By KHATIMU NAHEKA
- Awali Yanga ilipanga kupeleka kikosi cha mastaa wao, lakini baadaye Kocha Mkuu, Marcio Maximo, akabadili mawazo na kusema vijana waende na yeye atakwenda Pemba na kikosi cha kwanza kukisuka zaidi.
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati (Cecafa) limepokea majina 20 ya Yanga na kuyaangalia mara mbili na
kisha kuyaweka pembeni na kuwaambia viongozi wa Jangwani pamoja na
Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF): “Msitutanie hili siyo bonanza”
Awali Yanga ilipanga kupeleka kikosi cha mastaa
wao, lakini baadaye Kocha Mkuu, Marcio Maximo, akabadili mawazo na
kusema vijana waende na yeye atakwenda Pemba na kikosi cha kwanza
kukisuka zaidi.
Katika orodha ya wachezaji 20 wamo wa kikosi cha
pili ambao ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Nizar Khalfan, Rajab Zahir,
Hussein Javu, Said Bahanuzi, Omega Seme, Oscar Joshua. Kutoka kikosi cha
vijana wamewachukua Said Ally, Kulwa Baumba, Patrick Ngoyani, Joseph
Sadick, Amos Abel, Mwinyi Ndimbo, Henry Michael, Shaban Idd, Hamis Issa,
Juma Kayanda, Frank Shineiba na Frank Gerald.
Mwanaspoti linajua kwamba Cecafa pamoja na
waratibu wa michuano hiyo ambayo ni Shirikisho la Soka la
Rwanda(Ferwafa), ilizungumza na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima
(hayupo kwenye orodha) na akawahakikishia kwamba kikosi kilichotumwa ni
wachezaji wa benchi na vijana wakali wote wamewekwa kando akiwamo yeye.
Cecafa ikarudisha majina hayo kwa Yanga na TFF na
kisha kuwapa mpaka usiku wa kuamkia leo Jumanne wabadilishe, lakini
Yanga wakakomaa na hadi tunakwenda mitamboni kulikuwa na mzozo mkubwa
huku Yanga ikisisitiza kwamba uamuzi wake ni sahihi kwani wachezaji hao
ni wa Yanga kikanuni.
Hivyo Cecafa ikaamua kupiga simu Azam na
kuwaambia wakae tayari kuchukua nafasi ya Yanga kama klabu hiyo
itasimamia msimamo wake.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye, alisema
wamekigomea kikosi cha Yanga kwa vile ni dhaifu kisichoendana na hadhi
ya mashindano.
Musonye alisema waliitaka Yanga kubadilisha haraka
kikosi chao ikiwa ni pamoja kuwaingiza wachezaji wao wenye majina
makubwa wakiwemo kipa Juma Kaseja, Mbuyu Twite na wachezaji wao wawili
wapya Genilson Santos ‘Jaja’ na Andrey Coutinho pamoja na kocha wao
Maximo na kama hilo lingeshindikana mpaka usiku watawapiga chini na
kuipa Azam nafasi.
Yanga inapaswa kushiriki kwa vile ndio ilikuwa bingwa wa Bara msimu uliotangulia kabla ya uliopita.
“Unajua hii kwa Yanga inakuwa kama tabia yao kuwa
na visingizio vingi, kwanza walikuwa na kiburi cha kuchelewa
kuthibitisha kushiriki, lakini sasa wametuma watoto, leo ikikubaliwa kwa
Yanga kesho itafanywa na timu nyingine hatutaki kuruhusu hilo,” alisema
Musonye.
“Ukiacha hao wachezaji wanaosema wapo katika timu
ya taifa ambao hawazidi wanane, kuna wachezaji wengi wapo hapo Dar es
Salaam wakifanya mazoezi mfano ni Kaseja (Juma) hao Wabrazili kijana wao
Twite (Mbuyu), lakini angalia hata kocha Maximo naye haji, hiyo ni
dharau,” alisisitiza Musonye ingawa Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu
alikuwa akidai kwamba hawana taarifa na walikuwa wanasubiri tiketi tu.
Msemaji wa Ferwafa, Bonny Mugabe alisema: “Yanga
wameonyesha dharau kubwa kwa Cecafa, haya mashindano Rais Paul Kagame
amewekeza hela nyingi sana hatuwezi kukubali kuletewa timu ya majaribio.
Walichofanya Yanga ni dharau na hakivumiliki.
No comments:
Post a Comment