Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia katika hafla fupi ya
uzinduzi rasmi wa kampeni ya Tohara kwa wanaume Mkoani Rukwa
iliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi. Akihutubia
katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu 2014
Mkoa wa Rukwa unatakiwa uwe umeshafanya tohara za wanaume 22, 000 ikiwa
ni agizo la kitaifa ambapo hadi sasa jumla ya wanaume 7,000
wameshafanyiwa tohara.
Kwa
mujibu wa mratibu wa zoezi hilo Mkoani Rukwa tangu kampeni hiyo ianze
tarehe 17 Machi 2014 hadi jana tarehe 20 Machi 2014 jumla ya wanaume 583
wameshafanyiwa tohara ndani ya siku 4 katika kituo kilichopo tarafa ya
Challa. Kampeni hiyo inaenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU ambapo
kati ya wananchi 699 waliopimwa ni mmoja tu amekutwa na maambukizo ya
virusi hivyo katika tarafa hiyo ya Challa.
Akizungumzia faida za tohara kwa wanaume amesema husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi pamoja na kusaidia kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiwasalimia wananchi wa
tarafa ya Challa waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni
hiyo.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akizungumza katika hafla
hiyo. Akizungumzia juu ya zoezi hilo la tohara amesema tohara kwa
wanaume husaidia kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi
kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Zoezi la Tohara likiwa linaendelea katika zahanati ya Challa.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa Ndugu Smythies Pangisa awasalimu wananchi wa Challa.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha
(watatu kulia), Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Albinus Mugonya
(wa tano kulia) na watumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali Kuu ya
Mkoa wa Rukwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment