NAIBU
waziri wa fedha,Mwigulu Nchemba amesema, kukua kwa
utandawazi kumeifanya dunia kuwa kijiji , hivyo kuna kila hali ya
kuimarisha majeshi
ya ulinzi ya ndani kwa kushirikiana na majeshi ya nchi za nje kwa
kuyaongezea ujuzi zaidi wa kinadhalia katika kuimarisha usalama wa nchi.
Kauli
hiyo ameitoa jana katika mahafari ya kwanza ya kuhitimu kozi ya mafunzo
mkakati kwa maafisa wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)kutoka chuo cha
mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) baada ya kumaliza kozi ya mwaka mmoja
katika chuo cha uhasibu Njiro(IAA),ambapo jumla ya maofisa 52 kutoka nchi 10 za Afrika wahitimu kozi ya shahada ya udhamili na stashahada na kutunukiwa vyeti .
Nchemba
alisema kuwa kwa sasa nchi nyingi za afrika haziitaji kupigana kwa
ajili ya kupata uhuru ila zinahitaji ulinzi ili kupiga hatua katika
masuala ya kiuchumi wakati nchi hizo zikiwa salama ,hivyo alitoa rai kwa
mafunzo hayo kuendelezwa zaidi katika program mbalimbali ambazo
zitasaidia wahitimu kufanya vizuri zaidi katika kuimarisha utendaji wa
kazi zao.
Alisisitiza
kuwa lazima majeshi ya kiafrika yajiendeshe kisasa zaidi kwa kutumia
elimu na ujuzi kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya ndani na nje ili kwendana na hali ya utandawazi na teknolojia ya kisasa.
Naye
mkuu wa chuo hicho Prof,Johannes Monyo alisema kuwa ushirikiano wa chuo
cha uhasibu Arusha na chuo cha kijeshi Monduli ulikuja kwa kutiliana
saini mapema mwaka jana,katika kutoa taaluma hiyo baada ya mitaala yake
kupitishwa na taasisi ya elimu ya juu(Nacte).
Alisema
mafunzo hayo yatawasaidia wanajeshi hao na raia kuongeza ujuzi katika
shughuli zao,na kwamba chuo hicho kinatarajia kuanzisha program
nyingine ya mafunzo inayotarajiwa kuanza mapema mwakani,baada ya mtaala
yake kukamilisha na kupitishwa.
Monyo
alisema makubalinao ya kuanzisha mafunzo hayo yanawezesha chuo hicho
kupeana mafunzo juu ya kuboresha masuala mbalimbali ya kitaaluma ikiwemo
katika sekta ya fedha,utawala na diplomasia.
Aliongeza
kuwa mafunzo hayo yatawasaida pia kuwapa ujuzi wa kimkakati katika
masuala ya Kiuongozi ,kutatua migogoro,usimamizi
wa miradi,Diplomasia,Mawasiliano na sekta za kiraia, na matumizi
ya teknolojia .
Alisema
chuo hicho kilianza kutoa kozi ya kwanza kwa maofisa wa jeshi zaidi ya
52 pamoja na wakufunzi kutoka TMA wanaotoka katika Nchi mbalimbali zikiwemo za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Afrika (SADC) .
No comments:
Post a Comment