Watendaji
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari wakipanda
kwenye boti ndogo kwa ajili ya kuelekea kwenye kisiwa cha Bongoye
kufanya mkutano.
Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa wamefika kwenye kisiwa cha Bongoye. Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari, wakielekea kwenye sehemu ya kufanyia mkutano. Msemaji
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Mohammed Bahari akizungumza na
waandishi wa habari juu ya ruzuku kwa wavuvi.Katikati ni Afisa Habari wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi na mwisho ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi. Meneja
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk.
Milali Machumu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani).Katikati ni Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Mohammed
Bahari na mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank
Mvungi. Mkurugenzi
Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ruzuku kwa
wavuvi.Katikati ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank
Mvungi na mwisho ni Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Mohammed
Bahari. Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mohammed Bahari akizungumza na
waandishi wa habari juu ya ruzuku kwa wavuvi. Baadhi
ya Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na waandishi wa habari,
wakiteremka kutoka kwenye Boti baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Sea
Cliff wakitokea kisiwa cha Bongoye ambako ndiko kulikofanyika mkutano na
waandishi wa habari. Picha zote na Hussein Makame
………………………………………………………………………….
Frank Mvungi- Maelezo
SERIKALI
imetenga Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya ruzuku kwa wavuvi katika
kipindi cha mwaka wa Fedha 2013/14 ili kusaidia kukuza sekta ya uvuvi
hapa nchini
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt.
Mohammed Bahari wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam.
Dkt
Bahari amesema kuwa ruzuku hiyo itatolewa kwa kuzingatia vigezo ikiwemo
waombaji kuwa na vyama vya ushirika na vilivyosajiliwa kisheria.
Alitaja
vigezo vingine kuwa ni chama cha ushirika kiwe kinafanya kazi za uvuvi
kufuatana na sheria ya uvuvi na 22 ya mwaka 2003 na kanuni za uvuvi za
mwaka 2009 na miongozo mbalimbali.
Aliongeza
kuwa chama hicho kiwe na akaunti benki iliyo hai na kithibitishe kuwa
na uwezo wa kuchangia asilimia 40% ya gharama ya mradi husika, ambapo
Serikali itachangia asilimia 60% ya gharama ya mradi husika.
“Chama
husika kitapitisha maombi yao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika kwa
ajili ya kupitia maombi hayo na kuona kama yanakidhi vigezo viliwekwa na
baada ya hapo kuwasilishwa Wizarani” alisema Dk. Bahari.
Alisema
miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na ununuzi wa boti za uvuvi, injini
na vifaa vingine vitakavyowawezesha wavuvi kuongeza tija katika shughuli
za uvuvi
Dkt
Bahari alifafanua kuwa ruzuku hiyo kwa wavuvi itakuwa na manufaa
makubwa kama vile kuongeza mapato ya wavuvi na wafanyabiashara wa mazao
ya uvuvi.
Aliongeza
kuwa ruzuku hiyo pia itaongezeka maduhuli ya Serikali, kupunguza
vitendo vya uvuvi haramu,kuimarika kwa biashara ya mazao ya uvuvi na
kuongeza ajira katika sekta ya uvuvi.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi
alitoa wito kwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya uvuvi haramu
kuacha tabia hiyo mara moja kwa kuwa Serikali imeimarisha doria katika
maeneo yote .
Aliongeza
kuwa kwa wale wanatumia nyavu ambazo zimepigwa marufuku nao waache
mara mara moja tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa
wale wote watakaokwenda kinyume cha sheria ya uvuvi na. 22 ya mwaka 2003
na kanuni zake za mwaka 2009.
Alizihimiza
Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa sheria za uvuvi na kanuni zake
zinazingatiwa kikamilifu na kuwa uvuvi haramu na biashara ya samaki
wachanga vinadhibitiwa katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment