Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Pendo Gondwe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani leo kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji wa kituo hicho John Mnali na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Frank Mvungi.Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji wa kituo hicho John Mnali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani leo kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Pendo Gondwe. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe, akizungumza na kituo cha Tv1 baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la The Citizen, Henry Mwangonde akiuliza jambo wakati wa mkutano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
………………………………………………………………………………….
Na Frank Mvungi- Maelezo
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili miradi 9,442 tangu kuanzishwa kwake hadi 2013.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa TIC, Pendo Gondwe wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Gondwe alisema kuwa Watanzania wamekuwa na muamko katika uwekezaji ambapo katika miradi yote miradi ya Watanzania ni asilimia 52 na 25 ni miradi inayomilikiwa kwa ubia kati ya wageni na watanzania.
Aliongeza kuwa asilimia 23 ni miradi iliyowekezwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali ambapo alisema miradi ambayo inaongoza kwa uwekezaji ni Kilimo, Maliasili, Miundombinu, Nishati, viwanda na biashara, Usafirishaji, Elimu, Afya, Miundo mbinu na madini.
Alisema TIC inawahamasisha Watanzania kujitokeza kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kusaidia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Gondwe alisema TIC imekuwa na utaratibu wa kuhamasisha wananchi kushiriki katika uwekezaji katika sekta nmbalimbali ambapo kituo hicho kimekuwa kikitumia mikutano na makongamano kuhamasisha wananchi kusajili miradi yao.
Kituo cha uwekezaji kinatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya wawekezaji wa ndani kupitia dirisha moja yaani ONE STOP CENTRE ikiwemo kuandikisha kampuni, kujisajili na VAT, TIN, na leseni mbalimbali.
No comments:
Post a Comment