Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.
SHIRIKA la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura. Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.
Mpaka sasa AUTRALIA ilikuwa ikiendelea na udadisi picha za Satelite kusaka mabaki ya ndege hiyo ya Malaysia.
pamoja na ua ushirika wa Nchi za Norway, New Zealand na Marekani katika kutafuta mabaki hayo, tangazo hilo limekuja huku juhudi za
kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara la Hindi zikimalizika kwa
siku na siku bila mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita. Ndege na meli za nchi mbali mbali zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.BBC

No comments:
Post a Comment