Wakati uso wasaa ya dunia unaenda kasi sana, huku nao wana sayansi wakiumiza kichwa kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea, nayo Brazili ikiwa na maombolezo ya nahodha wake aliyewaisaidia kutwaa kombe la dunia pale Sweeden 1950 , wakati huo huo sherehe ya mzee Arsene wenger kutimiza mechi 1000 zikishereheshwa kwa kipgo kibaya cha goli 6-0 kutoka kwa Chalsea, bado uso wa saa wa dunia ukasema kwa nini Manchester United wakiwa mabingwa wa EPL wasistahili kukutana na bingwa mwingine wa Bundesliga ,Bayern Munchen. The Bavarians.
Luis Figo, nguli wa zamanI wa Barcelona , Real Madrid na Ureno huenda ameingia kwenye orodha ya watu ambao pengine wanachukiwa na mashabiki wa Man u, hiii ni kutokana na Droo ya robo fainali ambayo Figo alikuwa balozi wake .
Katika droo hiyo, klabu ya Manchester United imepangwa kucheza na bingwa mtetezi wa kombe hilo Buyern Munich, huku wenzao Chelsea wakipangwa dhidi ya Paris saint Germain ya nchini ufarasa.
Lakini tukio lililoshika hisia za watu wengi, na kuchafua mapumziko ya mwisho ya wiki kwa mashabiki ni hili la Mancheste united.
Mashabiki wengi kama sio wote, wakurugenzi, hata jopo la ufundi la Man United, na hata wachambuzi na waandishi mbali mbali wa habari za michezo wasingetamani Mashetani wekundu kwa hali waliyo nayo kukutana na Bayern ya Pep Guardiola.
Wamevurugwa: Wayne Rooney na Manchester United watautafuna mfupa wa Bayern Munich?
Si kwamba timu hizi ndio zinakutana kwa mara ya kwanza, la hasha..! kwa mujibu wa vyanzo vya habari, timu hizi zimekutana takribani mara 9.
Manchester United imefanikiwa kushinda mara 2, kutoka sare mara 4 na kufungwa mara 3, huku tukio linalokumbukwa na watu wengi na linalowapa matumaini si mashabiki hata wachezaji wa sasa wa Man United na viongozi wao, ni hili la mwaka 1999 katika fainali hizo ambapo Manchester ikiwa chini ya koch Sir Alex Ferguson ilishinda na kutwaa taji hilo.
No comments:
Post a Comment