TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 11, 2013

JK ampa rungu Magufuli-Bwanga – Biharamulo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyeshika mkasi) akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John P. Magufuli na kulia kwa Rais ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Eng. Mussa Iyombe. Wengine katika picha ni baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa Mikoa ya Geita na Kagera walioshiriki katika sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimwagilia mti alioupanda katika eneo la Buziku mkoani Geita wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Lori aina ya Scania la Kampuni ya MAP CO Ltd. likiwa na usajili namba T 895 AFH/T 226 AGB kama  lilivyokutwa eneo la Manyoni mkoani Singida likiwa limekatika katikati kutokana na kuelemewa na uzito wa mzigo lililoubeba
Umati wa wananchi waliojitokeza kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili eneo la Buziku mkoani Geita tayari kwa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo. (Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia  Tanzania)

 
========================================================================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtaka Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kuhakikisha kuwa Sheria ya Usalama Barabarani inasimamiwa vizuri ili kuhakikisha kuwa barabara zinazojengwa nchini zinadumu kwa muda uliokusudiwa.

Akizungumza katika eneo la Buziku mkoani Geita wakati akizindua ujenzi wa barabara ya Bwanga hadi Biharamulo yenye urefu wa kilometa 67, Rais Kikwete alisema kuwa wizara ya Ujenzi ni lazima ihakikishe inasimamia sheria zilizopo na hasa hii ya kutoruhusu magari yenye uzito uliozidi viwango vilivyoainishwa katika Sheria Namba 30 ya Mwaka 1973.

Akisistiza umuhimu wa kutunza barabara Rais Kikwete alibainisha kuwa “adui wakuu watatu wanao sababisha barabara kuharibika mapema ni; magari yanayobeba mizigo zaidi ya uzito uliowekwa kisheria, ujenzi duni usiozingatia viwango na kuachwa kwa maji kuzagaa barabarani”.

Wakati huo huo Rais Kikwete alielezea kufurahishwa kwa kuanza ujenzi wa mradi huo kwani wapo baadhi ya watu waliokuwa waliokuwa wakieneza taarifa kuwa sehemu hiyo ya barabara haiwezi kujengwa lakini sasa wameumbuka.

Awali akitoa maelezo ya mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Injinia Patrick Mfugale alielezea kuwa mradi mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umegharimu Shilingi bilioni 55 fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania. “Mradi huu utajengwa kwa muda wa miezi 27 na hivyo kukamilika mwezi Februari mwaka 2015” alisema Injinia Mfugale.

Naye Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Magufuli alimhakikishia Rais Kikwete kuwa wizara yake itahakikisha kuwa inamsimamia mjenzi wa mradi huo ambaye ni Kampuni ya Sinohydro Ltd. ya kutoka Jamhuri ya Watu wa China ili aukamilishe kwa muda na viwango vilivyokusudiwa na bila ya visingizio vya nyongeza ya gharama.

Akimpongeza Rais kwa kutekeleza ahadi yake, Waziri Magufuli alibainisha kuwa wananchi wa mikoa  ya Geita na Kagera wamefurahishwa sana kuona kuwa hatimaye barabara hiyo muhimu inajengwa kwani hiyo ndiyo sehemu pekee iliyokuwa imebaki ikiwa haina lami kwa barabara inayounganisha mikoa hiyo ya ziwa.

Wednesday, November 6, 2013

A Presidential Surprise


Today, President Obama and First Lady Michelle Obama kicked off the resumption of East Wing and Executive Residence tours by surprising White House tour guests in the Blue Room.
President Barack Obama and First Lady Michelle Obama greet visitors in the Blue Room during a White House tour, Nov. 5, 2015. (Official White House Photo by Pete Souza)
President Barack Obama and First Lady Michelle Obama greet visitors in the Blue Room during a White House tour, Nov. 5, 2015. (Official White House Photo by Pete Souza)

 

  Top Stories
Yesterday in the East Room, President Obama welcomed the Stanley Cup Champion Chicago Blackhawks to the White House --  the second time he's honored the team for their Stanley Cup win.
Yesterday, Katherine Archuleta was sworn-in as the 10th Director of the Office of Personnel Management (OPM) and will serve as the Federal government’s personnel chief. She will be the first Latina to hold this position.
READ MORE
We recently asked folks to share their experiences getting covered since the Health Insurance Marketplace opened for business on October 1st. Here are some of the stories we heard.

DACICO WANAFUNZI WAENDELEA NA MITIHANI KATIKA CUMPUS YA DAR, MBEYA NA SUMBAWANGA.

Baadhi ya Wanafunzi wa DACICO, Wakiwa katika Vyumba vya Mitihani Leo tarehe 6/11/2013, Cumpus ya Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wa DACICO, Cumpus ya Dar es Salaam, Muda mfupi kabla ya kuanza mitihani, wakisimama kwa ajili ya kupata Maombi.(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Monday, November 4, 2013

President Obama Speaks Out in Support of ENDA

President Barack Obama delivers remarks at the LGBT Pride Month Reception in the East Room of the White House, June 15, 2012. (Official White House Photo by Chuck Kennedy)
================================================================
This week, the Senate is expected to take up a critically important piece of legislation: the Employment Non-Discrimination Act, or ENDA. This bill would make it explicitly illegal under federal law to fire someone because of their sexual orientation or gender identity -- and it’s long overdue.
In an op-ed published in The Huffington Post, the President speaks directly to the American people to ensure everyone understands what’s at stake and why it’s so important that Congress move forward on this legislation:
"It's offensive. It's wrong. And it needs to stop, because in the United States of America, who you are and who you love should never be a fireable offense."

MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI WA MASUALA YA UJENZI WA RWANDA

  • Mh.Dr.John Joseph Pombe Magufuli akisalimiana na mkurugenzi wa maswala ya ujenzi wa Rwanda. Hapo ni Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania(Picha na Abdul Mabe).

Thursday, September 26, 2013

WANAFUNZI WA DACICO WAPATA KATIBA YAO.

Rais wa Chuo Cha DACICO kISIZA AKIKABIDHI KATIKA KWA MKURUGENZI WA CHUO, Idrisa Mziray.
 Mmoja wa Waasisi wa chuo cha DACICO , Mr. Six akito neno kwa wanafunzi kabla ya Uzinduzi.
Wanafunzi wa Chuo Cha DACICO TANZANIA- Wakiwa katika Picha ya Pamoja muda mfupi baada ya kufanya Uzinduzi wa KATIBA yao waliyoipendekeza na kushiriki kwa asilimia 100 katika kuirekebesha na kuipigania kila kukisha kwa walimu wao, aidha katika Hafla hiyo ya Uzinduzi huo, wanafunzi wa masomo na fani zote walishiriki kufanya Uzinduz.(Picha kwa hissani ya Miiss Demokrasia Tanzania 2013/2015).

MAOMBOLEZO


  • RAIS KENYATTA ATANGAZA SIKU TATU ZA KUOMBOLEZA
  •  JESHI LA KENYA LAHITIMISHA KIBARUA KIGUMU
  •  AL SHABAAB WADAI MATEKA 137 WAMEUAWA,WAONYA

  •  Waandishi  Wetu  n a Mashirika ya Kimataifa


  
K
enya imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa waathirika wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi na kusababisha mapigano yaliyodumu kwa siku nne 
. Rais Uhuru Kenyatta amesema bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia jana kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo. Katika hotuba yake kwa taifa juzi usiku, Rais Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na kuwa Kenya imejeruhiwa vibaya, lakini alielezea matumaini kwa kuwa shambulizi limeisha na kusema kwamba waliohusika watakiona cha mtemakuni. 
Juzi Rais Kenyatta ametangaza kuwa operesheni za kijeshi dhidi ya magaidi zimemalizika katika maduka ya kifahari ya Westgate.Alisema Kenya imewaaibisha washambuliaji hao, kwa kuua magaidi watano na kuwakamata wengine 11 ambao wamezuiliwa. Katika tukio hilo Watu 62 wameuawa ikiwemo wanajeshi watatu na wengine 8 wamejeruhiwa. Habari kutoka Kenya zinaeleza kuwa kuna hofu kuwa idadi ya watakaofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na wale wa Kenya kujaribu kuondoa miili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana.Nia ni kujaribu pia kutambua uraia wa washambuliaji hao. Baraza la usalama wa kitaifa lilitarajiwa kukutana jana kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kukabiliana na magaidi.

Magaidi watatu wa kundi la Al Shabaab lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo,waliuawa katika shambulizi hilo lililodumu kwa siku nne na kuwa washukiwa we n g i n e 11 wa l i k ama twa wakijaribu kuondoka nchini.Wakati huo huo, ofisa mmoja mkuu wa serikali ya Somalia, amesema kuwa hakuna suluhu la kijeshi kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini humo. Wanamgambo hao wamekiri kuhusika na mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.

  Akizungumza na mjumbe wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Yusuf Mohamed Ismail Bari Bari, alisema kuwa serikali yake na jamii ya kimataifa inapaswa, kuangazia zaidi mizizi ya tatizo la magaidi hao, upatikanaji wa rasilimali pamoja na uwakilishi wa kisiasa.Wakati huo huo, Wataalamu wa uchunguzi wa Kisayansi kutoka nchini Ufaransa na Israel wamewasili nchini Kenya kushirikiana na wazawa ili kujua silaha zilizotumika wakati wa shambulizi hilo la kigaidi.

  Wataalam hao wanalenga kubaini ni aina gani ya milipuko ilitumika kulipulia jengo hilo.Pia maofisa wa Serikali bado wapo eneo la tukio ili kuhakikisha usalama unakuwepo. Televisheni ya nchi hiyo ya Q TV imesema kuwa kazi ambayo ilikuwa nimeanza ni ya kuondoa vifusi ili kuweza kuondoa maiti zilizofukiwa baada ya sehemu ya jengo hilo kuanguka.
   Kwa mujibu wa matangazo hayo maiti hizo zitatambuliwa kwa kutumia kipimo cha DNA. Matangazo ya televisheni hiyo yalieleza kuwa ndani ya jengo hilo la kibiashara moshi mkubwa ulikuwa ukizidi kufuka lakini hakukuwa na taarifa zozote kwa waandishi wa habari kuhusu ni nini kilichokuwa kikiendelea.

   Katika hatua nyingine, Serikali ya Kenya imetangaza donge nono la dola milioni 25 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa magaidi sugu ulimwenguni. Tayari FBI imetoa orodha ya magaidi 23 wanaotafutwa.
   Wakati huo huo, wanamgambo wa Al-Shabaab kutoka Somalia jana walidai mateka 137 waliokuwa wakiwashakilia waliuawa katika jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi.Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa, AFP, idadi kamili ya waliokufa imekuwa ngumu kujulikana na inaweza ikawa ni kubwa zaidi kuliko idadi ya walioorodheshwa kukosekana.

   Wapiganaji hao wenye uhusiano na al-Qaeda, katika ujumbe waliouweka kwenye mtandao wa Twitter, walisema "mateka 137 waliokuwa wakishikiliwa na mujahedeen" wamekufa."Wanamgambo hao pia waliwatuhumu wanajeshi wa Kenya kwa kupiga makombora yenye sumu kuhitimisha mapambano ya kuwasaka.


Matukio ya ubabe wa Al-Shabaab


   Haya ni miongoni mwa mashambulizi makubwa ya kigaidi ambayo yamewahi kutekelezwa katika Kanda ya Afrika Mashariki.


Taarifa zinazohusiana na Kenya

  Septemba 21, 2013: Magaidi walitumia guruneti na bunduki kushambulia jengo la kifahari la Westgate mjini Nairobi, Kenya lenye maduka na mikahawa 80 na kuwaua watu 62 huku zaidi ya 175 wakijeruhiwa.Kundi la kigaidi la Al-Shabaab lilikiri kufanya shambulio hilo.
    Oktoba 2011-Machi 2013: Al Shabaab na wapiganaji wake walifanya mashambulizi kadhaa nchini Kenya na kuwaua zaidi ya watu sitini wakilipiza kisasi kile walichosema ni hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini huo kupigana dhidi yao.Serikali ya Kenya ilituma vikosi vyake nchini Somalia baada ya al-Shabaab kufanya mashambulizi kadhaa katika maeneo ya mipakani pamoja na kuwateka nyara watalii wa kigeni.

