Mchungaji Kiongozi SILVANUS D. KOMBA (Punda wa yesu) akihubiri katika kanisa hilo.
Baadhi ya wanakwaya katika kanisa hilo wakiiombea nchi kwenye misa hiyo
Makanisa yamekumbushwa kuwaombea wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mpya ili waweze kudumisha amani, utulivu, mshikamano na utengamano uliopo hapa nchini ili bunge hilo lisiwe sababu ya kuwagawa watanzania kwa matabaka ya kidini, kisiasa na kichama.
Ushauri huo umetolewa na Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God SILVANUS KOMBA,kwenye ibada ya kuliombea Bunge Maalum la Katiba na Taifa kwa ujumla iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo eneo la Sabasaba mjini Dodoma.
Alisema ili Wajumbe wa Bunge hilo wasiweze kuigawa Taifa kwa itikadi za kichama, kidini na kisiasa ni muhimu Makanisa yakatumia fursa zake kwa kueelekeza maombi kutoka ya Mungu ili kudumisha amani na utulifu ndani la Bunge hilo.
Mchungaji huyo katika mahubiri yake alisema kuwa kanisa hilo litaendelea kukemea kwa nguvu zote wale wote wanaochochea kwa maneno machafu yanayolichafua Bunge hilo pamoja na wajumbe na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Mrakibu mwandamizi wa Polisi PETER SIMA alisema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na serikali ina imani kubwa na Makanisa katika kuombea Taifa na Bunge la Katiba ambalo hivi sasa linaendelea kujadili Katiba Mpya.
SIMA akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP alisema kuwa makanisa yamekuwa yakifanya kazi yake kwa malengo ya kuwabadilisha watu wenye tabia mbaya kuwaweka kwenye usalama.
Alisema kwa upande wa Jeshi la Polisi hao kazi yao kuhakikisha inalinda usalama wa mali na watu wake, hivyo mambo yote hao yakifanyika kwa pamoja Taifa linakuwa katika hali ya usalama na hatimaye hata kwa Wajumbe wa Bunge wanakuwa salama.
“Ni imani yake kubwa katika maombi yaliyofanyika na kanisa hili, Katiba inayojadiliwa itapatikana na itawagusa Watanzania wote kutokana na juhudi za makusudi zinazofanyika ambazo waumini wamekuwa wakijitoa kwa ajili ya maombi” alisema Sima.
No comments:
Post a Comment