TASNIA
ya filamu Bongo imepata pigo tena baada ya msanii aliyekuwa akichipukia
kwa kasi, Patrick August ‘Bryton’ kufariki dunia kwa ajali mbaya ya
pikipiki.
Akizungumza
na paparazi wetu, Mwenyekiti wa Sherehe na Maafa kwa wasanii wa Wilaya
ya Kinondoni, Masoud Kaftany alisema Bryton alipata ajali usiku wa
kuamkia Jumapili maeneo ya Tabata - Relini wakati akirejea kwao maeneo
ya Tabata - Kinyerezi.
Alikuwa akiendesha mwenyewe pikipiki, akavaana uso kwa uso na gari, ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani marehemu alipasuka vibaya kichwa hali iliyosababisha damu nyingi kuvuja na kusababisha kifo chake
Baadhi
ya sinema alizoigiza enzi za uhai wake ni pamoja na Muuza Genge na
Mapenzi ya Fukara iliyomshirikisha Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wasanii
wengine. Mwili wa marehemu Bryton ulisafirishwa jana (Jumanne) kwenda Rombo,
mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyikwa leo
Jumatano.
No comments:
Post a Comment