    Julai 11 , mwaka 2010 : Wanamgambo wa Al Shabaab walilipua mabomu katika mji mkuu wa Uganda Kampala, katika mkahawa ambako mashabiki wa soka walikuwa wanatazama fainali ya michuano ya Kombe la Dunia, kwenye televisheni kubwa.
    Takriban watu 76 waliuawa. Kundi la Al-Shabaab lilisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Uganda kujihusisha na vita dhidi ya kundi hilo Somalia.Novemba 28, mwaka 2002: Kundi hilo la kigaidi lilishambulia hoteli ya kifahari iliyokuwa inamilikiwa na Waisraeli, katika eneo la Kikambala karibu na mji wa Mombasa na kuwaua watu 13.

   Dakika chache kabla ya shambulizi hilo, magaidi hao waliifyatulia makombora ndege ya Israel iliyokuwa inaruka katika Uwanja wa Kimataifa wa Mombasa, lakini waliikosa.Agosti 7, mwaka 1998: Kundi lingine la kigaidi la al-Qaeda lilishambulia balozi za Marekani mjini Nairobi na Dar es Salaam. Mashambulizi hayo yaliwaua watu 224 , wengi wakiwa Wakenya . Raia 123 wa Marekani pia waliuawa.

MWANAMKE AWATOKEA ‘PUANI’ WATU WATATU

  • MAHAKAMA KUU YAWAHUKUMU KUNYONGWA HADI KUFA


Na Moses Mabula, Nzega


Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imewahukumu watu watatu kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi mkazi wa Kijiji cha Mbagwa wilayani Nzega mkoani Tabora,Mganga Mgisha, ili mmoja wa wauaji hao apate fursa ya kuoa mke wa marehemu huyo.Katika kesi hiyo, mmoja wa wauaji hao, Kulwa Makomelo alikuwa na njama za kutaka kumuoa mke wa marehemu huyo,Catherine John, ambapo ilidaiwa alimlipa kiasi cha sh. 20,000 muuaji mwenzake, Kisena Lutonja, ili amsaidie kufanikisha mauaji hayo.


Mke wa marehemu huyo ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu hiyo.Akitoa hukumu hiyo iliyochukua muda wa saa tatu, Jaji Amiri Mluma, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa kuwa washtakiwa hao walipanga mauaji hayo.  Alisema washtakiwa wamepatikana na shtaka hilo la kupanga kuua na kufanya mauaji."Walipanga makusudi kumuua Mugisa, hivyo mahakama inawahukumu kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine.


   Jaji huyu aliiambia mahakama hiyo kwamba; "Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya watu kushambuliana kwa mapanga bila sababu na kujichukulia sheria mkononi natoa adhabu hii ili iwe fundisho kwa watu wa aina hiyo."
  Awali, mwanasheria wa Serikali, Iddforce Makandara, aliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao wote kwa pamoja walimuua, Mugisa kwa kumpiga kitu kizito kichwani na kisha kumshambulia kwa mapanga hadi kufa.Aliiambia mahakama hiyo kuwa mwaka 2005 watuhumiwa hao walikula njama za kumuua Mugisa ambaye ni mume wake na Catherine John.
  Alidai kuwa walifanya hivyo ili mjane wa marehemu aolewe na Makomelo, huku Lutonja akilipwa sh. 20,000 ili amsaidie kufanikisha mauaji hayo.Makandara aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wanaojichukulia sheria mkononi


Katika kesi hiyo, mmoja wa wauaji hao, Kulwa Makomelo alikuwa na njama za kutaka kumuoa mke wa marehemu huyo,Catherine John, ambapo ilidaiwa alimlipa kiasi cha sh. 20,000 muuaji mwenzake, Kisena Lutonja, ili amsaidie kufanikisha mauaji hayo.Mke wa marehemu huyo ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu hiyo. Akitoa hukumu hiyo iliyochukua muda wa saa tatu, Jaji Amiri Mluma, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa kuwa washtakiwa hao walipanga mauaji hayo.  Alisema washtakiwa wamepatikana na shtaka hilo la kupanga kuua na kufanya mauaji."Walipanga makusudi kumuua Mugisa, hivyo mahakama inawahukumu kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine.



