TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, March 25, 2014
Monday, March 24, 2014
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak asema na jamaa na familia za abiria wa ndege iliyotoweka MH370 , kwamba hakuna manusura
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.
SHIRIKA la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura. Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.
Mpaka sasa AUTRALIA ilikuwa ikiendelea na udadisi picha za Satelite kusaka mabaki ya ndege hiyo ya Malaysia.
pamoja na ua ushirika wa Nchi za Norway, New Zealand na Marekani katika kutafuta mabaki hayo, tangazo hilo limekuja huku juhudi za
kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara la Hindi zikimalizika kwa
siku na siku bila mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita. Ndege na meli za nchi mbali mbali zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.BBC
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita. Ndege na meli za nchi mbali mbali zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.BBC
KINANA ASIMAMA KIDETE KUHAKIKISHA CCM INAIBUKA KIDEDEA JIMBO LA CHALINZE
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ubena Zomozi huku akishangilia kwa
shangwe,leo Machi 24,2014.
Mgombea
Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani
Jakaya Kikwete akimwaga sera zake kwa Wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi
wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali
mbali ndani ya jimbo la Chalinze.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ubena Zomozi huku akishangilia kwa
shangwe,leo Machi 24,2014.
Wananchi
wa Kata ya Ubena Zomozi wakifatilia kwa makini sera za Mgombea Ubunge
katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya
Kikwete huku wakiwa wamejikinga kwa mvua kwa kutumia viti,wakati wa
Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya
jimbo la Chalinze.

Wananchi
wa Kata ya Ubena Zomozi wakiwa wamejikinga kwa mvua chini ya paa la
moja ya Nyumba zilizopo kwenye Kata hiyo wakati wa Mkutano wa Kampeni za
CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la
Chalinze.
SIKU YA 17 KUPOTEA NDEGE YA MALAYSIA: NDEGE YA MALAYSIA ILIRUKA CHINI YA FUTI 12,000.
Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Warren Truss, kulia, akizungumza na ofisa wa juu ya kikosi cha uokoaji na mratibu wa operesheni ya kuitafuta ndege iliyopotea, John Rice.
NDEGE ya abiria ya Malaysia iliyopotea kiutatanishi wiki mbili zilizopita, inadaiwa iliruka chini ya futi 12,000 kutoka usawa wa bahari kutokana na matatizo katika chumba cha rubani kabla ya kupotea katika rada, ripoti mpya zimeeleza.
Wakati ndege hiyo Boeing 777-200 ikiwa bado inatafutwa katika bahari ya Hindi, habari zinasema chombo hicho kilibadili uelekeo ikiwa juu ya bahari ya Kusini ya China.
Mara ya mwisho ndege hiyo ilionekana katika rada ya jeshi la Malaysia saa 2.15 asubuhi kwa saa za nchi hiyo, Machi 7 mwaka huu, ikiwa katika kisiwa cha Penang kilicho kusini mashariki mwa taifa hilo, muda kama saa moja baada ya kuwa imeruka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing nchini China.
Mapitio ya Rada yalionyesha ndege hiyo ikibadili mwelekeo baada ya kugeuka ghafla na kwa kasi upande wake wa kushoto kuelekea Malacca.
Ofisa mmoja aliyekataa kutajwa jina kwa vile siyo msemaji, aliiambia CNN kwamba kuruka chini ya futi 12,000 katika anga yenye ndege nyingi kama ilipokuwa ikipita kungeifanya ndege hiyo kutoonekana na ndege zingine.
CHANZO: DAILYMAILY
MWANAFUNZI MAKONGO AFARIKI KATIKA AJALI YA BAJAJ NA LORI JIJINI DAR ES SALAAM
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo, Priscus Mallya, baada ya kufariki katika ajali ya lori na Bajaj.
Bajaji ambayo mwanafunzi alikuwa amepanda akielekea shuleni Makongo ikiwa eneo la ajali.
MWANAFUNZI wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Makongo, Priscus
Mallya, amefariki dunia katika ajali iliyolihusisha lori na Bajaj katika
barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Bamaga, Dar.
Kwa mujibu wa watu waliokuwa eneo la tukio wakati ajali hiyo
ikitokea, wamesema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ndani ya Bajaj pamoja na
wenzake wawili wakielekea shuleni Makongo ambapo walikutana uso kwa uso
na lori kisha kumrusha na kutokea upande wa pili marehemu.
