Serikali 2 zitaendeleza hisia za Utanganyika kwa kasi
Mkuu wa Nchi kamaliza kuhutubia Bunge la Katiba. Kimsingi kaegemea upande wa msimamo wa Serikali 2 ambao ndio msimamo wa CCM chama anachoongoza. Hata hivyo kasisitiza kuwa iwapo tunataka Serikali 3 basi tuzingatie hofu zilizopo ikiwemo masuala ya Uraia, uwezo wa kifedha wa Serikali ya Muungano nk.
Ni dhahiri kero za Muungano zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50 haziwezi kutatuliwa na muundo ule ule uliozitengeneza.
Jawabu la muungano wa Tanzania ni muundo wa Serikali tatu wenye Serikali ya Muungano yenye nguvu na rasilimali. Tunaloweza kuongeza ni kuweka mfumo wa Tawala za Mikoa wenye kupanua demokrasia zaidi kwa kuchagua wakuu wa mikoa na kufuta wakuu wa wilaya.
Ni dhahiri Uraia itakuwa ni 'deal breaker' kwenye suala la muundo wa Muungano. Hili litajibiwa kwa kuwa na Nchi moja, dola moja na Serikali tatu.
You may also Like
Mtatiro:Kumpa Warioba Dakika 60 nikinyume na kanuni...
Angalizo! Kukataa muundo wa serikali tatu ni sawa na kulivun...
Mtikila: Wameanza kutufunga ‘Luku’
Zitto aungana na CCM kutaka kura ya wazi...
Kitila Mkumbo: Upinzani wa Tanzania ni dhaifu,chama kimoja k...
Mgombea Umakamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba...
No comments:
Post a Comment