- Wateja zaidi ya 300 kupata huduma kila siku katika tawi hilo
NMB
ikiwa ni benki chaguo la watanzania wengi. Jana Machi 19, 2014
ilifungua rasmi tawi lake jipya maeneo ya Sinza Mori mkabala na kituo
cha kuwekea mafuta cha ‘Big Born’ ikiwa na lengo la kuwafikia wateja
wake, ambapo takribani zaidi ya wateja 300 wamekuwa wakihudumiwa kila
siku katika tawi hilo.
Tawi
hili limeanza kufanya kazi hivi karibuni, ambapo limeonekana kuwa ni
msaada mkubwa kwa wakazi wa Sinza ikiwa ni moja kati ya maeneo yenye
wakazi wengi jijini Dar es salaam.
Hii
itakua pamoja na mitaa jirani kama, Kijitonyama, Mabatini,
Afrikasana,Tandale, Sayansi na maeneo mengine kwa kupata huduma za
kibeki kwa uharaka zaidi.
Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Sinza.
Wa
Kwanza kulia ni ni Meneja wa Tawi la NMB Sinza Bi.Kidawa Masood na
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Bw. Salie Mlay wakishuhudia
ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Akizungumza
katika ufunguzi huo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Bw. Salie
Mlay alisema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo ni kuwapa huduma kwa
ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo.
Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi hilo limekuwa ni mkombozi
kwa wateja wengi wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na
watu mbalimbali.
“Tawi
letu linatoa huduma zote za kibenki, na tunazidi kuwakaribisha wateja
wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benki yetu na pia tunatoa
huduma mbalimbali zikiwemo za Mashine za kutolea fedha(ATM) ambayo
hufanya muamala kwa masaa 24”
Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay (kati) akimwelezea Afisa
Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi (pili kushoto)
huduma mbalimbali zitolewazo na tawi jipya la NMB Sinza.
Ufunguzi wa tawi hili la Sinza unafanya idadi ya matawi yaliyopo Kanda ya Dar es Salaam kufikia ishirini na tatu.
Hivyo basi, kuifanya NMB kuendela kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
Tawi
hili linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa NMB kama mikopo ya pikipiki
za miguu miwili na mitatu, kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha nk.
Pia
litakua linafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu
asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi – 10:30 jioni) na
Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana
(2:30 asubuhi- 6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na
huduma ndani ya tawi hili.
Sehemu wa wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo
Akizungumza kwa upande wake wakati wa ufunguzi huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Afisa
Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi aliipongeza
benki ya NMB kwa kutambua umuhimu wa huduma za kifedha na kusogeza
karibu na jamii ili iweze kufaidika na kuwataka wananchi na wateja wapya
kutumia tawi hili pekee katika eneo hilo ili kupata huduma za kibenki
badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyo
mbali.
No comments:
Post a Comment