Maandalizi ya mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge kupitia CCM jimbo la Chalinze yaendelea vizuri ambapo jioni ya leo Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajiwa kuhutubia wakazi wa Chalinze na Vitongoji vyake pamoja na kumnadi mgombea wa ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
Barabara Kuu iendayo mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha ikiwa imependeza kwa bendera za CCM ,ambapo masaa machache yajayo kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za ubunge CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mratibu wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze akisoma vichwa vya habari vya magazeti ya leo kwenye moja ya vibanda vya magazeti Chalinze huku sehemu kubwa ya maeneo yote yakiwa yamebandikwa mabango yenye picha za mgombea kiti cha ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
Mratibu wa Kampeni za Ubunge CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye akibadilisha na Kamanda wa Vijana wilaya ya Bagamoyo Ndugu Haidary Mohamed wakati wa kukagua hatua za mwisho za maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa Kampeni.
Shumina Sharif Kiongozi wa kampeni kata ya Msata na Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa akiwa na mratibu wa kampeni za ubunge za CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni jimbo la Chalinze.
Mratibu wa Kmapeni za Chalinze CCM Nape Nnauye akijadiliana jambo na maofisa wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM jimbo la Chalinze.
No comments:
Post a Comment