Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhusu hali ya upatikanaji wa maji kwenye halmashauri hiyo wakati wakiwa kwenye moja ya kisima kinachotumika kusukuma maji kupeleka kwenye tanki la maji kasha kusambazwa katika maeneo mengine kijijini hapo
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali Ngemela Lubinga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhiwa lita 90,000 za maji na litaweza kuhudumia wakazi wapatao 2000 katika kijiji hicho cha Isinde siku ya kilele cha wiki ya maji .viongozi wa mkoa huo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali Ngemela Lubinga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhiwa lita 90,000 za maji na litaweza kuhudumia wakazi wapatao 2000 katika kijiji hicho cha Isinde siku ya kilele cha wiki ya maji .viongozi wa mkoa huo.
Na Kibada Kibada Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewahimiza wananchi wa Mkoa huo kutunza mazingira na kutoharibu vyanzo vya maji kwani kutofanya hivyo kunaleta madhara makubwa katika maisha ya kila siku.
Akiongea na wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha maji Mkoa yaliyofanyika kwenye kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu amesema wananchi wanatakiwa kutunza mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu.
Katika hotuba yake hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya huyo, imeeleza changamoto hizo za uharibifu wa mazingirazi zinazoukabili Mkoa wa Katavi kuwa ni uhamiaji holela wa wananchi kutoka mikoa ya Kigoma, Mwanza,Tabora,Simiyu na Shinyanga ambapo humami a na kuchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu kwenye vyanzo vya maji na mazingira
Aidha amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili kutunza na kuendeleza miradi ya maji waliyojengewa na serikali ili iweze kuwanufaisha wananchi wa Mkoa huo kwa kuwaondolea matatizo ya upungufu wa maji uliokuwa ukiwakabili.
Katika hatua nyingine amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili fedha inayopatikana isaidie kuendeleza ukarabati unaoweza kijitokeza iwapo kutakuwa na uharibifu wowote kwenye mradi wa maji kwa kuwa miradi ya maji ni mali yao.
Awali Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi katika taarifa yake ya ujenzi wa tanki la maji alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 200 zimetumika katika ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa kuchukua ujazo wa lita 90,000 (90m).
Msengi ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuwaondolea kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha Isinde kwa muda mrefu.
Naye Mhandisi wa Maji Mkoa wa Katavi, Elieda Mwakasungura katika Taarifa yake ya Mkoa wa kuhusu maji alieleza kuwa wananchi wanaopata maji safi na salama katika mkoan huo ni asilimia 48 hali ambayo inaonesha bado lipo tatizo la upatikaji wa maji safi na salama katika mkoa huo.
Miradi mingine inaendelea kutekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda katika kijiji cha Ikola,Ngomalusambo na Karema,miradi mingine inatekelezwa katika Halmashauri ya Nsimbo.
No comments:
Post a Comment