mkaoni Manyara, kilichojengwa na Marekani kupitia
Shirika lake la USAID. Jana (juzi) mimi na Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani wa Marekani Bw. David Hayes, tulisaini dokezo hili kwa lengo
la kukomesha matukio ya ujangili nchini,” alisema na kuongeza kuwa,
matukio ya ujangili yanaichafua nchi pia ni mateso kwa wanyama.Alisema
mapambano dhidi ya majangili yanawezekana ambapo Serikali imeanza
kujipanga ambapo Rais Kikwete, wakati wowote atatoa uamuzi kamka Amiri
Jeshi Mkuu wa nini kifanyike kudhibiti hali hiyo nchini. Alisema
suala la kucheleweshwa fedha zinazotokana na makusanyo ya WMA ambayo ni
asilimia 50 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi,
litafanyiwa kazi na wakati wowote mambo yatakuwa mazuri.Kwa upande wake, Bw. Hayes ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema lengo la nchi yake kutoa ufadhiri kwa jumuiya za WMA nchini, mbali ya kulenga kukomesha ujangili pia jamii zitanufaika kupitia mapato mbalimbali. “Kufanikiwa
kwa WMA ni fursa moja wapo ya kukomesha kabisa matukio ya ujangili
yanayotokea Tanzania, vitendo hivi vinachangia kuhatarisha usalama wa
binadamu, wanyamapori na hata kutatiza shughuli za utalii,” alisema Bw.
Hayes.Balozi wa Marekani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt's, alisema utaratibu wa wanajamii kuanzisha WMA nchini umeweza kuwa na mafanikio makubwa, kuboresha miradi ya shule, zahanati na kusomesha watoto kutokana na mapato yanayopatikana kutoka kwa wawekezaji walioingia nao mikataba. “Tangu
mwaka 2006, WMA tisa zimeweza kuingia mikataba na wawekezaji binafsi
katika sekta ya utalii ambapo zimefanikiwa kupokea zaidi ya dola za
Marekani milioni tano kutokana na shughuli za uwindaji na upigaji picha. “Hatua
hii imewezesha zaidi ya wanajamii 400,000 kunufaika kwa namna moja ama
nyingine pamoja na kupata ajira hivyo Marekani itaendelea kuzijengea
uwezo jumuiya hizi mara kwa mara ziweze kufikia malengo ya uhifadhi na
maendeleo kwa wananchi,” alisema.
MADAFU
|
Posted: 06 Feb 2013 12:52 AM PST
Wasamaria
wakisaidia kuidhibiti baiskeli baada ya kuangukia gari namba T 309 AWU.
Kushoto ni dereva wa gari hilo akiangalia sehemu iliyoharibika katika
gari hilo, kama walivyokutwa katika Barabara ya Sokoine Posta, Dar es
Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi) 
|
|
Posted: 06 Feb 2013 12:48 AM PST
Na Masau Bwire, Bunda
OFISA
Mtendaji wa Kata ya Iramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Bw. Simon
Katikizu, amenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kumshambulia
kwa mawe wakimtuhumu kuiba mahindi ya msaada. Tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Kijiji cha Isanju ambacho ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi ya msaada.Wakati
kazi ya kugawa mahindi hayo ikiendelea, wananchi hao walibaini upotevu
wa magunia zaidi ya 40 na baada ya kufanya uchunguzi, wakagundua wizi
huo ulifanywa na Bw. Katikizu hivyo walianza kumshambulia kwa mawe na marungu. “Tumemkamata
na mahindi ya msaada akiwa ameyaficha nyumbani kwake, katika Ofisi ya
Elimu, kilimo na mengine aliyaweka katika nyumba za rafiki zake, wakati
akijaribu kukimbia lilipigwa yowe,” alisema Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi CCM, katika kata hiyo, Bw. Mohamed Gamba.Alisema Serikali ilipeleka msaada wa magunia 318 ya mahindi kwa ajili ya vijiji vitano vya kata hiyo ambapo kila kijiji kilipaswa kupata magunia 63 kutokana na njaa inayowakabili wananchi. Vijiji
vilivyokumbwa na tatizo la njaa ni Isanju, Mugara, Sikiro, Nyarugoma na
Mwiruruma, lakini Bw. Katikizu aliiba kiasi kikubwa cha mahindi ambapo
kijiji cha Nyarugoma, kiliambulia magunia 26 ndipo wananchi walipokuja
juu na kugundua wizi huo. Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Joshua
Mirumbe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa, tayari
amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri amsimamishe kazi Bw. Katikizu kwa
kosa hilo. “Huyo Ofisa Mtendaji habari zake ninazo, aliwahi kuiba na kuuza mitumbwi 20 iliyokamatwa katika uvuvi haramu hivyo kutokana na tukio hili, nimeagiza Mkurugenzi amsimamishe kazi kuanzia leo (jana) na ashitakiwe kwa wizi,” alisema Bw. Mirumbe.Alisema
viongozi wa namna hiyo hawafahi kuendelea kuongoza na wanaitia doa
Serikali hivyo hawana budi kuondoka wabaki viongozi waaminifu na
waadilifu watakaowaletea wananchi maendeleo.
“Siko tayari kuona
viongozi wezi, wabadhilifu na wababaishaji wakiendelea kuwanyonya
wananchi kwa kuwaibia, kama wapo wajiondoe kabla sijawafikia, nitaanza
na huyo Ofisa Mtendaji ili iwe mfano kwa wengine,” alisema.Majira
lilipomtafuta Bw. Katikuzu na kumuuliza juu ya tuhuma hizo alidai madai
hayo ni uzushi uzushi na hakuna wizi wowote aliofanya bali yeye ni
miongoni mwa Watendaji waadilifu wilayani humo wanaoaminiwa kiutendaji
na Bw. Mirumbe.

|
|
Posted: 06 Feb 2013 12:41 AM PST
Na Miriam Sarakikya
BAADHI
ya wananchi wanaoishi mabondeni eneo la Tegeta kwa Ndevu, Wilaya ya
Kinondoni, Dar es Salaam, wameiomba Serikali iwasaidia kuwapa viwanja
ili waweze kuondoka katika maeneo hatarishi kutokana na kero wanayopata
kipindi cha mvua.Wakizungumza
na Majira kwa nyakati tofauti Dar es Salaam juzi, wananchi hao walidai
wanashindwa kuondoka maeneo hayo kutokana na ukata wa fedha za kununulia
viwanja. “Baadhi yetu wamejenga nyumba zao katika maeneo haya na wengine wamepanga, tunaiomba Serikali isikilize kilio chetu ili tuweze kuhamia maeneo salama tofauti na sasa kwani tunaishi kwa wasiwasi mkubwa,” alisema mkazi wa eneo hilo Bw. Edgar Msanganzila.Mkazi
mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema hivi
sasa eneo lao linafurika maji kutokana na mto uliopo jinani na makazi
yao hivyo kuhatarisha maisha yao na familia zao. Hivi karibuni wananchi hao waliitisha mkutano wa hadhara na kukubaliana kuupanua mto huo maarufu 'Mto Tegeta', ili kupata njia ya kupitisha maji kirahisi pindi mvua zinaponyesha lakini hadi sasa mpango huo haujafanikiwa.
Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000
|
Posted: 06 Feb 2013 12:40 AM PST
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, juzi ilimuhumuku mkazi wa
Dodoma Mjini, Yohana Chipini (23), kifungo cha miaka miwili jela baada
ya kupatikana na hatia ya kumuua Alord Ndeshio, bila kukusudia wakati
akidai sh. 4,000. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Shangali baada ya mshtakiwa kukiri kosa na kumtia hatiani. Jaji
Shangali alidai kuwa, amezingatia maelezo yaliyotolewa na upande wa
mashtaka pamoja na utetezi kuhusu chanzo cha mauaji hayo ambacho ni
ugomvi uliotokea kati yao wakati mshtakiwa alipokwenda kumdai marehemu
fedha zake.Aliongeza kuwa, baada ya ugomvi huo mshtakiwa
aliokota kipande cha ubao au kitu kinachoaminika kuwa kipande cha chuma
na kumpiga nacho marehemu kichwani. “Adhabu ya kuua bila
kukusudia ni kifungo cha maisha lakini kutokana na mazingira
yalivyoonyesha na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imempunguzia adhabu na
hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani,” alisema. Kabla
ya hukumu hiyo, wakili wa mshtakiwa, Steven Kuwayawaya, aliiomba
mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa akidai kosa hilo ni la kwanza na
amekiri kosa. Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuw,
mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2012 katika barabara ya Bahi,
Manispaa ya Dodoma.

|
|
Posted: 06 Feb 2013 12:38 AM PST
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Tarakea, mkoani Arusha, Bw. Martin Kija
(kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaki Okada wakitia saini
makubalino, Dar es Salaam jana, ambapo Serikali ya Japan itajenga
mabweni ya wasichana ya shule hiyo. Ujenzi wa mabweni hayo utawaondolea
tatizo la kutembea umbali mrefu kutoka maeneo wanayoishi. (Picha na Asia
Mbwana)
|
|
Posted: 05 Feb 2013 10:33 PM PST
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, juzi ilimuhumuku mkazi wa
Dodoma Mjini, Yohana Chipini (23), kifungo cha miaka miwili jela baada
ya kupatikana na hatia ya kumuua Alord Ndeshio, bila kukusudia wakati
akidai sh. 4,000. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Shangali baada ya mshtakiwa kukiri kosa na kumtia hatiani. Jaji
Shangali alidai kuwa, amezingatia maelezo yaliyotolewa na upande wa
mashtaka pamoja na utetezi kuhusu chanzo cha mauaji hayo ambacho ni
ugomvi uliotokea kati yao wakati mshtakiwa alipokwenda kumdai marehemu
fedha zake. Aliongeza kuwa, baada ya ugomvi huo mshtakiwa
aliokota kipande cha ubao au kitu kinachoaminika kuwa kipande cha chuma
na kumpiga nacho marehemu kichwani.“Adhabu ya kuua bila
kukusudia ni kifungo cha maisha lakini kutokana na mazingira
yalivyoonyesha na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imempunguzia adhabu na
hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani,” alisema.
Kabla
ya hukumu hiyo, wakili wa mshtakiwa, Steven Kuwayawaya, aliiomba
mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa akidai kosa hilo ni la kwanza na
amekiri kosa.Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuw,
mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2012 katika barabara ya Bahi,
Manispaa ya Dodoma.

|
|
Posted: 05 Feb 2013 10:30 PM PST
Na Mariam Mziwanda
MAOFISA Kilimo zaidi ya 20 kutoka Wilaya tano nchini, wapo kwenye mafunzo ya mradi shirikishi wa kupunguza wimbi la viwavi jeshi ambavyo ni kero sugu kwa wakulima na kusababisha njaa katika baadhi ya maeneo nchini.Akizungumza
katika mafunzo hayo Dar es Salaam juzi, mwezeshaji wa mafunzo hayo
ambaye pia ni Ofisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,
Kanda ya Kaskazini, Bw. Didas Moshi alisema mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuwatambua na kuwaangamiza kabla ya kukua. “Tumeanza
mafunzo haya na Wilaya tano ambazo ni Kisarawe, Nachingwea, Masasi,
Lindi Vijijini na Kilwa, mafunzo haya yanaendeshwa kwa msaada wa watu wa
Marekani ambao wameona viwavi jeshi ni kero kwa wakulima,” alisema.Akifungua
mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea kutoka katika Wizara
hiyo, Cornelius Mkondo, alisema mazao mengi ya wakulima nchini yamekuwa
yakiathiriwa na milipuko ya wadudu sugu wanaoshambulia mazao kwa haraka.Alisema viwavi jeshi wamekuwa wakipoteza nguvu kazi za wakulima hivyo imeamua kutafuta mbinu za kuwatokomeza. Aliongeza
kuwa, maofisa hao watafundishwa mambo mengi hususan jinsi ya kufahamu
mlipuko unavyotokea na kuimarisha mawasiliano kati ya vijiji, kata,
Wilaya hadi Taifa.“Lengo ni kujilinda na viwavi, katika
kuhakikisha operesheni hii inakuwa endelevu, tutashirikiana na kampuni
za simu ili wakulima waweze kufahamu utabiri wa hawa wadudu waharibifu,”
alisema na kuongeza kuwa, mradi huo mbali ya Tanzania pia unaendeshwa katika nchi za Kenya na Ethiopia.

|
|
Posted: 05 Feb 2013 10:29 PM PST
Na Rose Itono
WIZARA
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekabidhiwa majukumu ya kuweka viwango
vya ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za elimu
kuanzia awali mpaka sekondari.Sambamba
na hilo wizara pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa elimu ya
awali,msingi,sekondari na ile ya watu wazima inatolewa kwa kuzingatia
viwango vinavyokubalika. Wizara pia ina jukumu la kusimamia
utekelezaji wa utoaji wa elimu kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini
pamoja na kufanya mapitio,kuandaa na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya
Sera, Mipango, Sheria na kanuni za elimu zilizopo,kulingana na
mabadiliko ya dhima na dira ya Serikali huku ikiandaa mikakati ya
utekelezaji wake. Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya taaluma katika ngazi zote za elimu na mafunzo.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatekeleza mipango mbalimbali ili kuinua ubora wa elimu Ili
yote hayo yaweze kufanikiwa juhudi za wazazi na walezi kwa kushirikiana
na wanafunzi zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika kuleta matokeo
mazuri.Nimeongea hivyo kwa makusudi kwani kumekuwa na baadhi ya
wazazi,walezi ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi hasa wa kike
kwa kutaka kuwaoza kwa nguvu kwa nia ya kujipatia fedha ama mali.
Nionavyo hii ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kumyima haki yake ya msingi ya kupata elimu mtoto wa kile na kumjengea .Kutokana
na hali hiyo ipo haja ya serikali kuianzia ngazi zake za mtaa
kuielimisha jamii matatizo na madhara ya watoto wa kike kuolewa kabla ya
umri wao na umuhimu wa watoto kusoma. Nionavyo kwa kufanya hivyo
kutalipunguza tatizo la wazazi ambao wana tamaa za kujipatia pesa kwa
mahari kupitia watoto wao bila kuangalia madhara na vitu vya msingi
ambavyo mtoto wa kike atavikosa kutokana na kuolewa bila kuwa na elimu. Hivi
karibuni tumeshuhudia mtoto wa kike ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha
pili katika shule ya sekondari Tongani kata ya Mkaramo wilayani Pangani
akitoroka kwao na kukimbilia kujificha porini akikwepa kuachishwa shule.Nionavyo
hali hii ni hatari kiusalama kwa mtoto huyo ambaye angeweza kupata
madhara ya kukutana na wanyama wakali na hata kupoteza maisha.Hali
ya mtoto huyo kuamua kulala porini ilimuwezesha kufika kwa Mkuu wa
Wilaya ya handeni kuomba msaada ambao utamuwezesha kuweza kuendelea na
masomo. Nionavyo kulingana na hali hiyo ni wanafunzi wangapi
wenye ujasiri kama aliouonyesha msichana huyo ambaye aliamua kujitoa
muhanga na kuamua kulala porini ili kukimbia kuolewa.Kwa maelezo
ya mtoto huyo anasema aliamua kukimbilia kwa Mkuu wa Wilaya baada ya
kusikia kuwa kuna mradi wa 'Niache Nisome' ambao umeanzishwa kwa ajili
ya kumkomboa mtoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utotoni. Nionavyo
kwa mfano wa mradi huu ni wazi serikali ikaona umuhimu wa mradi huo
kusambaa nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kike kujikomboa na ndoa na
mimba za utotoni.
|