Ligi kuu soka Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho machi 19 mwaka huu kwa mechi kali ya vuta ni kuvute kati ya mabingwa watetezi, Young Africans dhidi ya makamu bingwa Azam fc , itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Shirikisho la soka Tanzania kupitia kwa Afisa habari wake, Boniface Wambura Mgoyo limesema tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu .
Vituo vilivyotajwa ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.
Wambura aliongeza kuwa baada ya saa 6 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 mchana.
Pia afisa habari huyo alibainisha viingilio katika mechi hiyo kuwa ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.
Wambura alimtaja mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam kuwa ndiye atakayechezesha mechi hiyo, huku akisaidiwa na Anold Bugado (Singida), Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam).
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa ni Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.
Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi kesho utakubali kuingia mfukoni na kulipa milioni 15 zingine endapo uharibifu utatokea uwanja wa Taifa?
Wakati mechi hiyo ikisubiriwa kwa hamu, kuna baadhi ya mambo yanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la tatu.
Siku za karibuni mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wamekuwa wakifanya vurugu ndani ya uwanja wa Taifa, huku wengine waking`oa viti kuashiria kupinga baadhi ya mambo yakiwemo maamuzzi ya waamuzi.
Mashabiki wa timu hizi kubwa wamekuwa wakikosa ustaraabu na uvumilivu pale timu zao zinaposhindwa kupata matokeo.
Pia maamuzi ya waamuzi yamekuwa chanzo cha vurugu hizi ambapo mashabiki huwa wanawalaamu marefa kuvurunda.
Kuna wakati kweli waamuzi wanakosea kwa sababu za kibinadamu, kwani hakuna aliyeumbwa mkamilifu.
Linapokuja suala la baadhi yao kufanya maamuzi nje ya sheria 17 za soka, hapo inakuwa ngumu kutafsiri kwanini inakuwa hivyo.
TFF wanatakiwa kuwakumbusha waamuzi kuwa mechi ya kesho ina uzito mkubwa mno katika harakati za ubingwa wa Tanzania bara.
Yanga wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo la pointi baina yao na vinara Azam fc.
Mpaka sasa Yanga wao nafasi ya pili kwa pointi 39 nyuma ya Azam waliopo kileleni kwa pointi 43.
Kama Azam fc atashinda kesho inawezekana ikawa mguu ndani- nje kutafuta ubingwa wake wa kwanza tangu kuingia ligi kuu msimu wa 2008/2009.
No comments:
Post a Comment