Mhandisi
wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili kilichopo katika eneo la
Madimba kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo na Petroli Tanzania
(TPDC) Sultan Pwaga akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ziara yake ya kikazi ya
kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili
kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitembelea
maeneo mbalimbali kinapojengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la
Madimba mkoani Mtwara wakati wa ziara yake mkoani Mtwara. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa huo Kapteni mstaafu Joseph Simbakalia, kulia ni Mhandisi
wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili Sultan Pwaga
Meneja
Mkuu Ujenzi kiwanda cha Dangote Tanzania Bhupendra Sharma akimwonesha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda moja ya
mashimo ambapo itafungwa mitambo ya kiwanda cha kutegeneza saruji eneo
la Msijute mkoani Mtwara.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikagua baadhi
ya vifaa ambavyo tayari vimeshafika eneo la Msijute mkoani Mtwara
kinapojengwa kiwanda cha saruji cha Dangote Tanzania.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya sekondari Mstafa J.Sabodo
wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Pinda alipowatembelea shuleni humo kuwapa pole kwa msimba wa wanafunzi
sita baada ya kugongwa na gari wati wa mchakamchaka karibu na eneo la
shulke yao.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda na Mke wake Mama
Tunu Pinda wakimjulia hali moja ya wanafunzi wa shule ya sekondari
Mstafa J.Sabodo Chistopher Ngalapa (miaka 16 kidato cha pili) aliyelazwa
katika Hospitali ya mkoa wa Mtwara Lugora baada ya kupata ajili tarehe
Januari 22, 2014.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO Mtwara )
No comments:
Post a Comment