Ni mara ya
kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya
Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili
alikokuwa amelazwa.Hakika @Ufoo Saro aliokoka kuuliwa mwaka jana
mwishoni@
Mtangazaji
wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye alijeruhiwa kwa
kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi, amefanya ibada na
kusema: “Namshukuru Mungu kwa kumponya.”
Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT)
Usharika wa Kibamba, Jimbo la Magharibi, Ufoo huku akitokwa na machozi
na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema: “Ni miujiza tu ya Mungu
yeye kunifanya mimi kuwa hai leo.”
Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili, aliwashukuru watu wote waliomtia moyo, kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa.
“Sina
cha kuwalipa, ninawashukuru sana kwa wema wenu, pia kwa kuniombea.
Mungu ni mkubwa na amenipigania, naendelea vizuri kwa sasa,” alisema na
kuongeza:
“Mungu
alinisimamia na nyinyi pia mliniombea, hakika sina budi kushukuru kwa
kila jambo. Nitasoma zaburi ya 146 katika Biblia Takatifu ili kumshukuru
Mungu kwa kunisaidia.”
Ufoo alisema kuwa ameamua kumshukuru Mungu kwa sababu siyo watu wote wanaopata matatizo kama yake wanapona.
Mchungaji aliyeongoza misa hiyo iliyoanza saa 1 asubuhi hadi saa 5 asubuhi,Joseph Maseghe alisema Mungu hakupanga Ufoo afariki dunia kwa kupigwa risasi.
“Mungu
bado anakuhitaji, hakupanga ndiyo maana upo nasi leo. Hautakiwi kulia
huu ni mwanzo wa maisha yako mengine, usilie unachotakiwa ni kumshukuru
Mungu kwa kila jambo,” alisema
No comments:
Post a Comment