Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya
Leseni alizozitoa za uchimbaji Madini. Wanaoshuhudia, aliyesimama ni
Kaimu Kamshina wa Madini anayeshughulikia Leseni Bw. John Mayopa na
anayeangalia ni Kamshina wa Madini Paul Masanja.Mmoja
wa Wamiliki Kampuni ya J.S Contractors Bw. Sisti Siyvester Mganga
akieleza jambo kuhusu Kampuni ya J.S na namna itakavyofanya kazi.
Kampuni hii inatarajia kuzalisha madini aina ya ‘dimension stone’ na
kokoto za ujenzi katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo.Mwakilishi
wa Kampuni Ya Osiris Gold T) Ltd. Bw.Shehzada Walli akimweleza Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Prof esa.Sospeter Muhongo kuhusu Kampuni hiyo.
Leseni iliyosainiwa ya kampuni hiyo itaiwezesha kuchimba madini ya
Dhahabu katika eneo la Rwamgaza Geita.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Kamal Steel akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini
Leseni za Uchimbaji Madini. Kampuni hiyo imepewa Leseni ya kuchimba
madini aina ya ‘Marble’ katika eneo la Kidayi Kilosa.
Na Asteria Muhozya
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo ameweka saini Leseni tatu
za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha madini aina
mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli hizo.
Kampuni
zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction, inayomilikiwa na
Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw. Nakui Chen Kampuni
hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa wa km 0.29. Aidha,
shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo na
Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi za
granite.
Vilevile,
kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T) Ltd.
inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni
namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu
katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita
Aidha,
Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina ya Marble
kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari ambao
wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa. Kampuni
hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.
Wakati
akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa leseni
kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili
wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo
umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.
No comments:
Post a Comment