TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 17, 2014

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA MPYA WAOMBEWA NA MAKANISA ILI KUDUMISHA AMANI

 Mchungaji Kiongozi SILVANUS D. KOMBA (Punda wa yesu) akihubiri katika kanisa hilo.

 SSP - PITER SIMA akitoa hotuba yake katika misa hiyo kwenye kanisa la mlima wa moto.
 Mchungaji SILVANUS D. KOMBA akiwa katika maombi pamoja na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani PITER SIMA - SSP mwenye tai ya mistari katika kanisa hilo
 Baadhi ya wanakwaya katika kanisa hilo wakiiombea nchi kwenye misa hiyo
Makanisa yamekumbushwa kuwaombea wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mpya ili waweze kudumisha amani, utulivu, mshikamano na utengamano uliopo hapa nchini ili bunge hilo lisiwe sababu ya kuwagawa watanzania kwa matabaka ya kidini, kisiasa na kichama.
Ushauri huo umetolewa na Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God SILVANUS KOMBA,kwenye ibada ya kuliombea Bunge Maalum la Katiba na Taifa kwa ujumla iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo eneo la Sabasaba mjini Dodoma.
Alisema ili Wajumbe wa Bunge hilo wasiweze kuigawa Taifa kwa itikadi za kichama, kidini na kisiasa ni muhimu Makanisa yakatumia fursa zake kwa kueelekeza maombi kutoka ya Mungu ili kudumisha amani na utulifu ndani la Bunge hilo.
Mchungaji huyo katika mahubiri yake alisema kuwa kanisa hilo litaendelea kukemea kwa nguvu zote wale wote wanaochochea kwa maneno machafu yanayolichafua Bunge hilo pamoja na wajumbe na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Mrakibu mwandamizi wa Polisi PETER SIMA alisema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na serikali ina imani kubwa na Makanisa katika kuombea Taifa na Bunge la Katiba ambalo hivi sasa linaendelea kujadili Katiba Mpya.
SIMA akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP alisema kuwa makanisa yamekuwa yakifanya kazi yake kwa malengo ya kuwabadilisha watu wenye tabia mbaya kuwaweka kwenye usalama.
Alisema kwa upande wa Jeshi la Polisi hao kazi yao kuhakikisha inalinda usalama wa mali na watu wake, hivyo mambo yote hao yakifanyika kwa pamoja Taifa linakuwa katika hali ya usalama na hatimaye hata kwa Wajumbe wa Bunge wanakuwa salama.
“Ni imani yake kubwa katika maombi yaliyofanyika na kanisa hili, Katiba inayojadiliwa itapatikana na itawagusa Watanzania wote kutokana na juhudi za makusudi zinazofanyika ambazo waumini wamekuwa wakijitoa kwa ajili ya maombi” alisema Sima.

SERIKALI YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu  ya mwanafunzi  na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.
 Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani).




Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani). Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO).
========  =======  ========


UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU
UTANGULIZI
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.
Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa ujumla.
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.
Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA. Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates). Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.
Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imedhamiria kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.

VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA
MWAKA 2014 KIDATO CHA SITA
Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:
a)      Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.
b)      Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii
(i)         makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alamaB litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).
(ii)        Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.
(iii)       Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama Dna ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama F ilikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1.
c)      Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika
(i)         Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance),
(ii)        Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance),
(iii)       Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance),
(iv)       Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);
(v)        Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance),
(vi)       Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na
(vii)      Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance).
Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.
d)      Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D naE ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua kielimu ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.
e)      Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.
f)       CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya Kidato  cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama 10) na kazi mradi  au Projects (alama 5). Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.
g)      CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao  zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali.  Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo yaQT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.
h)      Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani  Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.
i)        Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.
j)        Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.




Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini:
Jedwali Na 1
MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU
ALAMA
UWIGO WA ALAMA
IDADI YA ALAMA
TAFSIRI
A
75 - 100
26
Ufauli Uliojipambanua
B+
60 - 74
15
Ufaulu bora sana
B
50- 59
10
Ufaulu mzuri sana
C
40 - 49
10
Ufaulu mzuri
D
30 - 39
10
Ufaulu Hafifu
E
20 - 29
10
Ufaulu hafifu sana
F
0 - 19
20
Ufaulu usioridhisha

Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.
Jedwali Na 2
MUUNDO WA MADARAJA
MUUNDO WA ZAMANI
MUUNDO MPYA
MAELEZO
POINTI
DARAJA
POINTI
DARAJA
7-17
1
7-17
I
Kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana
18-21
II
18-24
II
Kundi la ufaulu mzuri sana
22-25
III
25-31
III
Kundi la ufaulu mzuri na wa wastani
26-33
IV
32-47
IV
Kundi ufaulu hafifu
34-35
0
48-49
V
Kundi la ufaulu usioridhisha

Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.
HITIMISHO
Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big Results Now (BRN). Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.

Imetolewa,

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Python swallows an alligator crocodile while still alive & fighting

TANZANIA KUFAIDIKA NA BILIONI 480 KWA MWAKA

1 (10)

Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga, na Mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya habari Frank Mvungi 
2 (6)Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda  katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga  
3 (6)Mhandisi wa mradi wa  magadi soda  Godfrey Mahundi akitoa ufafanuzi kuhusu makadirio ya gharama za mradi huo ambao unakadiriwa kutumia  kiasi cha dola za kimarekani milioni 500. Katikati ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba na wa mwisho ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga 
PICHA ZOTE  NA. Georgina Misama-MAELEZO

JESHI LA POLISI LABAINISHA KUFUKUZWA KWA ASKARI WANNE KWA KUJIHSISHA NA UHARIFU.

Kamanda  wa kanda maalum ya Dar es salaam  Kamishina Suleman Kova akizungumza na wanahabari muda huu ofisini kwake juu ya kufukuzwa kwa askari hao. 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne wa Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu. Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi mbalimbali kama ifuatavyo:
·        
E.6396 CPL RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi.
·       F.9412 PC SIMON wa Kituo cha Polisi Kati.
·       F.9414 PC ALBERNUS  KOOSA wa Kikosi cha Bendi ya Polisi D’Salaam
·       F.9512 PC SELEMAN wa Kituo cha Polisi Kigamboni
Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba askari hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la tarehe 09/03/2014 eneo la Mbezi Beach “A” ambapo majambazi wapatao  15 walifika katika ofisi ya Kampuni ya Kichina ijulikanayo kwa jina la HONG 

YANG inayojishughulisha na ujenzi na uselemala.
Katika tukio hilo majambazi wapatao 11 wakivamia ofisi hiyo majira ya saa 04:30 Asb, na kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslim, simu, n.k. na kutoweka.

Imegundulika kwamba baadhi ya majambazi hai ni askari Polisi. Uchunguzi wa kina  umefanyika na watuhumiwa hao 11 wamepatikana ndipo ilipobainika kwamba askari Polisi hao walishiriki katika tukio hilo.
Watuhumiwa wengine saba wa ujambazi waliokamatwa ni hawa wafuatao:
·       GERADI S/O RAJABU MTUTU, Miaka 36, Mfanya biashara, mkazi wa Mtoni Mtongani.
·       CHARLES S/O HIZA MBELWA, Miaka 37, Fundi magari, Mkazi wa Kurasini.
·       ADAM S/O MKOMBIZI MOHAMED, Miaka 40, Mkazi wa Kariakoo.
·       ALLY S/O RASHID SALUM, Miaka 38, Mkazi wa Vingunguti Spenco.
·       SALUM S/O ABDUL MUSSA, Miaka 22, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbagala Kuu.
·       JUMA S/O SAID HAMIS, Miaka 29, Mkazi wa Yombo kwa Limboa.

·       JUMA S/O OMARI NGWELE, Miaka 50, Mfanyabiashara Samaki Ferry, Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.

Watuhumiwa wote hao wametambuliwa na mashahidi mbalimbambali katika tukio hilo. Kabla ya kufukuzwa kazi, askari hao walishtakiwa katika mahakama ya kijeshi na walipatikana na hatia hivyo wamepewa adhabu ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kulifedhehesha Jeshi la Polisi. wamefukuzwa kazi kuanzia tarehe 17/03/2014 na sasa si askari tena bali ni raia wa kawaida.
Aidha jalada la kesi hiyo pamoja na majalada mengine ya kesi ya wenzao waliowataja yatapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali hivi karibuni kabla ya kuwafikisha mahakamani kwa makosa jinai.
Pamoja na malezo hayo, Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Jeshi la Polisi na hatua hizi ni fundisho kwa askari wa cheo chochote atakayejaribu kwenda kinyume cha taratibu na maadili ya kazi.
Jeshi la Polisi litaendelea kuwazawadia askari wenye kufanya vitendo vya ujasiri vinavyoendena na tabia njema kama ilivyofanyika hivi karibuni tarehe 07/03/2014. Pia Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu maafisa, wakaguzi na askari watakaokiuka maadili au kukiuka mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi (Good Conduct)


BREAKING NEWS:BUNGE MAALUM LA KATIBA LAAHIRISHWA KUTOKANA NA VURUGU

 

Mwenyekiti wa Bunge Mh Samwel Sitta Amelazimika Kuhairisha Bunge Jioni Hiii mara baada ya Kutokea Vurugu.Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katika Jaji Joseph Sinde Warioba Alitakiwa kuwasilisha Rasimu ya Pili katika Bunge Hilo.Wajumbe wa Bunge Walipoingia Ukumbini Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Mh Samwel Sitta Alipomwita Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mh Jaji Warioba ,

Wakati Mwenyekiti Huyo aliposimama Kuanza Kuwasilisha Baadhi ya Wajumbe waliendelea Kugonga Meza  kwa Nguvu Kuhu Wakizomea na Kusababisha Vurugu Ndani ya Ukumbi wa Bunge na Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Mh Samweli Sita alipojaribu Kuingilia Kati Lakini ILishindikana Na Ikalzaimu Kuliahirisha Bunge Maalum La Katiba Mpaka hapo
Atakapotangaza tena.
Mtafaruku huo ni baada ya Wajumbe na Baadhi ya wabunge wa upinzani kupinga Jaji warioba asiwasilishe rasimu ya katiba leo mpaka Rais ahutubie Bunge hilo kwanza.Mwenyekiti wa Bunge akaruhusu Jaji Warioba aendeleee na Uwasilishaji lakini wabunge wakaanza kujibizana na kupiga makofi na meza za bunge.Baadhi ya wajumbe wametoka nje na wengine wamebaki ndani huku wakiwa wamesimamaEndelea Kuwa nasi Kwa taarifa zaidi

BUNGE LIMEHAIRISHWA MDA HUU BAADA YA MTAFARUKU KUTOKEA

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mh Sammuel Sitta amehairisha Bunge baada ya kutokea kutoelewana kwa wajumbe na wabunge wa bunge la katiba.Chanzo cha mtafaruku huo ni baada ya Wajumbe na Baadhi ya wabunge wa upinzani kupinga Jaji warioba asiwasilishe Rasimu ya Katiba leo mpaka Rais ahutubie Bunge hilo kwanza.Mwenyekiti wa Bunge akaruhusu Jaji Warioba aendeleee na Uwasilishaji lakini wabunge wakaanza kujibizana na kupiga makofi na meza za bunge.Baadhi ya wajumbe wametoka nje na wengine wamebaki ndani huku wakiwa wamesimama.

ANGALIA PICHA ZA NYUMBA YA KAPTENI WA NDEGE YA MALYSIA ILIYOPOTEA NA ABIRIA 227 POLISI WAIFUNGA NA WANAFANYA UCHUNGUZI

Compound: A view of the entrance to Zaharie Ahmad's residence. Police have been stationed outside for the last week

Compound: A view of the entrance to Zaharie Ahmad's residence. Police have been stationed outside for the last week
Officers are said to have spent two hours searching the pilot's home today inside the luxury compound
Officers are said to have spent two hours searching the pilot's home today inside the luxury compound
Luxury: Shah is said to live at the property with his wife Faisa
Luxury: Shah is said to live at the property with his wife Faisa


In Shah's house a flight simulator has been set up and is understood to have interested police following up one line of investigation - that he had used the equipment to practice making his real-life Boeing 777 ‘invisible’ by turning off all communications.

Today, a police van with a large contingent of officers inside passed through a security gate at the entrance to the wealthy compound where father-of-three Captain Zaharie Ahmad Shah lives with his wife Faisa.

Four plain-clothed police officers were also, reportedly, seen at the home of the other pilot Fariq Abdul Hamid, 27.


Both pilots live in the upmarket Kuala Lumpur district of Laman Seri, about an hour's drive from the city centre - and each was visited today by a team of detectives who arrived in a white 'people mover' vehicle.

The homes are substantial and are, said one resident, typical of high income earners.
It is believed a team of search specialists entered Shah's house and spent two hours searching for signs of foul play, before moving into search the co-pilot's home a short distance away.
The New Straits Times reported last night that before police turned up at Hamid's home, his two brothers arrived there in a Mini Cooper, believed to belong to a friend.
They hurried into the house and remained there for a short time before hurrying away in the same car, taking with them transparent blue plastic bags containing clothes and toiletries.
Fariq's father, Abdul Hamid left with them. An hour later, the plain clothed officers left the house carrying two brown bags.


The concentration by police on the homes of the Captain and the co-pilot adds to suspicion that one - or both - of them might have had been responsible for the plight of the aircraft.Despite the investigation, Malaysian officials and friends of the pilots have told MailOnline this week that there are no reasons to suspect either the Captain or co-pilot of having personal problems that would have resulted in them taking control of the aircraft.

Mr Razak added authorities have not ruled out any possibilities in the international search for the plane, which now involves 14 countries, 43 ships and 58 aircraft.

'Clearly the search has entered a new phase. Over the last seven days, we have followed every lead and looked into every possibility,' Mr Razak said. 'For family and friends (of the passengers), we hope this new information brings us one step closer to finding the plane.'
Entrance: The gates outside the home of co-pilot Fariq Abdul Hamid who is also under police investigation
Entrance: The gates outside the home of co-pilot Fariq Abdul Hamid who is also under police investigation
Journalists gathered outside Hamid's home in Shah Alam as police turned their attention to those on board as part of the wide-ranging probe
Journalists gathered outside Hamid's home in Shah Alam as police turned their attention to those on board as part of the wide-ranging probe
Suspicions: Jonti Roos (centre) claims she and her friend were entertained by Fariq Abdul Hamid, 27, who is one of the pilots of the missing Malaysia Airlines flight (right). He is now part of an investigation by police in Kuala Lumpur
Suspicions: Jonti Roos (centre) claims she and her friend were entertained by Fariq Abdul Hamid, 27, who is one of the pilots of the missing Malaysia Airlines flight (right). He is now part of an investigation by police in Kuala Lumpur

Sunday, March 16, 2014

JIMBO LA CHALINZE KUMEKUCHA RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA HARAKATI ZA KUSAKA KURA


Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa wakazi wa Kijiji cha Miono,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano ya Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.
Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi (kulia) akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kabla ya kumpatia kipaza sauti ili aweze kuzungumza na wanakijiji

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014, wakati akiwasili kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.