TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 27, 2014

Chadema na mikutano yao

Sugu kuhutubia Chimara
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Chamara mkoani Mbeya juzi. 
 Katibu wa CCM
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Cadema), Dk. Willibrod Slaa akimnadi mgombea udiwani katika Kata ya Njombe Mjini kupitia chama hicho, Agrey Mtamba, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Njombe.
 Kumnadi Mgombea Njombe
Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Isitu, Chimara mkoani Mbeya, Felix Komba akizungumza katika mkutano wa Operesehni M4C Pamoja Daima mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, baada ya katibu huyo kujiunga na Chadema wakati wa mkutano huo uliofanyika Chimara Mkutano Makambako
Wananchi wa mji wa Njombe na vitongoji wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika mjini Njombe. Slaa kuhutubia Makambako
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Makmabako, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika.
 Slaa kuwasili Chimara 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwasili katika mji wa Chimara mkoani Mbeya, ambako alifanya mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika.

Mkutano wa Uzinduzi wa Maadhimishoya Sherehe za Miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM

TA1A0542 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] TA1A0557
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A0583
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A0814 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A0856 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa  CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Meet The NGOMA AFRICA BAND, the popular and most wanted band based in Germany

Field-Marshal ,Kamanda Ras Makunja(FFU),King of Anunnaki empire 
Soulful Vocals,Hypnotic Guitars and the driving Extraordinary rhythm of the “Bongo Dance” from East Africa

The NGOMA AFRICA BAND; known as the (Golden Voice of East Africa) or ” FFU- Field force unit”  is one of the few amongst african bands in Germany to have touched hearts and left audience dancing and week in the knees.
 Founded in 1993 and led by Tanzanian musician borned Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja - ”King of Anunnaki”.
Every concert is unique, uniting the audience after a few minutes on the dancing floor.
Bongo Dansi –meaning Dance able east african dance, is the ”Extraordinary Rhythm” that describes the NGOMA AFRICA BAND and makes the band the people´s choice.
Baptized under different names by excited fans – the Annunaki empire, FFU –Field Force Unit.
The NGOMA AFRICA BAND has succesfully written and released several hits amongst others the latest “Bongo Tambarare”, repertoires mostly in the native Tanzania and east african Kiswahili language.
Under the leadership and great visionary-Ebrahim Makunja AKA -Kamanda Ras Makunja; the NGOMA AFRICA BAND comprises of africa´s young and most talented musicians, drummers,guitarists bassist,percussionist, dancers amongst others multi-talented  soloist –Christain Bakotessa aka ”Chris-B”  Mo Benda,Jessy Ouyah, Flora William, Jonathan Sousa aka ”Jo Jo” ,Aj Nbongo making the NGOMA AFRICA BAND a complete travel party of eight vibrant musician and dancers.
Book The NGOMA AFRICA BAND and experience the extraordinary sensational Bongo dansi from East Africa´s best dancable music, best for indoor and outdoor festival and events of all kinds! Give your audience the best of Africa this season with the NGOMA AFRICA BAND

MPINGA CUP MZUNGUKO WA PILI MECHI ZILIZOFANYIKA KATIKA SHULE A MSINGI MUUNGANO MWISHONI MWA WIKI

100_1716 
 Wachezaji wa Timu ya Polisi Ufundi ya Temeke na Timu ya Lusaka ya temeke wakiwa wanawania mpira katika mechi mojawapo ya mashindano ya Mpinga Cup mzunguko wa pili, Timu ya Polisi Ufundi iliibuka na ushindi wa goli 1 – 0. 100_1717 
 Mchezaji wa Timu ya Kilimo Road ya Temeke akipiga moja ya mpira wa adhabu kuelekea katika lango la Timu ya Transforma ya Temeke, katika mchezo huu ndani ya dakika 90 timu zote zilitoka sare ya goli 1-1, na ndipo penalty zilpigwa ili kumpata mshindi na timu ya Transforma ilishinda kwa magoli 5 – 4.
 100_1723 
Mchezaji wa Timu ya Transforma ya Temeke akipiga moja ya penalti kuelekea katika lango la Timu ya Kilimo Road ya Temeke, katika mchezo huu ndani ya dakika 90 timu zote zilitoka sare ya goli 1-1, na ndipo penalti zilpigwa ili kumpata mshindi na timu ya Transforma ilishinda kwa magoli 5 – 4.
  100_1724 
Mchezaji wa Timu ya Kilimo Road ya Temeke akipiga moja ya penalti kuelekea katika lango la Timu ya Transforma ya Temeke, katika mchezo huu ndani ya dakika 90 timu zote zilitoka sare ya goli 1-1, na ndipo penalty zilpigwa ili kumpata mshindi na timu ya Transforma ilishinda kwa magoli 5 – 4.

