Mkuu
wa Mkoa Mhe. Ally N.Rufunga akipata maelezo ya maendeleo ya kiwanda
hicho mapema leo alipotembelea ili kuona shughuli zinazoendelea
Mashine za kuosha na kulainisha ngozi zikijaribiwa, chini ni ngozi zinazosubiri kuwekwa kwenye mashine hizo
Mkuu
wa Mkoa akioneshwa baada ya kazi ngozi laini inavyokuwa na tayari kwa
matumizi mbalimbali kama kutengeneza viatu,mabegi,pochi,n.k
Hizi ni mashine za kutengeneza yuzi katika kiwanda cha nyuzi na nguo kilichopo manispaa ya Shinyanga
Mkuu
wa Mkoa Mhe. Ally N. Rufunga akiona shughuli ya kujaribu mitambo katika
kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong leo alipotembelea kiwanda hicho
Kiwanda cha ngozi kilichopo manispaa ya Shinyanga ambacho kimekamilika na kazi ya kujaribisha mitambo inaendelea
…………………………………………………………………….
Kiwanda cha kutengeneza Ngozi kwa
ajili ya matumizi mbalimbali cha kampuni ya Kichina “Xiu hua” kilichopo
katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kimekamilika ambapo
mhandisi na msimamizi wa kiwanda hicho “Mr.Way” amesema kwa sasa
majaribio yanafanyika kabla ya kuanza uzalishaji wakati wowote.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametembelea kiwanda hicho mapema jana na kujionea majaribio ya mitambo ya kutengeneza ngozi za mbuzi,kondoo na ng’ombe.
Kiwanda hicho kinachotarajiwa kutengeneza jumla ya ngozi za kondoo na mbuzi Elfu kumi hadi 12 kwa siku na ngozi za ng’ombe 2500, kitaajiri zaidi ya Watanzania 500 ambapo Mr.Way amesema kipaumbele zaidi ni kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa pia ametembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Jielong Holdings, ameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Mr. Jerry Q kuwa wanaendelea kuzifanyia majaribio mashine na wakati wowote kitaanza kazi ya uzalishaji.
Mr.Jerry amesema kitaajiri zaidi ya wananchi 180 kitakapoanza uzalishaji na tayari kimeanza kuajiri.
Aidha,kiwanda cha kutengeneza nyuzi za nguo cha Dahong ambacho kinatarajiwa kuanza kazi mapema mwezi Machi baada ya kukamilisha kazi ya kufunga mashine mwishoni mwa mwezi Februari.
Msimamizi wa kiwanda hicho Mr.Saimon amesema kiwanda hicho kitaajiri wananchi zaidi ya 80.
Mhe.Rufunga amefanya ziara hiyo ili kujua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo vinatarajiwa vitakapokamilika pamoja na viwanda vingine, vitabadili sura ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo kwa kukuza uchumi wa mkoa,kwani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maisha ya wananchi wa Shinyanga yanabadilika kwa kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vitakavyozalisha ajira nyingi zitakazonufaisha wananchi.

No comments:
Post a Comment