WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTUMIA KALAMU VIZURI KATIKA KIPINDI CHA KUELEKEA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) na kuwaasa kutumia kalamu vizuri hasa katika kipindi hiki cha uandaaji wa katiba mpya kwa maslahi ya Taifa, kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
Mhadhiri katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dkt. Ayoub Rioba akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) na kueleza kuhusu umuhimu wa Vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uandaaji wa katiba mpya, Kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwalimu Bashiru Ally akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) na kuwaasa kutumia nyenzo zote ikiwamo Rasimu ya Katiba, Hotuba ya Mh. Rais Jakaya Kikwete hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika upatikanaji wa katiba mpya. kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa habari Hawapo Pichani) na kuwaasa wananchi kuwa na umoja hasa katika kipindi hiki cha upatikanaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya Taifa na Wananchi kwa Ujumla. kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment