
Kwa upande wake mganga
mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoani Manyara Dr Peter Mshali akizungumza na
EATV baada ya kukabidhiwa kwa polisi ili kufanyiwa upelelezi amesema katika
mahojiano na jopo la madaktari walibaini vyeti hivyo ni bandia aidha pia
mtuhumiwa Dr huyo Godlove Sozigwa si mtaalam kulingana na maelezo yake bali ni
tapeli na hatari endapo angebahatika kupata nafasi hiyo.
Naye kamanda wa polisi
mkoani hapa ACP Deusdedit Nsimeki amekiri na katika mahojiano amesema polisi
imebaini baada ya kumfanyia mahojiano na upekuzi kumkuta na kompyuta
mpakato(laptop) muhuri wa kuchonga wa hospitali ya rufaa ya Muhimbili, koti na
vyeti mbalimbali, lakini wanafanya upelelezi zaidi kabla ya kumfikisha
mahakamani.
Tangu awali EATV
ilishughudia mtego huo mapema asubuhi na baada ya mtuhumiwa Godlove Sozigwa
kufikishwa polisi amekiri kuwa yeye si daktari aliyesoma chuo hicho cha Muhimbili
bali anafanya hivyo kutokana na mazingira magumu, hasa kwa kuipenda taaluma ya
udaktari baada ya kujifunza katika kituo cha tiba cha Neptune cha matabibu ya
kichina kilichopo Ubungo Plaza jijini Dar-es-salaam na kupata uzoefu.
No comments:
Post a Comment