   Jaji huyu aliiambia mahakama hiyo kwamba; "Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya watu kushambuliana kwa mapanga bila sababu na kujichukulia sheria mkononi natoa adhabu hii ili iwe fundisho kwa watu wa aina hiyo."  Awali, mwanasheria wa Serikali, Iddforce Makandara, aliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao wote kwa pamoja walimuua, Mugisa kwa kumpiga kitu kizito kichwani na kisha kumshambulia kwa mapanga hadi kufa.Aliiambia mahakama hiyo kuwa mwaka 2005 watuhumiwa hao walikula njama za kumuua Mugisa ambaye ni mume wake na Catherine John.  Alidai kuwa walifanya hivyo ili mjane wa marehemu aolewe na Makomelo, huku Lutonja akilipwa sh. 20,000 ili amsaidie kufanikisha mauaji hayo.Makandara aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wanaojichukulia sheria mkononi


`BABU WA KIKOMBE LOLIONDO AIBUKA



 Na Mwandishi Wetu




Mchungaji Ambilikile Mwaisapila (Babu wa Kikombe) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na dunia kwa ujumla.Alitoa kauli hiyo juzi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.Mchungaji Mstaafu Mwaisapila alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia, lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge.“Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameoneshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa kugawa kikombe ikiwemo mahema, maji na ulinzi.


Waziri Mkuu, Pinda ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo na migogoro ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch. Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo vitabadili sura ya Taifa hili."Mungu ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali. Tuna makaa ya mawe ambayo ni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati ya umeme kutoka ardhini (Geo-thermal) katika Ziwa Natron," alisema.Alisema Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu uliopo nchini. Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.


  Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijana mbele ya Waziri Mkuu, Elias Kalumbwa, alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa ili waweze kujiajiri kupitia kilimo cha mboga na matunda.Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita kijijini hapo.  Naye MarthaSereri (70) alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo la Ngorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote. Aliomba pia wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo kwenye tarafa yao.  Aliomba wapatiwe mikopo ya matreka ili waweze kuongeza ukubwa wa mashamba yao. “Tunaomba mikopo ya matrekta na plau, haya mashamba umeyaona njiani yamelimwa na Wakenya. Ukikodisha trekta kila ekari unatozwa sh. 100,000/-. Je tutafika wapi? Mkitukopesha matrekta mtakuwa mmetusaidia zaidi,” alisema.


  Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema hoja zao ni za msingi na kwamba suala la vijana kupatiwa bwawa ni jambo linalowezekana kupitia mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPS)."Andaeni andiko lenu, inabidi litoke kwa wananchi na si Serikalini. Mkituletea ni jambo linalowezekana kwani liko ndani ya mipango ya wilaya," alisema.  Akijibu hoja kuhusu ukubwa wa jimbo, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao kwamba inawezekana kuongeza jimbo isiwe suluhisho la matatizo yao kwa sababu ya jiografia ya eneo lao."Kuongeza jimbo inaweza isiwe jibu la kila kitu kwani matatizo mnayopata yanatokana na jiografia ya eneo lenu, kutoka Ngorongoro, Loliondo hadi huku Sale.Mimi nadhani tuangalie pia uwezekano wa kuwapa Halmashauri ili kusogeza huduma kwa wananchi. Tutaangalia njia zote mbili na kuona ipi italeta majibu ya haraka kwenu," alisema.


