Mtoto Njiti akiwa amebebwa na mama yake.
WANAWAKE Mkoani Singida wamehimizwa kujenga tabia ya kuwakumbuka wanawake wenzao waliofungwa na walioko mahabusu gerezani ili waendelee kuaminiwa kuwa bado ni sehemu muhimu ya wanawake mkoani humu.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa la Free Pentekoste church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida mjini, Lessi Jaredi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wanawake wanatumikia adhabu jela na wale walioko mahabusu katika gereza la wilaya ya Singida.Msaada huo ulikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wananwake duniani.
Amesema wanawake waliopo magerezani, hawajapoteza utu wao na wala sio kwamba hawana msaada tena katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya watoto waliozaliwa kabla ya kufikia umri wa kuzaliwa (Njiti) ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida.
“Wanawake hawa ni wenzetu, ndugu zetu na watoto wetu, wapo gerezani kwa lengo la kusaidiwa kurekebisha baadhi ya mienendo na tabia zao tu. Kwa hali hiyo, tunapaswa kuwapenda,kuwathamin na kuwajali, ili kuondoa uwezekano wao wasianze kuhisi kwamba, wametengwa au sio sehemu muhimu ya jamii”,alifafanua Mwenyekiti huyo.
Akisisitiza zaidi, Lessi amesema wanawake hao waliopo gerezani wakitembelewa na hasa na wanaweke wenzao na kukpewa misaada, kitendo hicho kitawatia moyo na kamwe hawatakata tamaa katika maisha yao.
“Nitumie fursa hii kuwahimiza wanawake wa jimbo la Singid mjini na wa mkoa wetu wa Singida kwa ujumla, tujenge utamaduni wa kuadhmisha siku ya wanawake duniani, kwa kuwatembelea wanawake wenzetu walioko magerezani, haspitali na wenye matatizo mbali mbali, ili makundi hayo yaweze kutembua kwamba tunayajali na kuyathamini”,amesema.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo pia amewahimiza wanawake kuwatembelea wanawake walioko katika hospitali mbali mbali baada ya kujifungua watoto na hasa wale ambao watoto wao hawakufikisha umri wa kuzaliwa (njiti).
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida, Lessi Jaredi akimwombea mtoto Njiti ili Mungu aweze kumsaidia kuongeza uzito stahiki ambao utatoa fursa kwa wao kupewa ruhusa ya kurejea nyumbani kwao.
Amesema wanawake hao wanapaswa kufarijiwa mara kwa mara, sio tu na ndugu zao, bali na wanawake wengine kwa sababu wanalazwa muda mrefu wakisubiri watoto wao wafikishe uzito unaotakiwa.
“Sisi leo (jana 8/3/2014) wanachama wa UWW FPCT, tumetembelea wanawake sita walioko hospitali ya mkoa ambao wamejifungua watoto njiti. Tumebaini kwamba wana kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wao njiti, wanafikisha uzito unaotakiwa. Kazi hiyo ambayo ni pamoja na kuwalisha kikamilifu ili kupata uzito stahili, inawalazimu kukaa hospitalini kwa mud amrefu”,alifafanua.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao licha ya kuhifadhiwa kwenye chumba chenye joto, pia wapo wengine ambao wanalazimika kupakatiwa kifuani na mama zao, ili kuuunganisha ngozi ya kifuani ya mama na ya mtoto, kwa lengo mtoto njiti,apate joto la mama yake aweze kukua na kuongeza uzito.
Add caption |
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) Lessi Jaredi, akikabidhi msaada kwa mmoja wa wanawake waliojifungua watoto hawajafikia umri (Njiti) wa kuzaliwa.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu.
No comments:
Post a Comment