Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Iringa,Bi Jesca Msambatavangu akizungumza na wakazi wa
wilaya ya Mufindi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa kugombea
nafasi ya Udiwani
Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamejumuika katika kijiji cha cha Kilala Ibumu wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni za kugombea udiwani
Pichani ni Bwa.Hemed Mbena ambaye ndiye mgombea Udiwani katika kijiji cha Kilala Ibumu kupitia chama cha CCM akiwahutubia wakazi wa kijiji hicho,wilayani Mufindi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa kugombea nafasi ya Udiwani
Wananchi wametakiwa
kuwa makini katika kuchagua viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo na sio bora
kiongozi kwa kufuata ushabiki wa vyama.
Hayo yamesemwa na
katibu wa CCM wilaya ya Mufindi, MIRAJI MTATURU wakati wa uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi wa Madiwani katika kijiji cha kilala ibumu kata ya image wilaya ya
kilolo.
Mtaturu amesema kuwa
wananchi wanapaswa kutumia busara katika kuchagua viongozi na kuangalia chama
ambacho kinaweza kuwaletea maendele na sio kuchagua chama ambacho hawajui
kimetoka wapi wala hawajui kina malengo gani.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ,JESCA MSAMBATAVANGU amesema kuwa wananchi
wanapaswa kuchagua kiongozi anayetoka katika chama cha ccm kwani ndiyo chama
pekee kinachoweza kuwaletea maendeleo katika nchi na kutokimbilia chama cha
chadema kwa sababu kinachagia kuwapotosha vijana kwa kuleta fujo.
Aidha
amewataka
wananchi kuiamini CCM na kuipa uongozi huku akiwataka wananchi wa kijiji
cha Kilala Ibumu kumchagua HEMEDI MBENA ambaye ndiye mgombea udiwani
katika kijiji
hicho kupitia chama cha CCM.
No comments:
Post a Comment