(PICHA/STORI: ANDREW CARLOS, DENIS MTIMA/GPL)
TAZAMA SIMBA ILIVYOVUTWA SHARUBU UWANJA WA TAIFA NA COASTAL UNION!!
Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani wakati wa mchezo wao na Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wakisalimiana.
Benchi la ufundi la Simba.
Kikosi cha Coastal Union ya Tanga.
Kikosi cha Simba.
Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa Simba wakichagiza ushindi.
Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Coastal Union ya Tanga, Hamadi Juma katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Coastal ilishinda 1-0.
ASHABIKI SIMBA WATULIZWA JAZIBA, LOGA KUSUKA KIKOSI KAZI KUWAVAA AZAM , KAGERA SUGAR, ASHANTI, YANGA MECHI ZILIZOSALIA!!
Na Baraka Mpenja
KIPIGO cha bao 1-0 walichopokea Simba sc kutoka kwa Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga jana uwanja wa Taifa katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kimezidi kuwavuruga na kuwafanya wawe wanyonge ngwe hii ya lala salama.
Wagosi wa Kaya wakiwa katika morali ya ushindi , waliandika bao la ushindi dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa mlinzi wake wa pembeni, Hamadi Juma kufuatia mabeki wa Simba kujikoroga.
Matokeo hayo yamepokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaona kama ligi kuu inawaonea msimu huu.
Hata hivyo Uongozi wa Simba sc kupitia kwa Afisa habari wake, Asha Muhaji umewataka mashabiki na wanachama wao kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao.
“Matokeo ya jana hatukuyatarajia hata kidogo. Tumeshitushwa mno na kipigo hicho. Lakini hayo ndio mambo ya uwanjani. Mpira umechezwa vizuri na tumepoteza. Hatuna budi kuukubali ukweli japo unauma”. Alisema Asha.
Mwamuzi vipi?: Kocha wa Simba sc, Dravko Logarusic (wa kwanza kulia) akiwa hailewi cha kufanya na kuonesha kuwa muda bado wakati mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho
Shughuli ilikuwa pevu mno jana uwanja wa Taifa
Afisa habari huyo aliongeza kuwa kutokana na matokeo wanayozidi kuyapata, yanawapa watu cha kusema, lakini soka huwa lina tabia ya kupanda na kushuka.
“Siku za nyuma mashabiki wetu walikuwa wanatoka na furaha uwanjani. Kwa sasa mambo yamebadilika. Huo ndio Mpira, ukiupenda lazima uwe na moyo wa kukubaliana na kile kinachotokeo”. Alisema Asha.
Asha alisisitiza kuwa bado wamebakiwa na mechi nne, hivyo mashabiki waendelee kuiunga mkono klabu yao ili iweze kufanya vizuri.
IDDI BONGE BAADA YA KUMPIGA MWAKASANGA SASA AMTAKA MCHUMIATUMBO!!
| Bondia Amani Bariki ‘Manny chuga’ kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Selemani Moto wakati wa mpambano wao Many chuga alishinda kwa TKO ya raundi ya nne |
Bondia Kasimu Gamboo kulia akipambana na mohamed babeshi wakati wa mpambano wao Ganmboo alishinda kwa k,o ya raundi ya tatu ya mpambano huo.
| REFARII OMARI YAZIDU AKIMWINUA MKONO JUU BONDIA KASSIMU GAMBOO |
| BONDIA aLi Bugingo kushoto akioneshabna umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Mandula mandula alishinda kwa pointi |
Bondia iddi bonge akiwa ulingoni
Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
Bondia Iddi Bonge kushoto akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika mpambanio huo.
Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge’ mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga ‘Shoka ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam
mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na filimbi
Bonge alipiga ngumi ya kwanza na kumfanya ‘Shoka ya Bucha ‘ kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba ya uzito wa juu
mara baada ya mpambano huo bondia Iddi Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu
katika mpambano huo uliosindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally Jagalaga uku Amani Bariki ‘ Manny Chuga’ akimsambaratisha kwa TKO ya raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma bondia Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya raundi ya nne
Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa
WASHIRIKI 29 WA SHINDANO LA MAISHA PLUS 2014 WAINGIA RASMI KIJIJINI
Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi… Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya). Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Mkuu wa Kijiji… Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea… ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi… washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka… wengine walitamani kughairi kuendelea na safari. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe… Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Subscribe to:
Posts (Atom)




















