Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua
iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara
hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa
China nchini, Lu Younqing.
Mke
wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akimsikiliza Waziri wa Nishati na Prof.
Madini Sospeter Muhongo akizungumzia ujenzi wa bomba la gasi eneo la
Bungu mkoa wa Pwani.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na msafara wake wakiangalia eneo utakapochimbwa mtaro wa kupitishia bomba la gesi.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba kabla ya kuyalaza na kuyafukia chini kwenye mitaro
Mkuu
wa mkoa wa Lindi akiwa na Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili mkoani
humo na kuendelea na ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu akimkaribisha
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho
kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa ujenzi
kiwanda cha MEIS faida zitzkazotokana na kiwanda hicho ikiwa ni pamoja
na upatikanaji wa gasi kijijini hapo kwa njia rahisi baada ya
kuunganishwa kutoka bomba kuu la gasi ikiwemo ajira kwa wanachi na
upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu ili kuboresha makazi yao.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha MEIS kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.
Picha ya sura na muonekano wa kiwanda cha MEIS kitakapokamilioka
……………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-Maelezo Mtwara
SERIKALI
imewapa jukumu wananchi wanaoishi maeneo linapopita bomba la
kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam la kulitunza na
kulilinda kwa manufaa yao na taifa zima.
Wito
huo ulitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Pinda leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi
wa mradi wa bomba hilo.
Waziri
Mkuu Pinda alisema Serikali inavihakikishia vijiji lilipopita bomba
hilo kuwa watapatiwa umeme unaotokana na uzalishaji wa gasi na utakuwa
wa gharama nafuu.
Zaidi
ya hayo, gasi itatumika kwa matumizi ya nyumbani kwa kuunganishiwa
bomba la gasi na ambao hawatafanikiwa watakuwa na fursa ya kupata
mitungi ya gesi ambayo itakuwa ya bei nafuu.
Waziri
Mkuu ameagiza mashirika ya Shirika la gasi na Petroli Tanzania (TPDC)
na Mradi wa Nishati Vijijini (REA) wachukue jukumu la kuboresha maisha
ya wananchi wa maeneo lilipopita bomba hilo katika maeneo ya barabara,
shule, kuwapatia maji safi na salama,kuwaboreshea utoaji wa huduma za
afya kwa kuboresha zahanati na vituo vya afya kama mchango wao kwa
jamii.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema
kuwa serikali kupitia shirika la TPDC na REA itahakikisha wanachi
waishio vjijini wanapata umeme mapema iwezekanavyo.
Kwa
kuthibitisha kauli hiyo Prof. Muhongo alisema serikali kupitia TPDC na
REA imetenga sh. Bilioni 20 kwa awamu ya kwanza ambayo itasimamiwa na
REA wakati awamu ya pili nayo itatumia bilioni 20 iotkaysimamiwa na
TPDC.
Katika
ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na mke wake bi Tunu Pinda, Balozi wa
China nchini, Lu Younqing, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter
Muhongo, mbunge wa Mchinga Said Matanda na Fatma Mikidadi mbunge wa viti
maalum.
Maeneo aliyotembelea Waziri Mkuu ni pamoja na Vikindu, Jopika, Bungu, Ikwiriri, Somanga, Somanga Fungu, Kitomanga na Lindi.
No comments:
Post a Comment