Meneja
Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi (kushoto), akimkabidhi Kamanada wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga,
taarifa ya zoezi la upimaji afya kwa madereva wa mabasi ya abiria na
malori iliyofanywa wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika Kituo cha
Mizani cha Mikese, mkoani Morogoro mwaka jana. Anayeshuhudia ni
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve
Kilindo. TBL ilifadhili zoezi hilo.
Mteknolojia
Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes
Rwenyagila (kushoto) akimkabidhi Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, taarifa ya zoezi la
upimaji afya kwa madereva wa mabasi ya abiria na malori lililofanywa
wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika Kituo cha Mizani cha Msata,
mkoani Pwani mwaka jana. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na
Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo.
Afande
Mpinga (wa pili kulia) akiwa na Kilindo wa TBL pamoja na madakari
waliowasilisha utafiti huo. Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia
alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi
na Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani,
Johannes Rwenyagila
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo
(wa pili kulia) akizungumza baada ya madaktari wa Hospitali za Tumbi na
Morogoro (hawapo pichani), kukabidhi matokeo ya upimaji wa afya za
madereva 800 mabasi ya abiria na malori wakati wa maadhimisho ya Wiki ya
Usalama Barabarani, mwaka jana katika vituo vya mizani vya Mikese
Morogoro na Msata Pwani. Zoezi hilo lilifadhiliwa na TBL. Aliyepokea
taarifa ya matokeo hayo, Dar es Salaam juzi, ni Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu na Berther Mturi
wa TBL.
Mteknolojia
Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes
Rwenyagila (katikati), akielezea jinsi walivyoendesha zoezi hilo. Kulia
ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria. Steve Kilindo pamoja na Afande
Kahatano wa kikosi cha usalama barabarani Makao Makuu.
Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi (kushoto), akielezea jinsi
walivyofanya utafiti huo.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga (katikati) akielezea kufurahishwa na matokeo ya utafiti
huo.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga (kulia), akionesha moja ya matokeo ya utafiti.
No comments:
Post a Comment