TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 17, 2014

TIMU BORA UTAFUTA USHINDI UWANJANI-MASHABIKI WASEMA USAJILI WA TIMU KUBWA NI ZAIDI YA MAMILIONI

Na:Mwandishi Wetu.

MPIRA wa miguu ni mchezo unaochezwa hadharani. Mipango ya timu uwanjani, umakini wa wachezaji kutumia nafasi na juhudi za timu, bila kusahau mchezaji mmoja mmoja huamua matokeoa kirahisi.
Kuna mchezo mchafu unaotajwa kuchezwa na viongozi wa timu, waamuzi na makocha wa timu zinazoshiriki ligi kuu.
Si rahisi kufahamu mambo haya kwasababu hufanywa kwa mtandao mkubwa na kwa siri kubwa.
Kibaya zaidi wapo viongozi wanaoendesha mpira na hutuhumiwa kushiriki katika njama za kutafuta matokeo nje ya uwanja.
Ni kawaida kuona kiongozi wa mpira kitaifa ana unazi na timu fulani, hivyo anajihusisha na mchezo mchafu.
8Vinara Azam fc, pointi 43 wataweza kuandika historia ya kutwaa ubingwa msimu huu kwa mara ya kwanza?
Kila zinapokuja mechi muhimu zaidi, tabia ya mashushu kuzingira miji ambayo mechi zitachezwa husikika.
Mara nyingi utasikia kuna jopo la watu limetumwa kutoa rushwa kwa wachezaji wa timu pinzani ili kupata matokeo kirahisi.
Pia wachezaji wengine wanatuhumiwa kuuza mechi ili kujipatia fedha isiyohalali, huku wakisahau kuwa wanawaumiza mashabiki wao.
Wachezaji wanafahamu wazi kuwa kuna watu nyuma yao ambao hupoteza pesa zao, muda wao kwa kuwafuata popote walipo kuwashangilia.
Unadhani mtu anayetoka Tunduma-Mbeya Mpaka Dar es salaam, au kaitaba mjini Bukoba anafaidika na nini?.
Huyu mtu anatumia pesa zake ambazo hazirudishwi na mchezaji wala kiongozi wa timu, bali inakuwa hasara kwake.
Anafika kukushangilia, halafu kwa tamaa zako unachukua `vijisenti` na kucheza hovyo.
Ukiwa mwanandinga unafurahia kuona kuzirai au kazimia kwa mashabiki uwanjani?. Unafaidika nini sasa?. 
IMG_0610Ndoo wanaitetea msimu huu?: Yanga wapo nafasi ya pili wakijikusanyia pointi 39 
Najua huwezi kuwalipa mashabiki wako kwa kukushangilia. Fadhila pekee ya kuwarudishia ni kuucheza mpira kwa kiwango cha juu na kuwafurahisha.
Huu mchezo wa kupanga matokeo na kuhonga timu pinzani unatajwa sana na bila shaka upo na wanaohusika wapo.
Nao waamuzi wameshaingia katika sakata hili. Ni kawaidia kumuona mwamuzi akivurunda kwa makusudi kabisa.
Yapo makosa ya kibinadamu, lakini kuna wakati mwamuzi anazidisha , na kwa bahati mbaya hatuna mfumo mzuri wa kupitia maamuzi baada ya mechi.
Wenzetu huwa wanarekodi mechi, baada ya hapo jopo la waamuzi hukutana na kuitazama, makosa yote hubainishwa na mwamuzi husika huulizwa.
Je, ulikuwa sahihi kutoa adhabu kwa makosa haya?. Mwenyewe utamsikia akisema ile haikuwa kadi kabisa, hivyo wanao uwezo wa kufuta maamuzi na kumchukulia hatua kama alifanya yale kwa makusudi.
Kwetu hapa hatujafikia hatua hiyo zaidi ya kusubiria ripoti ya makamisaa wa mechi ambao pia hutajwa kuhusika katika rushwa.
mbeya-cityWataweza kutwaa ubingwa?: Mbeya City wapo nafasi ya tatu kwa pointi 39, tofauti na Yanga wenye pointi 39 nafasi ya pili  ni mabao ya kufunga na kufungwa
Nakumbuka wakati Simba sc wakijiandaa kukabiliana na Mbeya City uwanja wa Sokoine, viongozi wa Mbeya City walisikika wakisema kuna mashushu wa Simba wametumwa Mbeya.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel Kimbe alihojiwa na mtandao huu na kueleza kuwa kuna vikao vilikuwa vikifanyika na mashushu hao kuihujumu klabu ya Mbeya City.

No comments:

Post a Comment