WATANZANIA WATAKIWA KUWEKEZA ANJOUAN


  Na Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kisiwa cha Anjouan nchini Comoro ili kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi ya kijamii na kiuchumi kati ya pande hizo mbili. Gavana wa Anjouan, Anissi Chamsidine,al ielezah ayoalipotembel eaKituo cha Uwe kezaji Ta nz ania(TIC) janajijini Dar es Salaam."Tuna fursa nyingi za uwekezaji katika kisiwa cha Anjouan na tunaamini Watanzania wako katika nafasi nzuri ya kuzitumia," alisema na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni wadamu na wa kihistoria.

   Alisema kuna umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika eneo la uwekezaji na kutaja maeneo ambayo yan ahitaji uwekezaji kuwa ni elimu,utalii,nishati na katika sekta ya afya."Tuna hospitali kubwa zinajengwa lakini tatizo ni kukosekana kwa wataalamu wa afya ikiwemo wauguzi na madaktari hivyo tunaomba Watanzania waje kutusaidia katika eneo hilo," alisema.

   Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Juliet Kairuki amesema kuwa ujio wa Gavana huyo na ujumbe wa wawekezaji utasaidia kufungua fursa za uwekezaji na ushirikiano mzuri kiuchumi kati ya nchi hizo.  "TIC na Serikali inathamini ziara ya Gavana na ujumbe wake, uhusiano wetu ni wa siku nyingi na tungependa kuimarisha," alisema na kuongeza kuwa ziara hiyo itasaidia kuvutia uwekezaji kutoka katika kisiwa hicho.

WATANZANIA WATAKIWA KUWEKEZA ANJOUAN

  Na Mwandishi Wetu  


Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kisiwa cha Anjouan nchini Comoro ili kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi ya kijamii na kiuchumi kati ya pande hizo mbili.


   Gavana wa Anjouan, Anissi Chamsidine,al ielezah ayoalipotembel eaKituo cha Uwe kezaji Ta nz ania(TIC) janajijini Dar es Salaam."Tuna fursa nyingi za uwekezaji katika kisiwa cha Anjouan na tunaamini Watanzania wako katika nafasi nzuri ya kuzitumia," alisema na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni wadamu na wa kihistoria.  

 Alisema kuna umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika eneo la uwekezaji na kutaja maeneo ambayo yan ahitaji uwekezaji kuwa ni elimu,utalii,nishati na katika sekta ya afya."Tuna hospitali kubwa zinajengwa lakini tatizo ni kukosekana kwa wataalamu wa afya ikiwemo wauguzi na madaktari hivyo tunaomba Watanzania waje kutusaidia 

katika eneo hilo," alisema.   Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Juliet Kairuki amesema kuwa ujio wa Gavana huyo na ujumbe wa wawekezaji utasaidia kufungua fursa za uwekezaji na ushirikiano mzuri kiuchumi kati ya nchi hizo.  "TIC na Serikali inathamini ziara ya Gavana na ujumbe wake, uhusiano wetu ni wa siku nyingi na tungependa kuimarisha," alisema na kuongeza kuwa ziara hiyo itasaidia kuvutia uwekezaji kutoka katika kisiwa hicho.

BALOZI WA HISPANIA KUWASHAWISHI WAFANYABIASHARA KUWEKEZA NCHINI


Na Gladness Mboma



 
Balozi wa Hispania nchini,Bw.Luis Cuesta amesema kuwa atawashawishi wafanyabias hara wa nchini mwake kuja kushirikiana na Watanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali kwa kuwa ina fursa nyingi za kiuchumi.  Bw.Cuesta aliyasema hayo juzi wakati alipomtembelea Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP, Bw.Reginald Mengi,ambapo alisema Tanzania ikitumia vizuri fursa mbalimbali z ilizopo wana nafasi kubwa ya kupiga hatua za kiuchumi.


  Alitaja fursa zilizopo nchini ni sekta ya gesi,utalii, mafuta na bahari na kusisitiza kwamba ikiwa maeneo hayo yataendelezwa yanaweza kusaidia nchi kupiga hatua kubwa.“Hispania ina watu wapatao milioni 43 ambayo inakaribiana idadi ya Watanzania, lakini sisi tumeweza kupiga hatua katika uchumi kutokana na kujikita katika sekta za nishati na utalii,”alisema.


Alisema kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya kibiashara ikiwemo amani,hali ya hewa, rasilimali, upatikanaji wa gesi na fursa nzuri ambayo inaweza kuwanufaisha Watanzania wote.Naye Dkt . Mengi alisema mazingira mazuri ya uwekezaji yatafanikiwa iwapo wawekezaji kutoka Hispania watakaokuja nchini wataungana na Watanzania katika ushirikiano.

“Kamakutakuw anaushirikiano wa dhatika tika sektambalimbali kati ya wawe kezaji wanjenaWatanz anianc hiinaweza kupigahat uaku bwa zakiuchumi.Dkt.Mengi alisema kuwa kunahaj a yaWatanzania kujifu nzamazu ri kutoka kwaHispaniahusu sanna mnailivyopiga hatuakati kasekta ya nishati na utalii. 

MFUMO WA ELIMU UBORESHWE NCHINI'



 Na Allan Ntana, Tabora

Serikali  kupitia watendaji wake imeshauriwa kuboresha mfumo wa utoaji elimu hapa nchini ili elimu hiyo iweze kumpa msingi mzuri na mwanga utakaomsaidia mwanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yake.Sambamba na hatua za kumuwezesha kufanya vizuri katika kujiendeleza kielimu.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Kanisa la FPCT hapa nchini, Mchungaji David Batenzi katika sherehe za mahafali ya 23 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Umoja iliyoko wilayani Igunga mkoani Tabora.Sherehe iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo inayomilikwa na kanisa hilo.Alisema, serikali inaweza kupitia upya mfumo wake wa elimu na ikiwezekana ikaufanyia marekebisho kwa lengo la kuboresha mtaala unaotumika kwa sasa ili mfumo huo uweze kumsaidia mwanafunzi kupata msingi mzuri kielimu." Hatujisik i vizuri tunapoona matokeo mabaya kwa wanafunzi wetu hasa yanaposababishwa na dosari kadhaa za kimfumo kutokana na kubadilishwa mara kwa mara pasipo kufanya utafiti, katika hili viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu hiyo hapa nchini wanapaswa kulaumiwa, mfano matokeo ya kidato cha nne mwaka jana hali ilikuwa tete," alisema askofu

VODACOM YAIPIGA 'JEKI' WIZARA YA MICHEZO

.Ibrahim Mussa na Theophan Ng'itu

 
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imekabidhi vifaa vya michezo kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo vyenye thamani ya sh.milioni 11,000,000 jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Kelvin Twissa alisema Vodacom ina furaha kushiriki katika mpango unaolenga kutambua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa ngazi ya shule nchini. "tunahitimisha ahadi tuliyoitoa kwako, kwamba tutakuunga mkono katika kufanikisha jambo hili pia Vodacom, tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kupitia wizara yako, hivyo nasi tunajisikia furaha kuwa sehemu ya mikakati ya serikali," alisema Twissa.

Aliongeza kuwa Vodacom, inatambua kuwa michezo ni sehemu ya kuzalisha ajira na kwa sababu hiyo hawaoni ugumu wa kuwekeza kwenye michezo, ili kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania. Vodacom ilikabidhi jezi seti 12, mipira 40 na kombe moja kwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Fenella Mukangara pia watatoa posho kwa ajili ya waamuzi na wasimamizi watakaoendesha mashindano hayo.

Naye Waziri Mukangara aliishukuru kampuni hiyo kwa kujitolea kushiriki katika kudhamini michezo mbalimbali nchini ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara. " Vifaa hivi ambavyo tumevipokea leo(jana) , tutavitumia katika mashindano ya soka yatakayoshirikisha timu 12 kutoka shule za sekondari za Manispaa zote tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, Temeke, Ilala na Kinondoni," alisema. Aliongeza kuwa wamechukua Mkoa wa Dar es Salaam kama mahali pa kuanzia, lakini wizara ingependa mpango huo uendelee katika mikoa yote Tanzania Bara.