Mwenyekiti wa Benki ya Covenant Balozi Salome Sijaona akimkabidhi mratibu wa uhamasishaji wa vikundi vya Wilaya ya Temeke Bi.Tukae Kondo ufunguo wa pikipiki baada ya kuwapatia mikopo wajasiliamali mbalimbali.Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi imewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo na mitaji. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenat Sabetha Mwambenja, akiwasisitizia jambo juu ya kurejesha mikopo baadhi ya wajasiriamali waliopata mikopo ya pikipiki iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasilia mali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo . Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Balozi Salome Sijaona
Mwenyekiti wa Benki ya Covenant Balozi Salome Sijaona akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano cha Yombo Vituka cha jijini Dar es Salaam,Charles Rweyemamu ufunguo wa gari aina ya basi lenye thamani ya shilingi Milioni 45 .Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant Sabetha Mwambenja akiongea na Waandishi wa habari juu ya benki hiyo kutoa mikopo kwa wajasiliamali wadogo nchini ili waweze kujikwamua kimaisha kwa kuwapatia mitaji ambayo ilijumuisha Basi la abiria ,pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment