TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 4, 2014

FLORA MBASHA, ROSE MUHANDO,SHUSHO NDANI YA KANISA LA GWAJIMA

Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.

Flora Mbasha akiimba katika kanisa la Gwajima.
Halima Mdee akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia waumini wa kanisa hilo.
Mchungaji Gwajima akicheza kwa shangwe.
Rose Mhando akicheza kwa hisia na shangwe kubwa.
Umati wa watu waliohudhuria misa hiyo wakifuatilia kwa makini.
Upendo Nkone akiimba kwa hisia kali.
Gwajima (kushoto) akicheza pamoja na Christina (Kulia).WAUMINI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo wamefanya ibada ya shukrani kwa kupata helikopta. 
Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo itatumika zaidi kutoa huduma  sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani kote.
Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.
Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.
Picha/Stori na Gabriel Ng’osha na Shani Ramadhani/GPL

ASKOFU KAKOBE NAMNA ANAVYOWAUDHI WANACCM NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, ILE ISHU YA UKAWA.


Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameongeza chumvi katika Mchakato wa Katiba kwa kueleza kuwa anaunga mkono msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutorejea kwenye awamu ya pili ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.

Kakobe pia alimtupia lawama Rais Jakaya Kikwete akisema hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo chanzo cha kuvuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Kakobe ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita takriban siku tatu tangu Rais Kikwete alipotoa hotuba yake ya kila mwezi na kujivua lawama hizo alizokuwa akitupiwa na watu wa kada mbalimbali.

“Naunga mkono Ukawa si kwa asilimia 100 bali asilimia 150 kwa msimamo wao wa kususia vikao. Tena sitegemei kusikia wamerejea bungeni, wakirejea watakuwa wamelogwa. Lazima wahakikishe upungufu huo unafanyiwa kazi kabla ya kurejea kwenye awamu ya pili ya vikao hivyo vilivyopangwa kuanza Agosti 5,” alisema.

Aliongeza: “Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume. Sioni kosa langu ni kutoa maoni kuhusu baadhi ya vipengele vya rasimu kwa sababu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine,” alisema Kikwete kwenye hotuba hiyo.

Hata hivyo, jana Kakobe aliyezungumza kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Kanisa la FGBF alisema kuwa anapingana na utetezi huo kwani hauna hoja ya msingi kwani alishavuruga mchakato huo tangu awali.

“Hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo iliyoharibu mambo yote hadi sasa tumefika katika hali hii.Anafanya hivyo akiwa na dhamira ya kuvuruga mchakato huo ili usiendelee kwa kuhofia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanguka katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Mapendekezo ya wananchi, ambayo yameorodheshwa kwenye rasimu, yanakinzana na matakwa ya chama hicho hiyo ndiyo sababu,” alisema Kakobe kwa msisitizo.

Askofu huyo alisema, ikibidi Rais Kikwete angefanya uungwana kwa kurejea tena kwa wananchi kwa kuandaa hotuba nyingine ili kuwaomba radhi kwa kuvuruga mchakato huo ndiyo mambo mengine yaendelee.

“Hata kama yeye ni kiongozi, kama amekosea, anatakiwa kuomba radhi…lazima awatendee wananchi haki yao kwa kukiri kuwa yeye ndiye chanzo cha mvurugiko huo ili kuruhusu mchakato wa Katiba uendelee ili Watanzania wapate Katiba wanayoitaka,” alibainisha Askofu Kakobe na kuongeza:

“Sasa umefika wakati wa chama tawala kukubaliana na mabadiliko yanayotokea. Wananchi wa sasa siyo wale wa zamani wakuburuzwa tu. Siku hizi watu wajanja, watu wanataka kuona maoni waliyopendekeza yanafanyiwa kazi bila kuweka usiasa ndani wala si vinginevyo.”

Alisema kuwa juhudi zote za kuunda kamati kwa ajili ya kufanya vikao vya maridhiano ili kutaka Ukawa warejee bungeni zimekuwa zikigongwa mwamba kutokana na kukosa uthabiti juu ya hilo.MWANANCHI

GWAJIMA NA KUFURU YA PESA,

  • ug2014
Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.
Flora Mbasha akiimba katika kanisa la Gwajima.
Halima Mdee akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia waumini wa kanisa hilo.
Mchungaji Gwajima akicheza kwa shangwe.
Rose Mhando akicheza kwa hisia na shangwe kubwa.
Umati wa watu waliohudhuria misa hiyo wakifuatilia kwa makini.
Upendo Nkone akiimba kwa hisia kali.
Gwajima (kushoto) akicheza pamoja na Christina (Kulia).
WAUMINI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo wamefanya ibada ya shukrani kwa kupata helikopta.
Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo itatumika zaidi kutoa huduma  sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani kote.
Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.
Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.

HATIMAYE MASOGANGE HATUNAE TENA AUKANA UTANZANIA?!!!....

Kama mnavyojua  kwakipindi cha miezi isiopungua mi nne sasa..Dada yetu Agnes Gerald aka Masogange aliamia nchini Afrika Kusini..Ambako kimsingi alipata bwana wa kuishinaye huko kama domozege ilivyolipoti mwezi uliopita
Sasa leo hii asubuhi kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM masogange ametupia picha ya pasi ya kusafiria ya Afrika Kusini...na ku-caption alama ya kupiga makofi....hii nikuuonesha kuwa kwasasa sio raia tena wa Tanzania..kwa mujibu wa sheria zetu hapa Tanzania,haziruhusu uraia wa nchi mbili kwa hiyo kama ni kweli basi Masogange sio mtanzania mwenzetu tena...Baadhi ya watu waliocomment kumsifia ameonesha kuwajibu kwa furaha zaidi...
Dah haya mama maisha popote!!!

Benki ya NBC yatoa mkopo wa mabilioni kwa Mohamed Enterprises

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini  hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100  kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuipatia kampuni ya Star  Oils mkopo wa takribani sh bilioni 100 ili kuAongeza ufanisi katika kampuni hiyo ya uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa nne kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (wa nne kulia), watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya utiaji saini makubaliano hayo.

PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE MEETS MCC’S NEW CHIEF EXECUTIVE OFFICER, DANA J. HYDE

mcc1
President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with MCC’s new Chief Executive Officer, Dana J. Hyde and her delegation  at the Ritz Carlton hotel in George Town Washington DC mcc4
President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with  MCC’s new Chief Executive Officer, Dana J. Hyde and her delegation  at the Ritz Carlton hotel in George Town Washington DC. Second left if Energy and Minerals Minister Prof Sospete Muhongo and right is Tanzani’a envoy to the US Ambassador Liberata Mulamulamcc2mcc3

AMAZING ! HUYU NDIE MUHUBIRI MWANAMKE ALIYECHORA TATOO KWENYE MATITI YAKE, IT'S CRAZY..CHECK OUT

Preacher With Tatoo
Anaitwa muhubiri Latascha Emanuel kutoka marekani ni muhubiri wa kike ambae anakuwa mfano wa kuigwa kwa jambo 1 tu la ujasiri wa kusimama na kuhubiri lakin matendo na muoekano wa mwili wake tuuache kama ulivyo..
A preacher with tatoo Latascha Emanuel
Advertisement

WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA AITAKA TAASISI YA KILIMO CHA MBOGA MBOGA (TAHA) KUONGEZA JUHUDI KATIKA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA.

Mkurugenzi mtendaji wa TAHA, Jackline Mkindi akiwaeleza wadau wa Kilimo waliohudhuria kuwa ni muda mrefu kilimo cha  mazao ya Maua, Matunda, mboga mboga, viungo, mbegu na viazi kimesahaulika na kwamba ni kilimo kinachoweza kumkomboa mkuilima kutokana na urahisi wa ulimaji wake aliwasisitiza waendeleze Kilimo hicho.
Meza Kuu 
Wadau Mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano huo

