Kamera za usalama zikimwonyesha rubani wa ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777, Zaharie Ahmed Shah, kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.
Mwanafunzi, Firman Siregar, akiwa na wazazi wake, ni mmoja wa abiria 239 waliokuwa katika ndege hiyo yenye orodha ya safari namba Flight MH370.
Mwandishi wa habari akichukua picha nyumba ya rubani Fariq Abdul Hamid eneo la Shah Alam, karibu na Kuala Lumpur.
Maafisa nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege hiyo kutoweka.
Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, au goodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
Juhudi za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.
CHANZO: PICHA DAILYMAIL / HABARI BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment