TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 24, 2014

MAWAKALA WA REDIO JAMII WATAJA FAIDA ZA MRADI WA SIDA PANGANI

DSC_0043

Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akisisitiza jambo katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya.
Na mwandishi wetu, Pangani
Mawakala wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari .
Wakitoa tathmini ya maendeleo ya mradi katika warsha inayowapa uwezo wa kuweka kumbukumbu za kazi zao na vyanzo vya habari kwa kutumia Tehama iliyofanyika Pangani, washiriki hao wamesema mafanikio hayo siyo tu katika taaluma bali pia yamewajenga na kuwaimarisha kimaisha.
Mmoja wa washiriki hao alisema, “kusema ukweli natoa shukrani zangu kwa SIDA na UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwa sababu mimi binafsi nimeweza kununua kompyuta pakato (laptop) kwa ajili ya kuendeleza niliyoyapa kwa vitendo, na niko mbioni kununua simu za kisasa aina ya ‘tablet’,” alisema Sospether Rugemarila kutoka Fadeco FM redio.
DSC_0105Sehemu ya washiriki wakifutilia kwa umakini mafunzo hayo.
Katika kipindi cha miaka miwili cha mradi huo, mafunzo mbalimbali yametolewa kwa mawakala wa redio jamii kama vile matumizi ya mtandao katika kutafuta habari, mbinu mbalimbali za kupeleka taarifa na vipindi vya redio kupitia mtandao, matumizi ya simu aina ya ‘smartphone’ katika kuripoti taarifa maalum au majanga na matumizi ya mitandano ya kijamii kwa lengo la kuwasiliana, kushirikiana na kubadilishana mawazo, taarifa na vipindi vya redio.
“Sisi baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya simu aina ya “smartphone” tulifungua akaunti ya pamoja ya Facebook kwa jina na UMMAREJA kama ulingo wetu wa kubadilishana mawazo, taarifa na masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wetu kama mawakala,” alisema mwenyekiti wa umoja huo Msuli Mwaijengo kutoka Kyela FM redio.
DSC_0281Sospeter Rugemarila wa FADECO FM Redio, akizungumzia mafanikio aliyoyapata kutokana na mafunzo ya kuzipa uwezo Redio Jamii matumizi ya Teknolojia mpya katika kukuza upatikanaji na upashaji habari vijijini.
Sabina Nestory ni miongoni mwa mawakala ambao walikuwa na uwezo mdogo sana kabla ya mafunzo haya kuanza. Lakini ila anapohudhuria mafunzo mapya na kiwango chake pia kimekuwa kikiongezeka kiasi cha kumfanya aone umuhimu wa kununua simu aina ya ‘smartphone’ ambayo anasema itamrahirishia kutafuta na kutuma taarifa mbalimbali kwa niaba ya chama cha Umoja wa Wanawake katika Habari na Mawasiliano Sengerema (WAHAMASE) unaomiliki kituo cha Sengerema FM redio.
“Mimi nilipohudhuria mafunzo ya Tehama Ifakara nilikwenda moja kwa moja dukani kununua simu ya ‘smartphone’ ili nione inafanyaje kazi, ninayo, bado naisoma huku nikiendelea kuitumia kwa kuripoti matukio mbalimbali ya vijijini hususan ya maendeleo”.
DSC_0290Peter Marlesa wa Sengerema FM Redio, akielezea jinsi alivyofanikisha kutayarisha makala na vipindi mbalimbali zikiwemo habari za Mahakama na migogoro vijijini.
Mafunzo hayo yameweza kuwapandisha ngazi baadhi ya mawakala kuwa wafanyakazi vituoni baada ya kuonyesha umahiri na ujasiri katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku kama ilivyofanyika Mtegani FM redio, Makunduchi Zanzibar na Sengerema FM, Sengerema Mwanza. Peter Marlesa ni miongoni mwa waliobahatika kupanda ngazi kutokana na umahiri na ubunifu wake katika kuandaa vipindi mbalimbali kwa kujituma.
“Baadhi ya mambo niliyofaidika na mradi ni utayarishaji wa vipindi vya makala ya redio, jarida, vipindi vinavyohusu makundi maalum, habari za mahakamani na migogoro na taarifa za habari. Ni mara ya kwanza katika kituo chetu kuandika habari za mahakamani na maeneo tata vijijini.”
Kwa mara ya kwanza warsha hii ya kuwapa uwezo wa kuweka kumbukumbu imewakutanisha mawakala 25 kutoka redio tisa ambazo ziko kwenye mradi wa kuzipa uwezo redio jamii matumizi ya Tehama ulioanza mwaka 2012 ambao baada ya hitimisho watapitiwa vyeti vya ushiriki. Redio hizo ni Fadeco, Kahama, Kyela, Micheweni, Mtegani, Orkonerei, Pambazuko, Pangani na Sengerema.
DSC_0112Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa maelekezo jinsi ya kufanya mazoezi kwa vitendo.
DSC_0347Sabina Nestory wa Sengerema FM Redio, akionyesha Smart Phone yake aliyoinunua wakati wa mafunzo ili kufanikisha mafunzo ya matumizi ya simu na habari kwa vitendo.
DSC_0268Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama kutoka UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiewaelekeza jambo washiriki namna ya kuhifadhi habari kwa kutumia simu yenye uwezo mkubwa (Tablet).
DSC_0084Programme Assistant wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka UNESCO, Rosemary Lyamba, akitoa maelekezo kwa washiriki katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0178Picha juu na chini ni washiriki wa warsha hiyo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya TABLET.
DSC_0064
DSC_0263Washiriki wakiwa kwenye kazi za vikundi.
DSC_0400Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na mawakala wa Redio Jamii nchini.

No comments:

Post a Comment