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ameitaka taasisi ya Kilimo cha mbogamboga(Tanzania Horticultural Association)TAHA kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wakulima.
Rai hiyo aliitoa juzi katika kongamano la Uwekezaji lililofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ambapo alikuwa mwenyekiti wa kongamano hilo.
Waziri Mkuu mbalo na kuwataka TAHA kuongeza juhudi pia alisifu juhudi zao katika kuinua kilimo na matumizi ya fursa za uwekezaji kwa wakulima.
Akizungumza katika Kongamano hilo, Mkurugenzi mtendaji wa TAHA, Jackline Mkindi, aliwaambia wadau wa Kilimo waliohudhuria kuwa ni muda mrefu kilimo cha  mazao ya Maua, Matunda, mboga mboga, viungo, mbegu na viazi kimesahaulika na kwamba ni kilimo kinachoweza kumkomboa mkuilima kutokana na urahisi wa ulimaji wake.
Alisema wakulima inabidi waelimishwe kuhusu kilimo cha mazao hayo kwa sababu hakihitaji maeneo makubwa na mtaji wa kutosha bali hulimwa katika eneo dogo lakini yakilenga soko la nje na sio kulima kwa mazoea kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Alisema ili kilimo cha mazao hayo kiwe na manufaa kwa wakulima wa Nyanda za Juu kusini na kukidhi mahitaji ya soko la nje inabidi serikali iangalie Changamoto zianazovikabili viwanja vingine vya ndege katika usafirishaji wa mazao hayo kama Uwanja wa Kilimanjaro( KIA) na Dar Es Salaam( JIA).
Mkurugenzi huyo alisema maeneo yanayopaswa kuangaliwa mapema kabla ya kuanza kwa kilimo cha mazao hayo kwa Uwanja wa Kimataifa wa Songwe ni pamoja na uwepo wa Ndege kubwa ya kusafirisha mizigo inayoweza kupeleka bidhaa hizo moja kwa moja sokoni pasipo kuathiriwa.
Aliyataja maeneo mengine kuwa ni kuwepo kwa eneo kubwa na jengo karibu na Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kupozea mazao hayo ili yasiharibike na sehemu maalumu ya kushushia mazao hayo na kupakilia kwenye ndege pasipo kuyabughudhi na kuyaharibu kabla ya kufika sokoni.
Alisema kutokuwepo kwa vitu hivyo kunapunguza ubora wa bidhaa hizo kama maua ambayo hayatakiwi kunyauka hadi yanafikishwa sokoni ndipo yanakuwa na soko la uhakika nje ya nchi.
Aliongeza kuwa soko la nje ya mazao hayo lipo na linauhitaji mkubwa isipokuwa ni kuzingatia vigezo vya usafirishaji ili kuyafanya yafike sokoni kama yalivyotolewa shambani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro alisema lengo la mafunzo hayo ni kujadili namna ya kuwawezesha wananchi kujikita katika uzalishaji wa mazao ya matunda, mboga mboga na maua  ili waweze kuboresha vipato vyao.
Alisema pia ni utekelezaji wa agizo la Raisi kuhusu manufaa ya uwanja wa Ndege kwa kilimo hicho kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo aliwataka viongozi wenzie kutekeleza kwa vitendo agizo hilo na siyo kuiongea tu mdomoni

HATARI: 'BOKO HARAM' WAJA TANZANIA!

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni ukosefu wa ajira na ujinga.
Olusegun Obasanjo na Benjamin Mkapa
Rais mstaafu wa Nigeria, Jenerali Olusegun Obasanjo (aliyeinama) akimuonyesha kitu Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa, katika mkutano wa marais wastaafu uliofanyika jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

SIRI ya kuanza kwa kundi la ugaidi la Boko Haram linaloendesha vitendo vyake vya kigaidi nchini Nigeria, iliyofichuliwa wiki iliyopita na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Olusegun Obasanjo, sasa inaweza kuiathiri Tanzania.
Obasanjo, akiwa katika kikao na viongozi wenzake wastaafu jijini Dar es Salaam, alisema ukosefu wa elimu na ajira kwa vijana wa nchi hiyo ndiyo chimbuko la Boko Haram.
Onyo hilo la Obasanjo kwa serikali za Afrika kujikita katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira na elimu linaweza kuwa chachu kwa viongozi wa Tanzania kutafuta ufumbuzi badala ya kushambulia wanasiasa.
Obasanjo aliongeza kuwa kundi la Boko Haram ambalo linatokea kusini mwa Nigeria, limekusanya wapiganaji wengi ambao hawana ajira, huku wengi wao wakiwa hawajapata elimu na ajira.
Akitoa ushauri kwa nchi za Afrika kuondoa tatizo hilo ili kuhakikisha uchumi wake unakua na kuondoa uwepo wa makundi kama hayo yanayosababisha kushusha uchumi, ni lazima wahakikishe wanatoa elimu na kutengeneza ajira kwa vijana wa mataifa yao.
Wito kama huo umewahi pia kutolewa na viongozi kadhaa nchini, akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, waliotaka kutafutwa kwa ufumbuzi wa tatizo la vijana wasiokuwa na ajira.
Lowassa, amekuwa akielezea namna ambavyo ukosefu wa ajira unavyotengeneza bomu kwa vijana linalosubiri kulipuka muda wowote, akitolea mfano wa kujitokeza kwa vijana 10,000 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakiwania nafasi 70 pekee za kazi Idara ya Uhamiaji.
Katika mazungumzo yake, Lowassa aliwaeleza wanahabari kwamba ili kuepusha ongezeko hilo linalokua kwa kasi, serikali ni lazima ihakikishe inatengeneza ajira kwa kuwa kila mwaka zaidi ya vijana 30,000 wanahitimu katika vyuo mbalimbali nchini.
Lowassa aliyejiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amekuwa akiishauri serikali kuchukua hatua kukabiliana na tatizo la ajira, ambalo limemsababishia malumbano na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka aliyejibu mapigo Machi 21, 2012 bungeni kwa kutoa takwimu zinazoonyesha namna serikali ilivyotengeneza ajira.
Kwa upande wake, Mbowe alilalamikia serikali kwa kutokuwa makini kwa kushindwa kulitafutia ufumbuzi tatizo la ajira kwa vijana ambalo aliomba liwe hoja maalum bungeni, serikali kuu, halmashauri na katika baraza la mawaziri kwani ni janga la taifa.
Wakati Mbowe akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha bungeni kuhusu mapendekezo ya serikali ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2014/15, alisema ajira ni mkakati na siyo suala la kufumania.
Akielezea njia za kuondoa tatizo hilo, aliishauri serikali kubadili mfumo uliopo wa kurundika kila kitu serikali kuu katika kutengeneza ajira kwani haiwezi kufanikiwa na badala yake alitaka kuwe na mkakati wa kutengeneza ajira katika halmashauri zote 133.
Mbowe alisema kuwa haoni sababu ya kuwa na wakurugenzi na wataalam wa uchumi katika halmashauri wasiokuwa na uwezo wa kutengeneza ajira.
Aliishauri serikali kuanzisha Mamlaka ya Majengo (Real Estate Authority – REA) itakayohusika kusimamia majengo mijini na kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia kujenga ajira kwani bila ya kufanya hivyo, vijana watalazimika kukimbilia mijini kwa sababu vijijini hakuna maendeleo wala mwelekeo.
Alisema ni aibu kwa halmashauri za Kinondoni na Ilala kutegemea ruzuku toka serikali kuu wakati zina vyanzo vingi vya mapato ambavyo vinaweza kusaidia kutengeneza fedha na ajira kwa vijana.
Aliongeza kuwa idadi ya Watanzania kwa sasa wanafikia milioni 50 na kila mwaka wahitimu wa vyuo vikuu wanafikia zaidi ya 40,000 huku kukiwa hakuna ajira.
Tanzania Daima Jumapili, imedokezwa kuwa kutovalia njuga kupuuza ushauri huo kunaweza kuchangia kushamiri kwa makundi ya kihalifu kama Boko Haram aliyoitaja Obasanjo.
Tayari hapa nchini kumezuka makundi ya kihalifu ambayo baadhi yao ni Watoto wa Mbwa, Panya Road na Badface ambayo yalitikisa maeneo mbalimbali kwa uhalifu uliozimwa na vyombo vya dola, lakini unaweza kuzuka tena siku za usoni.
Vijana hawa wamekuwa wakienda kupora wakiwa kundi kubwa lenye watu 30 hadi 100 wakiwa wamebeba silaha za jadi ambazo huzitumia kuwashambulia wanaowapora.
Zipo taarifa nyingine zinasema kwamba vijana hao hutumia njia ya kuimba kwa sauti kubwa wimbo huu; “Tunatakaa… pesa zetuu..!” huku wakiingia ndani kuchukua vitu vya thamani na kuwaacha baadhi ya majirani wakiduwaa kwa kudhani mtu anadaiwa kumbe anaibiwa.
Makundi ya vijana hawa yanaelezwa kuwa maskani yao yapo maeneo ya Manzese, Kigogo, Mburahati, Kigogo Luhanga na viunga vyake.
Vijana wanaofanya uhalifu kama huo, pia wamekuwa wakipatikana katika Mkoa wa Mara wakitumia majina ya Jamaica Mob, Mbio za Vijiti na Midomo ya Furu ambao mara kadhaa wamekuwa wakiwasumbua wakazi wa mkoa huo kwa kuwaibia na baadaye kuwajeruhi kwa silaha za jadi.
Mkoani Kilimanjaro pia liliibuka kundi la vijana lililokuwa likifanya uhalifu lijulikanalo kwa jina la Kunguru Hafugiki.
Tanzania Daima Jumapili, limekuwa likifuatilia baadhi ya nyendo za viongozi wa serikali katika kutatua kero za ajira, ambao wengi wao wamekuwa wakitoa zawadi za fedha na ahadi kwa vijana wakati wa uchaguzi badala ya kujikita kwenye miradi itakayokuwa endelevu.
Ahadi hizo na fedha hizo ndizo zinadaiwa kuwajenga chuki vijana pindi zinaposhindwa kutekelezwa na kujikuta wakishiriki kwenye vitendo vya kihalifu.
Chanzo: TanzaniaDaima: 'Boko Haram' waja nchini

Matukio katika Picha Nane Nane Lindi

 Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Edga Senga akipokea maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florence Turuka kuhusu masuala ya Maafa alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Mkoani Dodoma, Tarehe 3 Agosti, 2014.
Mratibu Msaidizi wa Tovuti ya TAYOA Bw. John J. Mindu akimweleza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Florence Turuka kuhusu tovuti ya vijana ya vijanatz. Com inayoelezea masuala ya Biashara, Afya, Ajira kwa vijana ili waweze kujiendeleza, wakati alipotembelea Banda hilo katika Maonesho   ya Wakulima NAne Nane tarehe 3 Agosti, 2014.