Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akicheza draft na
vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nape
yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM
ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na
vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa
pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM
zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana
na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye
kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko
la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido
Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia
mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya
mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua
Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya
mara baada ya mpira kumalizika.
No comments:
Post a Comment