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.

DV7A3218
     
 JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
·                  WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIKONGWE.
·                  WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA  BARABARANI.
·                  WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLIS KWA KUKUTW A NA BHANGI
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA NA WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA TUKIO LA  UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA  20:00HRS HUKO MAENEO YA  ISYESYE JIJINI MBEYA  AMBAPO OBADIA JONAS {41} MFANYABIASHARA  NA MKAZI WA ISYESYE ALINYANGANYWA GARI LAKE LENYE NAMBA ZA USAJILI T.675 CLX AINA YA  TOYATA KLUGER. MUHANGA ALIVAMIWA NA KUNDI LA WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA GETINI KWAKE AKITOKEA KATIKA BIASHARA ZAKE MAENEO YA ILOMBA JIJINI MBEYA, WATU HAO WAKIWA NA SILAHA AINA YA SMG PAMOJA NA MAPANGA WALIPIGA RISASI MBILI HEWANI KISHA KUWAAMURU KUSHUKA NDANI YA GARI NA KUMJERUHI MUHANGA KATIKA PAJA LA KULIA NA BAADAE KUONDOKA NA GARI HILO PAMOJA NA PESA TASLIM AMBAZO THAMANI YAKE BADO KUFAHAMIKA. JESHI LA POLISI LILIFANYA JITIHADA ZA MARA MOJA NA KUFANIKIWA KULIPATA GARI HILO. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWASAKA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI. MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI  AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII/WANANCHI  KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  WALIKO WATUHUMIWA HAO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. PIA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA WAWE MAKINI KATIKA KUSAFIRISHA FEDHA TOKA ENEO MOJA KWENDA LINGINE NA NI VYEMA WAWE NA USIRI. 

Sunday, January 26, 2014

China yachangia zaidi ya milioni 300 katika huduma za kijamii.


Lu Youqing 
Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing
………………………………………………………………………………………
Na Immaculate Makilika –Maelezo.
 
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China jana  katika uwanja wa Taifa wa  Uhuru jijini Dar es salaam imesheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano baina ya China na Tanzania ,ikiwa pia ni siku ya mwaka mpya wa kichina ambayo hujulikana kama sikukuu ya “Spring”.
Katika kusheherekea siku hiyo Serikali ya China pamoja na makampuni yamechangia zaidi ya milioni 300 katika huduma za kijamii,huku michango hiyo  ikiwa kama ifuatavyo; Serikali ya watu wa China imechangia milioni 100 kwa ajili ya kuchimba visima,Uhifadhi wa wanyamapori na mafunzo kwa wenyeji,wafanyabiashara wa China wamechangia milioni 50 kwa ajili ya visima na elimu huku Jumuiya ya Ujenzi wa Afrika wamechangia milioni 15 kwa ajili ya viatu vya wanafunzi.
Halikadhalika,Kampuni ya Madawa imechangia milioni 25 kwa ajili ya madawa ya kutibu malaria,huku milioni 100 zilichangwa na Jumuiya ya Muungano wa Wachina na fedha hizo zikielekezwa kwa vijana na wananchi wa Tanzania na kuhitimishwa na mchango kutoka Benki ya Biashara ya China ambayo imechanga milioni 20 kwa ajili ya vijana na elimu ya Tanzania.
Aidha ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu aliyekuwepo kwenye sherehe hizo kwa niaba ya Waziri Mkuu  Mizengo  Pinda, aliwashukuru sana watu Serikali ya China pamoja na wafanyabiashara na makampuni hayo  kwa misaada katika kuchangia maendeleo ya huduma za kijamii kwa watanzania.Urafiki wetu utaendelea kukua kwa faida ya watu wetu kama alivyosema waziri Nagu “China na Tanzania tunaurafiki wa dhati kwa muda mrefu sasa”.
Balozi wa China nchini Lu Youqing kwa upande wake alisema mwaka huu si tu kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini pia ni miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania.“Mwaka uliopita nchi hizi mbili zilikua na ziara kwa kiasi kikubwa ,huku tukishuhudia ujio wa Rais  wa China Xi jinping, hali hiyo imeleta msukumo mpya wa mahusiano unaolenga kuleta manufaa yenye usawa kwa nchi hizi mbili”.
Alisema watu wa China wamejidhatiti katika kujenga Taifa lao la China, watu wa Tanzania na Afrika kwa ujumla pia wamejidhatiti kufufua ndoto za maendeleo kwa nchi zao,tuungane sote pamoja katika kutimiza ndoto zetu za maendeleo katika mwaka huu mpya.
Sherehe hizo zilizohudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi wa China nchini,huku wakionekana wenye furaha wakati wote na kufuatilia kwa makini kila aina ya burudani iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo.
Bwana Jerome Wu,mwananchi wachina alisema hii ni mara yake ya tatu kuhudhuria sherehe za mwaka mpya wa kichina akiwa nchini Tanzania na kuongeza kuwa amefurahishwa sana na utofauti uliopo mwaka huu,na kupongeza jitihada zinazofanywa na Serikali za nchi hizi mbili katika kudumisha urafiki huo na kuongeza kuwa yeye hupata fursa ya kukutana na jamaa na marafiki kwenye sherehe hizi.
Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali na Jeshi  walihudhuria ikiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Asha Rose Migiro,Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Prof. Anna Tibaijuka na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele.
Uhusianao baina ya nchi hizi mbili ulianzishwa na Baba wa Taifa hayati Mwl Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong kwa nia ya kuhudumia wananchi wao,hatahivyo umekua ni uhusiano wenye manufaa makubwa kwa kusaidia kujengwa kwa reli ya Tanzania – Zambia,kiwanda cha nguo Urafiki, uwanja wa Taifa Uhuru, na miradi mingine ikiendelea ikiwa ni pamoja na  ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na bomba la gesi asilia toka Mtwara wakati miradi hiyo ikitazamiwa kuboresha uchumi na maisha ya watanzania pamoja na kudumisha urafiki huu baina ya Tanzania na China.

Mahakama Nkasi yamuamuru mume kujenga nyumba ya mtalaka wake

Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto wake wanne aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa amekaa kwenye kifusi cha sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa nyumba hiyo ili kumfukuza eneo hilo.MAHAKAMA ya mwanzo Mjini Namanyere, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imetoa amri ya kumtaka Ndebile Kazuri kujenga nyumba ya aliyekuwa mke wake Maria Tarafa iliyopo kijijini Isale ambayo aliibomoa akishinikiza mtalaka wake aondoke eneo ambalo alikuwa akikaa kabla ya kutengana.
Mwishoni mwa mwaka jana (2013) Mahakama hiyo ilivunja ndoa ya wanandoa hao wenye watoto wanne baada ya Kazuri kuwasilisha kesi mahakamani akitaka ndoa yake na mkewe ivunjwe. Hata hivyo baada ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo mke amewasilisha kesi mahakamani hapo akitaka mali za ndoa hiyo zigawanywe na mume awajibike kuwatunza watoto wake, jambo ambalo halikuzungumziwa kwenye kesi ya awali.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Bi. Tarafa alisema Mahakama ya mwazo imetoa amri ya kumtaka mtalaka wake kujenga nyumba aliyomvunjia yeye na watoto wake wanne akishinikiza aondoke nyumbani hapo, bila kupewa haki ya mgao wa mali zilizochumwa wakati wa ndoa.
“…Juzi tumetoka Mahakamani nilikwenda kufungua kesi nikiiomba mahakama igawe mali ambazo tulichuma na mume wangu muda wote wa ndoa yetu lakini mume wangu hataki zigawanywe, ila mahakama imemuamuru kwanza ajenge nyumba ambayo amenivunjia pale nyumbani nikiwa na watoto akitaka niondoke nyumbani, ameambiwa awe ameimaliza kabla ya Februari 14,” alisema Bi. Tarafa akizungumza kwa njia ya simu.

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII – TENGERU SANJARI NA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WIZARA

MHE. SOFIA SIMBA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO 
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inaadhimisha miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 27 Januari 2014 mpaka tarehe 31 Januari 2014.
Maadhimisho ya miaka 50 haya yataenda sanjari na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wizara utakaohusisha Maafisa Maendeleo ya Jamii  wa Mikoa na Wilaya kutoka Tanzania nzima wanaofanya kazi katika Halmashauri zetu, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Wadau wengine.

KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MWAKA 2014 NI;
“Taaluma ya Maendeleo ya Jamii: Nyenzo Muhimu katika Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini wa Kaya”.
Vilevile kutakuwa na maonesho  ya kazi za mikono, kutoka katika vikundi vya wanajamii wa Halmashauri za Arusha na Arumeru. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) watafanya maonyesho, pia watatoa huduma za afya kwa jamii.
Hivyo, wanakaribishwa wadau na wananchi wote kwa ujumla kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO KWA HISANI YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

DKT. BILAL AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO

`12 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo asubuhi Jan 26, 2014. Picha na OMR
01 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo asubuhi kwa ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65 zilipatikana kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi Julai. Kati ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni ahadi.Picha na OMR 
 1 
Picha ya pamoja 
 2 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
04
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jan 26, 2014. Picha na OMR 05
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jan 26, 2014. Picha na OMR
09 
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
10 11_1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
13_1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe. Picha na OMR
……………………………………………………………………….
Zaidi ya shilingi milioni 65 zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililoko jijini Dar es salaam.
Kati ya fedha hizo zilizokusanywa katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa jengo la ukumbi huo ilyoongozwa na Mhadhama Kadinali Polycap Pengo kiasi cha shilingi milioni 60.5 zilikuwa ni ahadi na  shilingi milioni 5 zikiwa ni fedha taslimu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za kidini katika kudumisha amani na upendo ndani ya jamii bila ya kujali tofauti za aina yo yote ile.
Alisema kuwepo kwake katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi mbali mbali za dini  nchini.
“Sisi Watanzania tumefika hapa kutokana na uongozi thabiti wa waasisi wa Taifa letu. Hivyo, tunataka nchi ya watu wanaomwogopa Mungu, watu wanaopendana, watu wanaovumiliana na watu wanaotakiana mema katika shughuli zao.”
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Bibi Rose Rupia kamati yake inahitaji shilingi milioni 600 zaidi kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa jengo la ukumbi huo na kwamba tayari wameshatumia kiasi cha shilingi bilioni moja katika ujenzi huo.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, DKT. ASHA- ROSE MIGIRO ATEMBELEA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

1. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) akipokea nakala za ripoti za Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiwemo Rasimu ya Katiba kutoka kwa  Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Tume hiyo aliyoifanya mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Saalam.
 2. 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) wakati alipowasili katika Ofisi za Tume hiyo kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa  Ofisi hiyo katika ziara yake aliyoifanya mwishoni mwa wiki.
 (PICHA NA TUME YA KATIBA)

TANZANIA KUISAIDIA MADAGACAR KUONDOLEWA VIKWAZO ILIVYOWEKEWA NA JUMUIYA ZA KIMATAIFA.


Picha na 1 
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013. Picha na 2
 Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo. Picha na 3 
Picha na 6
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa Madagascar  waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini. 
Picha na 4 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano, Rais wa Zambia Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry Raojolina. Picha na 5Viongozi mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo Picha na 7 
Gwaride maalum la jeshi la Madagascar wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina. Picha na 8 
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akikagua gwaride la majeshi ya Madagascar baada ya kuapishwa. Picha na 9
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiwasili Ikulu ya nchi hiyo mjini Antananarivo.
……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Antananarivo, Madagascar.
 
Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Madagascar katika masuala mbalimbali  na kuhakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na jumuiya za kimataifa vinaondolewa kufuatia nchi hiyo kurejesha utawala wa kidemokrasia.
Akizungumza katika mahojiano maalum  mjini Antananarivo, Madagascar, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa sasa serikali ya Madagascar imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano sio tu na Tanzania bali nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya za kimataifa.
Waziri Membe ambaye alikuwa amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Madagascar Bw. Hery Rajaonarimampianina zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo jana  amesema kuwa Tanzania imefurahishwa na hatua hiyo na kuongeza kuwa huo ni ushindi mkubwa kwa SADC.
Amesema kuwa mwaka 2009 Madagascar iliingia katika machafuko yaliyosababisha serikali halali iliyokuwepo madarakani ya Rais Mark Ravalomanana kupinduliwa na kufafanua kuwa Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Kitengo cha Amani na Usalama cha nchi za jumuiya ya SADC (TROIKA) imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inapatikana nchini humo.
“Kiongozi mpya wa Madagascar aliyepatikana na kuapishwa ni ushindi kwa Tanzania kwa sababu Rais Jakaya Kikwete amejihusisha sana na upatikanaji wa kiongozi huyo, kama tunakumbuka rais Kikwete alimuita nchini Tanzania kwa mazungumzo rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajoelina mara nne, mazungumzo haya yamezaa matunda tunayoyaona leo” amesema Mh. Membe.
Amefafanua kuwa yapo mambo makubwa ambayo Tanzania imeyafanya kufanikisha kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Madagascar ikiwemo upatikanaji wa katiba  ambayo ilikamilika mwezi wa 8 mwaka 2013 ,kufanikiwa kuwashawishi Andry Rajoelina na Mark Ravalomanana waliokuwa mahasimu kutoshiriki kugombea katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Amesema Tanzania imefurahishwa na kitendo cha rais Andry Rajoelina aliyeingia madarakani kwa kufanya mapinduzi kukubali kuachia madaraka na kuachia utawala wa demokrasia utawale nchini humo.
Ameeleza kuwa Tanzania sasa iko tayari kushirikiana na Madagascar na kama mjumbe wa SADC itahakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo vinaondolewa pia kuhakikisha kuwa kiongozi huyo mpya anashiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika utakaoanza tarehe 30 mwezi huu.
 “Tulimwahidi rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajolina kuwa atakapotekeleza hayo tunayoyataka ikiwemo kuanzisha mchakato wa katiba,  kuruhusu utawala wa demokrasia, na kuruhusu uchaguzi ili kupata rais mpya sisi tutakuwa mstari wa mbele kushawishi nchi za SADC na nchi za AU kuwaruhusu kushiriki mikutano yote ili waweze kuijenga nchi yao na jambo hilo tutalifanya ” amesisitiza Mh.Membe.
Katika houtuba yake mara baada ya kuapishwa rais Rajaonarimampianina amesema kuwa utawala wake unaanza ukurasa mpya wa kuijenga upya nchi hiyo iliyokuwa imegawanyika kisiasa na kusababisha chumi wake kudorora huku akiueleza umati mkubwa wa watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kuwa ataongeza mapambano dhidi ya rushwa na kuleta amani, utulivu na maridhiano kwa mustakabali wa taifa hilo.
Madagascar ambayo sasa inaingia katika utawala mpya wa rais Hery Rajaonarimampianina ambaye hapo awali alikuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo iliingia katika machafuko yaliyosababisha kuondolewa kwa utawala wa rais Mark Ravalomanana aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini.
 Hery Rajaonarimampianina  akiungwa mkono na rais aliyepita Andry Rajoulina anakuwa rais wa 4 wa nchi hiyo  kufuatia ushindi  mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013 uliompatia  asilimia 53.3  dhidi ya mpinzani wake Bw. Jean Louis Robinson aliyepata asilimia 46.5.

Ziara ya Waziri Mkuu mkoa wa Mtwara.

IMG_0135 
Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili kilichopo katika eneo la Madimba kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo na Petroli Tanzania (TPDC) Sultan Pwaga akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo. 
 IMG_2103 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitembelea maeneo mbalimbali kinapojengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba mkoani Mtwara wakati wa ziara yake mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa huo Kapteni mstaafu Joseph Simbakalia, kulia ni Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili  Sultan Pwaga
  IMG_2119 
Meneja Mkuu Ujenzi kiwanda cha Dangote Tanzania Bhupendra Sharma akimwonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda moja ya mashimo ambapo itafungwa mitambo ya kiwanda cha kutegeneza saruji eneo la Msijute mkoani Mtwara. IMG_2125
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikagua baadhi ya vifaa ambavyo tayari vimeshafika eneo la Msijute mkoani Mtwara kinapojengwa kiwanda cha saruji cha Dangote Tanzania. IMG_2143
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya sekondari Mstafa J.Sabodo wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipowatembelea shuleni humo kuwapa pole kwa msimba wa wanafunzi sita baada ya kugongwa na gari wati wa mchakamchaka karibu na eneo la shulke yao. IMG_2157
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda na Mke wake Mama Tunu Pinda wakimjulia hali moja ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mstafa J.Sabodo Chistopher Ngalapa (miaka 16 kidato cha pili) aliyelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Mtwara Lugora baada ya kupata ajili tarehe Januari 22, 2014.
 (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO Mtwara )

ZIARA YA VIONGOZI WA CHADEMA MKOANI MBEYA

Mabango Mbeya
Baadhi ya wananchi wa mji wa Mbeya wakiwa wabeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Lwanda Nzovwe mjini Mbeya jana. Silinde kuhutubia Mbeya
Mbunge wa Mbozi Mashariki, Davi Silinde (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
Slaa kuhutubia Mbeya 1
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana. Slaa kuondoka Makongorosi 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wakiondoka kwa shamrashamra, baada ya kuhutubia mkutano wa hadahara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Slaa na mtoto 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwa amembeba mtoto Sheila Shukurani (3), kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara matika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Sugu kuhutubia Mbeya 
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya na vitongiji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana.