TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, July 28, 2014
Bahati Bukuku apata ajali ya gari akielekea Kahama kwenye Huduma
Usiku wa kuamkia leo, muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama kwenye huduma.
Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku
kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa awali zimeshindikana, kutokana na
kushindwa kugeuka wala kuinuka - akiwa amelazwa.
![]() |
| Frank amesafishwa kichwa na anaendelea vema. Muujiza wake ni kwamba nguo aliyokuwa amevaa ilichanwa na vioo, lakini yeye mwenyewe hajachubuka kutokana na vioo hivyo. |
Tayari ndugu na marafiki walishafika
kutoka Dar es Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita
kuwajulia hali na kuwafariji.
Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU
(31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na
kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine
linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema
ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara
kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.
Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za
vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za
injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER
(20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam
ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote
wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao
zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar
es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU
na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la
Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
![]() |
| Jennifer Mgendi (kushoto) akimjulia hali rafiki yake, Bahati. |
Sunday, July 27, 2014
SIMANZI ZAENDELEA KUTAWALA NDANI YA NYUMBA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT)
Jaji
Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa
wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo LUGHA
GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho ya
Taifa mwanzoni mwa wiki.
Mshiriki
wa TMT, Mwanaafa Mwinzago akifunika uso wake kwa kutoamini kuwa
ameponea kwenye tundu la sindano kutokana na kuondolewa katika maumivu
ya Jua la Utosi na kuendelea na mashindano hayo
Mshiriki
Wa TMT, Moses Obunde (Mwenye Suti) akimpongeza Mshiriki Mwenzie Mzee
Kapalata Mtawa kwa kuweza kuondolewa Kwenye Jua la Utosi na Kupelekwa
Kivulini katika Shindano la TMT linaloendelea.
Washiriki
walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku
mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.
Simanzi Zikianzia hapo sasa mara baada ya Washiriki kupunguzwa ili apatikane mmoja wa kuondoka.
Majaji
wa shindano la TMT wakimsikiliza kwa makini Mshiriki wa TMT, Mwanaafa
Mwinzago (anayeonekana kwenye runinga mbele) wakati akijielezea kabla ya
filamu fupi aliyoshiriki kuonyeshwa ili majaji waweze kutoa hukumu kwa
washiriki wa kundi hilo
Majaji
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katikati wakiwasikiliza
washiriki wa kundi la kwanza wanavyojielezea kabla ya filamu fupi
waliyochezwa kuonyeshwa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wiki
iliyopita
Majaji
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiangalia filamu fupi
iliyochezwa na washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)
katika ukumbi wa makumbusho kabla ya kuanza kutoa hukumu kwa washiriki
ni nani anatoka na nani anabaki.
Wakabaki wawili na hatimaye mmoja kati ya hao aliweza kuondolewa katika mashindano hayo
Hatimaye
Mshiriki Isalito Isaya Akaweza kurudi ndani ya Mjengo wa TMT kutokana
na Kura zake kumzidi Mshiriki mwenzie Pendo ambaye aliweza kuaga
mashindano hayo kutokana na kura kuwa chache
Baadhi
ya Washiriki wa TMT wakimuaga Mshiriki mwenzao Pendo Edward (Katikati)
ambaye aliweza kutolewa kwenye mashindano kutokana na kura kuwa
chache.Picha Zote na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatua
ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia wiki
ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano hilo
wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano
bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo za
watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti wake
na uzuri wake pia.
Mshiriki
mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza kuchomwa na jua la utosi
lililompelekea kutoka kwenye shindano hilo kubwa la Tanzania Movie
Talents (TMT) ambapo mpaka sasa washiriki kumi na tano (15) ndio
wamebaki katika nyumba ya TMT na hali ya simanzi bado inaendelea katika
nyumba ya TMT kwa wiki hii ambapo mshiriki mwingine atatakiwa kutoka.
Shindao
la TMT limekuwa likivuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje
ya Tanzania kutokana na Utofauti wake na ubora wake na kupelekea
watanzania wengi sana kufuatilia shindano hilo kwa ukaribu na umakini
zaidi.
Hatimaye
wiki hii Tanzania Movie Talents iliamua kuzindua Zoezi la kuwapigia
kura washiriki wake kupitia ukurasa wetu wa facebook ambapo sasa
watanzania na wapenzi wa TMT ambao wanauwezo wa kupata na kutumia
internet sasa wanaweza kuwapigia kura washiriki waliowavutia kupitia
ukurasa wetu wa facebook na vilevile kuendelea kuwapigia kura washiriki
kwa kutumia simu zao za mkononi.
Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678.
Na Jinsi ya Kumpigia kura mshiriki kupitia ukurasa wetu wa facebook BOFYA HAPA kwa kupata maelezo.
WAZIRI MKUU AONYA MATUMIZI YA RUSHWA UCHAGUZI MKUU
*Awaasa wananchi wasikubali kugeuzwa mtaji na wagombea
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amewaonya Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia rushwa
ili kupata nafasi za uongozi na hasa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba, 2015.
Ametoa onyo
hilo leo mchana (Jumapili, Julai 27, 2014) wakati akizungumza na mamia ya
waumini na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada ya uzinduzi wa dayosisi mpya
ya Ruvuma ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuwekwa wakfu Askofu
Amon Mwenda aliyeteuliwa kuongoza dayosisi hiyo.
“Ninawasihi
wananchi wawe makini na viongozi wanaopenda kutoa rushwa hasa katika kipindi
hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Kama mtu ana nia ya kweli ya kuongoza
ni kwa nini atumie fedha ili kupata nafasi ya uongozi?,” alihoji.
“Tatizo ni
kwamba hata wananchi hivi sasa wanakubali kupokea kile kinachotolewa na
wagombea. Atakuja huyu atakupa hiki na mwingine naye atakupa kile, lakini ujue
akiingia madarakani anaanza kurudisha haraka vile alivyowagawia,” alisema.
Aliwaonya
wananchi kuwa makini ili wasije wakageuzwa mtaji wa kuwanufaisha watu binafsi. “Tukikubali
kutumika ni sawa tutapata viongozi wakati wa uchaguzi, lakini watakuwa ni wale
wasio na hofu ya Mungu, wenye kujali maslahi yao kuliko ya wananchi
waliowachagua,” aliongeza.
Aliwaomba
viongozi wote wa dini waliohudhuria sherehe hizo pamoja na waumini wote
waendelee kuliombea Taifa ili Mungu aliepushe na janga hilo la watu kupenda rushwa.
Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wazidi kuuombea mchakato wa kupata Katiba mpya
ili wabunge wote warejee ndani ya Bunge na kuikamilisha kazi waliyoianza.
Alimuomba
Askofu huyo mpya apokee jukumu hilo kwa mikono miwili na kumuahidi kuwa kama
Serikali watakuwa naye bega kwa bega kuwaongoza Watanzania walioko kwenye
dayosisi yake. Dayosisi hiyo mpya inahusisha mkoa wote wa Ruvuma na wilaya ya
Ludewa eneo ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 72,630. Kati ya hizo km. za
mraba 64,233 ni za mkoa wa Ruvuma na km. za mraba 8,397 ni za wilaya ya Ludewa.
Mapema, akitoa hotuba yake ya kwanza mara
baada ya kusimikwa rasmi, Askofu Mwenda alisema dayosisi mpya ya Ruvuma
imezaliwa katika kipindi chenye changamoto nyingi za kidunia na utandawazi
ukiwemo mmomonyoko mkubwa wa maadili.
Hata hivyo,
akiainisha malengo ya dayosisi hiyo ambayo anakuwa Askofu wake wa kwanza,
Askofu Mwenda alisema mbali ya kufundisha neno la Mungu, dayosisi hiyo
itahimiza ufanyaji kazi ili wakazi wake wawe na akiba ya chakula cha kutosha.
Alisema
watashirikiana na Serikali na wadau wa ndani najje katika kutoa huduma za
kijamii hasa elimu na afya. Aidha alisema atakabiliana na changamoto za sasa
ambazo alizitaja kuwa ni mmomonyoko wa maadili, rushwa, mauaji ya albino,
unajisi wa watoto na ubakaji wa wanawake.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo, Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Alex
Malasusa alisema Kanisa lingependa kupata viongozi ambao ni wacha Mungu. Akirejea
mahubiri yake, Askofu Malasusa alisema inashangaza kuona kuna baadhi ya watu
wanagombea nafasi za uongozi lakini hawana mapenzi na Mungu aliyewaumba watu
anaotaka kuwaongoza.
“Bila
kujali imani ya mtu, tunatamani tungepata kiongozi ambaye anamcha Mungu. Awe
anapenda kuhudhuria ibada. Awe anampenda Mungu ndipo atawapenda watu anaowaongoza,”
alisisitiza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 27, 2014
MADAKTARI WAONYESHA MFANO KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI KUU YA MKOA WA RUKWA.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia
damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia
damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali
Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu
ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo.
Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
Dkt. Marwa akichangia damu.
Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)
TUHUMA NZITO KWA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA, WATOTO NA NDUGU WA VIGOGO WAJAZA MAJINA NAFASI ZA KAZI UHAMIAJI TANZANIA.
Matokeo
ya Usaili wa nafasi za kazi Uhamiaji yaliyotolewa katika magazeti
Julai, 2014 yameonesha kuwa katika Idara hiyo watanzania wengine mbali
ya watoto au ndugu wa wafanyakazi wa
Idara hiyo hawawezi kupata ajiya ndani ya Idara hiyo ya Serikali
kirahisi. Majina ya wengi walioitwa kazini ni watoto au ndugu wa
wafanyakazi wa idara hiyo.

1. Abdulhaq Amin Mandemla – Mtoto wa afisa Uhamiaji Amin Mandemla
2. Alphonce Kishe – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Aleluya Kishe
3. Asha Burhani Idd – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Tatu Burhani Idd
4. Beatrice Temba – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Joseph Kasike
5. Geofrey Justine Mhagama – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Rose Mhagama
6. Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Daniel Mgendi
7. Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Makwinya
8. John Alfred Mungulu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Alfred Mungulu
9. Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji Milambo
10. Michael J. Choma – mtoto wa Afisa Uhamiaji John Choma
11. Shimba H Zakayo – mtoto wa Afisa Uhamiaji Zakayo Mchele
12. Upendo E. Mgonja - mtoto wa Afisa Uhamiaji Mgonja
13. Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Adam Kidesu
14. Elizabeth Edward – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Edward Martin
15. Ester Mahirane – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Mahirane
16. Basil Lucian John – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Lucian
17. Frank E Kajura- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Kajura
18. Jacob P. Ulungi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Magnus Ulungi
19. Janeth John Milinga – Ndugu wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Milinga
20. Janeth R Lukuwi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Eliza Lukuwi
21. Joseph N. Yondani – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Mary Yondani
22. Leila khatib Irovya - Mtoto wa Afisa Uhamiaji Abbas Irovya
23. Lucian F. Mlula – ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Mlula
24. Neema Kasian Lukosi- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Zubeda Abbas
25. Pendo D. Gambadu – ndugu wa Afisa Uhamiaji Gambadu
26. Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward mwenda
27. Theresia Ernest Kalunde – Mtoto wa Ernest Kalunde
28. Veronica G Vitalis – Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
29. Victor G. Mlay- Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
30. Catherine J. Mapunda- mtoto wa Afisa Lucy Mapunda
Hii ni sampuli tu ila zaidi ya asilimia tisini ni watoto na ndugu wa Maafisa Uhamiaji.
Nadhani ingekuwa vyema wasingekuwa wanatangaza nafasi hizi bali wawe wanagawiana ndani kwa ndani.
Alamsiki.
Loga amvizia Hamis Kiiza
By MWANDISHI WETU
Kocha wa Simba,Zdravko Logarusic ‘Loga’
alisema; “Nawajua hao wachezaji Okwi na Kiiza ni wachezaji wazuri
niliwaona msimu uliopita, sina pingamizi kama nitaletewa hapa,
ninachotaka ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kunifanyia kazi
ninayotaka.”
UONGOZI wa Simba umegawanyika wapo ambao
hawataki kusikia usajili wa mchezaji yoyote kutoka Yanga lakini wapo
mabosi watatu huwaambii kitu kuhusu Emmanuel Okwi.
Kocha wa Simba,Zdravko Logarusic ‘Loga’ alisema;
“Nawajua hao wachezaji Okwi na Kiiza ni wachezaji wazuri niliwaona msimu
uliopita, sina pingamizi kama nitaletewa hapa, ninachotaka ni mchezaji
mzuri mwenye uwezo wa kunifanyia kazi ninayotaka.”
“Sina uhakika kama viongozi wangu wanataka
kuwasajili, lakini mimi isingekuwa hii kanuni ya shirikisho hata
ukiniletea wote hakuna shida, siwezi kumkataa mchezaji mzuri sababu
ikiwa ni klabu anayotoka, nitamchukua mchezaji yeyote kutoka Yanga na
hata Azam.” Mwanaspoti linajua kwamba Yanga wanafikiria kuachana na
Hamis Kiiza ingawa na Okwi na mwenyewe yuko kwenye wakati mgumu.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema hataki
wachezaji wabinafsi kwenye kikosi chake na hababaishwi na majina makubwa
hivyo atahitaji muda wa kuwatazama Okwi na Kiiza ili kuona uwezo wao
uwanjani kabla ya kumtema mmoja.
“Nasubiri waje kwanza, wacheze ili niwaone
wanavyocheza na uwezo wao kwa ujumla na baada ya hapo nitafanya maamuzi
sahihi yatakayokuwa na mafanikio.
“Kwa kifupi sitaki mchezaji mbinafsi, mchezaji
anayewaza nafsi yake pekee bali nataka mchezaji anayewaza mafanikio ya
Yanga na anayejituma kuhakikisha timu inanyakua kombe kwani mchezaji
anashinda mechi lakini timu ndiyo inayoshinda makombe,” alisema Maximo.
RAZA ATOA YA MOYONI KUHUSU MCHAKATO WA KATIKA MPYA
Mwakilishi
wa Jimbo la Uzini(CCM) Mohamedraza Hassanal akizungumza na Waandishi wa habari
katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar.Katika
mazungumzo yake alisema ni Vyema Bunge la Katiba likaghairishwa ili kutoa fursa
zaidi Watu wajihusishe na harakati za Uchaguzi Mkuu wa 2015 na Kupatikane Wasaa
mpana wa kujadiliana kwa dhamira ya dhati ya kupata Katiba Bora inayoridhiwa na
upande wa Bara na Visiwani.
MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOA WA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.
Mwantumu Mahiza akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said
Meck Sadiki leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa neno
la shukrani kwa Mkuu wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza kwa Kuukabidhi mwenge wa Uhuru
Salama Mkoani Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa neno
la shukrani kwa Mkuu wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza kwa Kuukabidhi mwenge wa Uhuru
Salama Mkoani Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili mkoani Dar es Salaam.(Picha na Hassan
silayo na Benjamin sawe).
Kikundi cha vijana toka Halmashauri ya Manispaa
ya Temeke wakisherehesha wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru uliokabidhiwa
kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa
Pwani Bi. Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam
Kikundi cha vijana toka Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala wakisherehesha wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru uliokabidhiwa
kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa
Pwani Bi. Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam
Meya
wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(mwenye miwani)
akishiriki kucheza pamoja na Kikundi cha vijana
toka Manispaa hiyo wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru leo Jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Vijana James Kajugusi(katikati) akiwaeleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga(Kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru
leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Vijana James Kajugusi alipowasili wakati wa kuukabidhi mwenye wa
uhuru kutoka wilaya yake.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga
akisalimiana na Vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa walipowasili kutoka Wilaya
ya Mafia
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akikimbiza Mwenge wa
Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi tayari kuanza ziara yake Mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo (Mwenye T-shirt
nyeupe) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.
Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.
Mwantumu Mahiza akikimbiza mwenge wa Uhuru Tayari kwa kuukabidhi kwa Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga
akisalimiana na Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda wakati wa
kuwasili kwa mwenge wa uhuru leo Jijini Dar es Salaam.
CAG AHUDHURIA KIKAO CHA 68 CHA BODI YA WAKAGUZI WA UMOJA WA MATAIFA NEW YORK, MAREKANI.
CAG wa Tanzania Ludovick S. L
Utouh pamoja na wajumbe wenziwe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa
Mataifa wakisaini ripoti 29 za taasisi za umoja huo zilizokaguliwa.
Wajumbe hao ni Liu Jiayi kutoka China, Amyas Morse kutoka
Uingereza ambae ni Mwenyekiti wa Bodi na Shashi Sharma kutoka India.
Ripoti hizo zilisainiwa tarehe 24/7/2014.
Picha ya makabidhiano ya mikoba ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa
iliofanyika kati ya mjumbe kutoka China anayemaliza muda wake wa miaka
sita aliyesimama wa pili kutoka kulia na mjumbe mpya kutoka India wa
pili kutoka kushoto.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi ya Umoja wa Mataifa na wawakilishi wao wa Umoja wa Mataifa.
Picha ya pamoja kati ya CAG,
watumishi wake pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa Kamlesh Vikamsey.

CAG akifanya mahojiano na mwahandishi wa Habari wa redio ya umoja wa mataifa Bi Priscila Lecomte.
Subscribe to:
Posts (Atom)







