Na:zuhura Masoud.
Hoteli
ya Kimataifa ya Ikondolelo ya Kibamba jijini Dar es Salaam, imeendelea
kuwa gumzo kutokana na kuweka burudani mbali mbali ndani ya Kumbi
zinazopatikana katika hoteli hiyo ambayo ni ya kisasa na yenye adhi ya
kimataifa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakazi wa Maeneo tofauti tofauti ya Jijini Dar es
salaam , wamesema kuwa wanampongeza mkurugenzi wa IKONDOLELO HOTELI kwa
kuweka miundombinu kabambe ya kuhakikisha wakazi wa maeneo mbalimbali
wanapata fursa ya kushiriki Kimichezo ya aina mbalimbali iliyopo katika
hotel hiyo.
Aidha
Hoteli hiyo ambayo imejengwa kwa ustadi mkubwa, imewekewa mandhari ya
kuvutia kwa wageni wote wanaopata fursa ya kwenda kutembelea maeneo hayo
ikiwamo wakazi wa jiji wanaokwenda kwa lengo la kujiburudisha kwa njia
mbali mbali ikiwamo, Kuogelea, kucheza Poltable,Burudani ya Muziki na
mengine mengi.
Hata
hivyo wameogeza kusema kuwa, hapo awali kabla ya hoteli hiyo kujengwa
maeneo hayo, kwao burudani zilikuwa zikionekana tu kama ni kwa baadhi ya
watu kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu kitendo kilichokuwa
kinawaweka katika Dunia ya giza na kuwaondoa katika utandawazi wa Dunia
ya Sayansi na Teknolojia.
IKONDOLELO
ambayo kwa ujumla imejengwa kwa Ustadi mkubwa, imefanikiwa kuwekewa
Bwawa la kuogela la kisasa ambalo linakidhi mahitaji ya watu wa aina
zote nje na ndani ya jimbo la Ubungo kwa ujumla ikiwemo na maeneo ya
Kibaha wilaya ya Pwani.
mbali
na bwawa hilo pia IKONDOLELO ni moja ya Hoteli ambayo inamazingira ya
kupendeza hususani kuna maeneo ya kupendeza kwa ajili ya mapumziko kwa
watu walio na fungatena serehe mbalimbali kupata kumbi kuwa zenye uwezo
wa kuingiza watu wengi pamoja na waleMikutano, na mengine mengi.
katika
Hoteli ya IKONDOLELO kati ya vitu ambavyo pia vinaonekana kuwavutia
wakazi wa maeneo hayo ni pamoja na Eneo la Maegesho ya Magari(Parking)
ambayo ni ya kipekee kutokana na kila mgeni mwenye usafiri kuwa na
uhakika na Ulinzi wa Mali ama vifaa wanapokuwa ndani ya Hoteli hiyo .
Meneja
wa Hoteli hiyo Bwana, Samweli mnyika ambaye aliweka wazi kuwa kutokana
na kutambua hali ya maisha na mahitaji ya watu, waliamua kuweka burudani
kwa lengo la kuwaweka watoto na vijana karibu na mazingira ya nyumba
zao pasipokutoka kwenda mbali ususani wakati wa sikukuu ambazo burudani
zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu wote waoapata
fulsa ya kuingia ndani ya IKONDOLELO.
Aidha
amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia wamezingatia ubora wa gharama kwa
wahitaji, ambapo alisemakuwa garama zao ni nafuu kwa wale wanaokwenda
kwa ajili ya kukodi Ukumbi kwa ajili ya Maharusi na sherehe alimbali.
naye
Mkurugenzi wa Hoteli hiyo bwana Philip Selekwa Humbie alisema kuwa
anawashukuru wote wanaoendelea kumpa ushirikiano katika kuijenga upya
Hoteli hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwa ndiyo Hoteli kubwa kuliko
zingine inayopatikana maeneo ya Jimbo la Ubungo, ikiwa CCM Kibamba, njia
ya Kibwegele.
"Binafsi
ninawakaribisha sana wateja wangu ambao wanapata muda na kuweza kuja
hapa, kwa hiyo niseme kuwa nawapenda kwa kuwa wanapata fulsa pia ya
kuniunga mkono, na hata nyinyi wandishi pia nawakaribisha, hapa kwangu
kuna kumbi nyingi, mnaweza hata kuja kubadilisha manzali kwa ajili ya
sherehe zenu, au hata mje mpate kuogelea kama unavyoona jinsi watu
walivyowengi yaani wanaendelea kufurahi kila mmoja kwa nafasi yake.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU HIZI
0713210839 au 0712884082
0713210839 au 0712884082
No comments:
Post a Comment