Mama
wa mtoto Dorothea Njavike (1) ambaye aliunga moto mkoani akiwa mchanga
na kuathirika kwa kupata ulemavu, Milka Kabelege (kulia), mama mkubwa wa
mtoto huyo, Salome Kyegulo (kushoto), wakiwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam juzi ambapo wamefika
jiji kupata matibabu katika Hospitali Maalumu ya CCBRT. Gharama za
kusafiri kutoka mkoani Mbeya kwa ndege kuja Dar es Salaam zimefanywa na
Bohari ya Dawa (MSD). (PICHA KWA HISANI YA MSD)
…………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
BOHARI
ya Dawa (MSD), imejitolea kumsafirisha hadi Dar es Salaam kwa matibabu
katika Hospitali ya CCBR mtoto Dorothea Njavike (1) aliyepatwa na janga
la kuungua moto mkoani akiwa mchanga.
MSD
na CSR wamejitolea kummsafirisha mtoto huyo juzi pamoja na mama yake
mzazi Milka Kabelege, mama yake mkubwa Salome Kyegulo kwa ajili ya
kumsaidia mtoto huyo wakati wa matibabu yake katika hospitali hiyo
maalumu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam.
“Baada
ya kupata taarifa ya kuungua mtoto huyo kupitia vyombo vya habari sisi
MSD tuliguswa tukaona ni vizuri tumsaidie kumsafirisha mtoto huyo kwa
ndege pamoja na wazazi wake kuja Dar es Salaam kwa kupata matibabu na
kuwarudisha mkoani Mbeya baada ya matibabu” alisema Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa.
Dorothea,
ambaye ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la moto amepata ulemavu
sehemu za uso, ambapo pua, mdomo, kidevu na jicho moja viliungua pamoja
na mikono yake yote miwili kuanzia sehemu za maungio ya viganja.
Kutokana
na hali hiyo juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na vikundi
mbalimbali hadi kufikia uamuzi wa kumpeleka jijini Dar es Salaam kwa
matibabu.
Kwa
mujibu wa mmoja wa wawezeshaji kutoka kundi la Motherhood la Dar es
Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Anitha alisema madaktari watakao
mtibu mtoto huyo ni kutoka Tanzania ambao wataungana na wale wa mataifa
mengine kwa ajili ya kuangalia namna ya kuweza kurekebisha uso na maeneo
mengine yaliyoathiriwa na moto huo.
Mmoja
wa madaktati aliyempokea mtoto huyo juzi baada ya kufika katika
Hospitali ya CCBRT ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema
mtoto huyo ataanza kupata matibabu kwa hatua za awali wakati
zikisubiriwa taarifa zaidi zilizomo kwenye faili lake kutoka Hospitali
ya Rufaa ya Mbeya akikokuwa akipatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment