Nzega.
Zaidi ya magari 1,000 yamekwama kwenye Barabara Kuu ya Mwanza - Dar es
Salaam katika Kijiji cha Ngonho, Kata ya Miguwa, wilayani Nzega,
kutokana utekaji wa malori uliofanywa juzi usiku.
Kutokana
na tukio hilo, waligoma kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya
abiria na malori ya mizigo kukwama wakati abiria wapatao 3,000
wakitaabika kwa kukosa chakula na maji.
Madereva
hao waligoma kuondoa magari yao baada ya kukasirishwa na kitendo cha
polisi wa Nzega kushindwa kuwasaidia wakati walipotekwa.
Madereva
hao wameapa kutoondoa magari hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe au Mkuu wa Mkoa wa Tabora,
Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo hilo ili kusikiliza kilio chao.
Unyama wa watekaji
Mganga
Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, Emmanuel Mihayo alisema
watu walijeruhiwa vibaya kwenye utekaji huo kwa kukatwa masikio na
kutobolewa macho.
Dk Mihayo
aliwataja majeruhi hao kuwa ni raia wa Burundi, Herelina Eddy, ambaye
alitobolewa macho na hali yake ilikuwa mbaya na alikuwa kwenye
maandalizi ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga kwa matibabu zaidi.
Alisema
majeruhi wengine wawili wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali
hiyo. Majeruhi hao ni Abraham Ismail na Omary Adrian, ambao wote ni
wakazi wa Dar es Salaam.
Alisema Adrian alikatwa sikio na shavu pamoja na mkono wa kushoto wakati Ismail alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.
Polisi watuhumiwa
Mmoja wa
madereva waliotekwa, ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa
polisi wa Nzega waliombwa kutoa msaada lakini walikataa. CHANZO
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment