VIONGOZI wa serikali mkoa wa Dodoma wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Rehema Nchimbi wakiwa wamejipanga tayari kumpokea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa kutembelea mradi wa visima virefu vya maji eneo la Kibaigwa, wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.
Mradi huo wa maji una thamani ya zaidi ya shilling billion 2.3.
Ufunguzi wa mradi huo ni sehemu ya maadhimisho ya 26 ya Wiki ya Maji ambapo kitaifa yanafanyika Dodoma tarehe 16-22/03/2014. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment