Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.
WAUMINI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat
Gwajima leo wamefanya ibada ya shukrani kwa kupata helikopta.
Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za
dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo
itatumika zaidi kutoa huduma sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani
kote.
Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.
Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye
Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili
maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho,
Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.
No comments:
Post a Comment