TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, October 26, 2014

HABARI ZILIZOTAWALA SIKU YA JANA KWENYE VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI NI PAMOJA NA

Mke wa Rais wa China aipa msaada Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama

IMG_4094
Na Anna Nkinda – Beijing, China Mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan ameahidi kutoa vifaa vya shule vikiwemo vya maabara pamoja na vitabu kwa ajili ya shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ili  wanafunzi hao waweze kusoma vizuri masomo ya sayansi. Mama Liyuan aliitoa ahadi hiyo  jana wakati akiongea na  mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika ukumbi maarufu wa watu (Great hall of the People) uliopo mjini Beijing.
“Nina mapenzi na Taasisi ya  WAMA, nakupongeza kwa kazi unayoifanya ukiwa Mke wa Rais ya kuwainua wanawake kiuchumi na kuwasaidia  watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao nao wanapata elimu sawa na watoto wengine”.
Najua kitaaluma wewe ni mwalimu na unapenda shule mwaka huu nitakuunga  mkono zaidi katika masuala ya shule,  hii itawasaidia wanafunzi kusoma vizuri. Pia nitakuwa na ushirikiano  endelevu na Taasisi ya WAMA”, alisema Mama Liyuan.
Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kila kwenye maendeleo changamoto hazikosekani alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambazo ni  upungufu wa maabara, kutokuwepo kwa wataalamu wa maabara na walimu wa masomo ya sayansi wa kutosha.
Mama Kikwete  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema  katika upande wa elimu Serikali kwa kushirikiana na wananchi wamejitahidi kujenga shule nyingi za  Sekondari lakini  bado kuna  upungufu wa walimu wa masomo ya  sayansi , kutokuwa na maabara za kutosha, kutokuwa na vifaa vya maabara na  upungufu wa wataalamu wa maabara .
“Ninaomba  kuwe na ubadilishanaji wa ujuzi wa kazi (Exchange Program) kwa walimu wetu wa nchi hizi mbili hii itawasaidia kupata  utaalamu zaidi katika fani zao na kutoa mfano wa wataalamu wa maabara ambao wakija nchini watasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafundisha wanafunzi masomo ya sayansi kwa njia ya vitendo”, alisema Mama Kikwete.
Shule hiyo ambayo inamilikiwa na Taasisi ya WAMA wanafunzi  wake ni watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaotoka  katika mazingira hatarishi  kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani iko  kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Hii ni mara ya pili kwa Mama Liyuan kuiunga mkono Taasisi ya WAMA ambapo mwaka 2013 alipotembelea nchini  alitoa Yuan milioni moja  sawasawa na shilingi milioni  250 za kitanzania na mabegi ya shule 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama na vyerehani 20 kwa ajili ya Umoja wa Vikundi vya WAMA  (UVIMA).
Mama Kikwete  ameambatana na mumewe Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku sita.
===============================================================

Dk. Shein Azungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Zanzibar Ikulu.

IMG_2736WAKUU wa Mikoa na Wilaya Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,wakati alipokutana nao Ikulu Zanzibar.(Picha na Othman Maulid) 
IMG_2747KATIBU Mkuu  Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, akizungumza wakati wa Mkutano huo na Wakuu wa Mikoa na Wilaya walipokutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu Zanzibar.(Picha na Othman Maulid
IMG_2756RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya wa Zanzibar, wakati alipokutana nao Ikulu Zanzibar leo 25/102014.(Picha na Othman Maulid)
 =============================================================

KAMPUNI YA KARIATI YAKABIDHI WAKULIMA MATREKTA MANNE LEO, JIJINI DAR ES SALAAM

 
Kampuni ya Kariati Matracktor Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati, leo imekabidhi matrekta manne kwa wakulima wa wilaya ya Kondoa (matrekta matatu) na Mbarali (trekta moja), katika hafla iliyofanyika leo asubuhi, kwenye Ofisi za Kariati Matrektor, Kinondoni, Dar es Salaam. Zinazofuatia ni picha za hafla hiyo. Picha/Maelezo na Bashir Nkoromo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kariati Matractor, Omary Kariati akimkabidhi fungua za trekta Mwakilishi wa wkulima wa Kondoa, Karoli Lubuva, katika hafla ya makabidhiano hayo, iliyofanyika leo.
Kariati akikata uatepe kuzindua makabidhiano ya trekta hizo
Kariati akiwapa maelezo kuhusu trekta husika kabla ya kuzikabidhi kwa wawakilishi wa wakulima hao leo
Kariati akilijaribu moja ya matrekta hayo akiwa na mwakilishi wa wakulima kutoka Kondoa Karoli Lubuva.
=============================================================

Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira yatembelea kiwanda cha Mifuko ya Plastiki (East African Industy)

unnamedWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. Abdulkarim Hassan Shaha (wapili kulia),Pamoja na  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakikaguwa Mazingira katika moja ya kiwanda cha Mifuko ya Plastiki (East African Industy)kilichopo Mbagara jijini Dar es Salaam. unnamed1Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (kushoto),akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli (Mb),baada ya kuwasili kiwanda  kinachozalisha mifuko ya plastiki cha Binfijaa kilichopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam. unnamed2Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kulia),Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli Mb (wa tano ulia), pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakikaguwa mifuko Inayozalishwa na kiwanda cha BinFijaa kilichopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.
================================================================

Dr Slaa akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na TCD.

 
====================================================================

Mwandosya amuwakilisha JK Sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Zambia

unnamed 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya  akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo. unnamed3Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya (wa tatu kulia ) pamoja na Mkewe Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa wa Zambia wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia Mhe Edgar Lungu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, na wa  pili kulia ni Makamu wa Rais wa Nigeria Monance Namadi Sambo. unnamed5Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya  na mkewe Lucy Mwandosya wakisalimiana na Rais wa kwanza wa Zambia Mzee Kenneth  Kaunda wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo ambazo zimefanyika Mjini Lusaka jana.
Picha na Mpiga Picha wetu
================================================================

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NCHINI POLLAND

 PG4A6758Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland jijini Warsaw akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. Wengine Pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland, Bw. Marek Kloczko,Naibu Katibu  Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje ya Polland, (Under Secretary Of State Ministry of Foreign Affairs),  Bibi Katarzyna Kacperczyk na Bwana  Jerzy Pietrewiez ambaye ni  Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi ya Polland  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A6721Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watanzania waishio Polland baada ya kuwasili jijini  Warsaw kwa ziara ya kikazi  Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6747Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland  jijini Warsaw akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6770 Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda wakati alipowahutubia jijini Warsaw Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6813Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua matrekta yanayotengenezwa katika kiwanda cha  ROL- BRAT  kilichopo Warsaw, Polland akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6832Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua matrekta yanayotengenezwa katika kiwanda cha  ROL- BRAT  kilichopo Warsaw, Polland akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6897Waziri Muu, Mizengo  Pindaakipata maelezo kutoka kwa mshauri wa uchumi nchini Polland Bw, Aleksandr Zincman(kushoto)  kuhusu usindikaji ngano wakati alipokagua kiwanda cha kusindika unga   cha  Chojnow nchini Polland akiwa kayika ziara ya kikazi nchini huo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)   PG4A6900Waziri Muu, Mizengo  Pindaakipata maelezo kutoka kwa mshauri wa uchumi nchini Polland Bw, Aleksandr Zincman(kushoto)  kuhusu usindikaji ngano wakati alipokagua kiwanda cha kusindika unga   cha  Chojnow nchini Polland akiwa kayika ziara ya kikazi nchini huo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)    PG4A7041Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka  kwa mshauri wa uchumi nchini Polland Bw, Aleksandr Zincman (kulia) wakati alipotembelea  kiwanda cha kutengeneza  maghala ya kuhifadhia nafaka (silos), mashine za kukausha nafaka na mashine za kusafisha nafaka cha Chojnow nchini Polland akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
==================================================================

MKUTANO WA KUANDAA RAMANI YA MJI WA ZANZIBAR WAFANYIKA

04Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano wa Mpango  wa kuandaa ramani ya mji wa Zanzibar akizungumza na washiriki wa mkutano huo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.06   Baadhi ya washiriki wa mkutano uliojadili mpango wa kuandaa ramani ya Mji wa Zanzibar wakifuatilia maelezo yaliyotolewa kwenye mkutano huo katika Hoteli ya Marumaru.
03Mshauri mwelekezi kutoka kampuni ya Shapira Hellerman ya Israel,   Jos Hellerman akitoa taarifa  ya ramani ya Mji wa Zanzibar katika mkutano uliozungumzia mpango wa kuandaa matumizi bora ya ardhi katika Hoteli ya Marumaru, Shangani Mjini Zanzibar. 01Mkurugenzi  Mipango Miji na vijiji Muhammad Juma akitoa maelezo kwa washiriki wa mkutano wa kuandaa ramani ya Mji wa Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Marumaru, Shangani.
==============================================================

Tanzania and China Marks 50 Years of Diplomatic Relations

D92A7592President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the celebrations to mark 50 years anniversary of the establishment of the diplomatic relations with China held at Diaoyutai State Guest House in Beijing yesterday evening. D92A7608President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the celebrations to mark 50 years anniversary of the establishment of the diplomatic relations with China held at Diaoyutai State Guest House in Beijing yesterday evening. D92A7667President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and China’s Vice President Li Yuanchao cuts a special cake during the celebrations to mark 50 years of establishment of Diplomatic relations between Tanzania and People’s Republic of China yesterday in Beijing.  D92A7680President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete together with China’s Vice president Li Yuanchao unveils special coins during the celebrations to mark 50 years anniversary of the establishment of the diplomatic relations with China held at Diaoyutai State Guest House in Beijing yesterday evening.(picha na Freddy Maro)D92A7687President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete together with China’s Vice president Li Yuanchao unveils special coins during the celebrations to mark 50 years anniversary of the establishment of the diplomatic relations with China held at Diaoyutai State Guest House in Beijing yesterday evening.(picha na Freddy Maro)
===========================================================

Benki ya Exim yasaini mkataba wa mwaka mmoja na Stand United FC

unnamed
Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim Kanda ya Ziwa, Bw. Justus Mukurasi (wapili kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Stand United, Bw. Amani Vicent (wapili kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga jana. Mkataba huo utaiwezesha benki kuidhamini timu hiyo katika ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom (VPL) katika msimu wa 2014/2015. Wakishuhudia wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Tawi la Shinyanga, Bw. Hatunga Nicodemus na Katibu wa kamati ya Fedha, Bw. Bakari Salum (Wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.  
unnamed3  Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
 
Benki ya Exim imesaini makubaliano ya kuifadhili timu ya mpira wa miguu ya Stand United FC ya mkoani Shinyanga. Hii ni timu ya kwanza kupata ufadhili toka Benki ya Exim. Ufadhili huo wa mwaka mmoja utaisaidia timu hiyo kushiriki katika ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.
 
“Makubaliano haya yanaikutanisha Benki ya Exim na mchezo mkubwa kuliko yote Tanzania,” alisema mkuu wa matawi ya Benki ya Exim kanda ya ziwa, Bw. Justus Mukurasi jana katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga. Aliongeza kuwa hakuna mchezo wenye watazamaji, wafuatiliaji na mashabiki wengi zaidi nchini kama mpira wa miguu.
 
“Timu ya Stand United inanguvu kubwa ya kuunganisha mashabiki  wa kanda ya ziwa. Hivyo ni jambo stahiki kwa Benki ya Exim kuisaidia timu hii ambayo mashabiki wake ni miongoni mwa wateja wa Benki ya Exim,” alisema Bw. Mukurasi.
 
Mukurasi aliongeza kuwa pande hizo mbili zilifanikiwa kuingia katika makubaliano ambayo yataiwezesha benki hiyo kuifadhili timu ya Stand United toka Ligi Kuu Tanzania bara ilipoanza.
 
“Kwetu sisi udhamini tuliofanya sio tu wa nembo, nbali ni ufadhili wa muda mrefu utakaozinufaisha pande zote mbili,” alisema Mukurasi.
 
”Tunatumai kuwa kila mmoja wetu ataweza kujifunza kutoka kwa mwenzake ili kupata matokeo mazuri kwa pamoja. Exim itasaidia kukuza na kuundeleza mchezo wa soka na hivyo kuiwezesha benki yetu karibu zaidi na wateja wake,” alisema Bw. Mukurasi.
 
Naye, Mwenyekiti wa Stand United FC, Bw. Aman Vicent alisema kuwa timu yake inayofuraha kubwa kuingia katika makubaliano na Benki ya Exim. “Tunadhamiria kuimarisha uhusiano huu ili kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu,” alisema Bw. Vicent.
 
“Kwa niaba ya Stand United FC, ningependa kuishukuru Benki ya Exim kwa jitiada zao za kusaidia wachezaji wetu na timu kwa ujumla. Tunafanya kazi kubwa kuhakikisha tunainua vipaji vya wachezaji wetu ili na wao waweze kufika mbali zaidi,” aliongeza Bw. Vicent.

HABARI ZILIZOTIKISA SIKU YA IJUMAA WIKII HII NI PAMOJA NA :

President Kikwete meets China’s prime Minister Li Keqiang in Beijing

unnamed 
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meet and hold talks with Prime minister of the Peoples’ Republic of China Rt.Honorable Li Keqiang at the Great Hall of the people in Beijing this morning when the president paid a courtesy call on him.President Kikwete is on a State Visit in China at the invitation of China’s President Xi Jinping(photos by Freddy Maro)unnamed3

=============================================================

MTANDAO WA WANATAALUMA TANZANIA (TPN) WATOA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA

 Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Professional Approach Development, Lillian Madeje, akitoa mada kwenye kongamano hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
 Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa, akihojiwa na wanahabari kuhusu ngongamano hilo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal kwa ajili ya kufungua kongamano hilo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa akihutubia katika kongamano hilo.
 Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
  Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
 Hapa mdau wa mtandao huo akijisali kwenye daftari la mahudhurio.
  Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa (katikati), akiwa na viongozi wa mtandao huo. Kutoka kutoka kushoto, Naibu Katibu wa mtandao huo, Daniel Stephen, Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile na Mjumbe wa Mtandao huo, Modesta Mahiga.
 Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo.

 Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
………………………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
 
WATANZANIA wametakiwa kujiunga katika fursa mbalimbali za kiuchumi ili kukuza maendeleo ya nchi katika kiwango kinachostahili.
 
Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo  na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal wakati wa Ufunguzi wa wa kongamano la Mtandao wa Wanataaluma Tanzania(TPN).
 
Alisema kuwa ni wakati muafaka kujishughulisha na fursa za kiuchumi ili kufikia malengo ya millenia.
 
Alisema Serikali inaunga mkono jithada chanya zinazofanywa na sekta binafsi ambazo zipo kwa lengo la kuendeleza jamii na nchi kwa ujumla.
 
Mgimwa aliwata Watanzania wajiunge na TPN kwani una lengo la kuwahusisha katika sekta mbalimbali ikiwemo ujasiriamali ambao mara nyingi unakuwa katika kukuza maendeleo ya nchi.
 
“Watu wengi wanaweza kujiuliza kwamba wajiunge watapata nini lakini ukweli ni kwamba watanufaika na taaluma ambayo itakuja kuwasaidia katika maisha yao.
 
“Napenda niwapongeze kwani nimeona vijana wengi wamejiunga na mtandao huu ambao naamini utawasaidia vijana kuondokana na tatizo la ajira,”alisema.
 
Naye Rais wa TPN Phares Magesa alisema kuwa watu waache kusubiri kuwezeshwa badala yake wawe na mwamko wa kujiwezesha wenyewe.
 
Alisema lengo la sekta hiyo ni kutumia sekta ya ujasriamali katika kusaidia jitihada za Serikali  kukuza maendeleo ya nchini.
 
“Naamini kwamba kila kijana ambaye amehudhuria kongamano hili akitoka hapa anaweza kuwa mtu mzuri wa kujihusisha na ujasiriamali,”alisema.
 
Alisema kuwa maadhimio ya mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto mbalimbali zionazpojitokeza katika jamii na kuweza kuzitatua kwa wakati.www. habari za jamii.com
==============================================================

President Kikwete receives a rousing welcome in Beijing

D92A8241
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete introduces former OAU/AU Secretary General Salim Ahmed Salim to China’s President Xi Jinping during the formal reception held at the Great Hall of the People in Beijing this evening.Left is the Minister for Foreign Affairs Bernard Membe and second left is CCM Secretary General Abdulrahman Kinana. D92A8361President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and his host Chinese President Xi Jinping inspects a guard of honor mounted China’s People Defense force in Beijing this evening during a formal reception at the Great Hall of the people. President Kikwete is on State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping. D92A8392President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his host President Xi Jinping waves to the cheering crowd during a formal reception for the President and his delegation held at the Great Hall of the People in Beijing at the climax of his State visit this evening.(photos by Freddy Maro) D92A8416

=====================================

PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UN)

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Dar es Salaam leo, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 69 tangu kuundwa kwake. Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Karimjee. 
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez (kushoto) akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakifuatilia matukio mbalimbali ya hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maadhimisho hao.
Waziri Tibaijuka akihojiwa na wanahabri kuhusu 
maadhimisho hayo.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiwa 
kwenye maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisubiri kuondoka baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Gwaride maalumu la watoto la bendera likitoa 
heshima kwa mgeni rasmi.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni 
wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
 
PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UNTibaijuka alitoa wito huo leo katika sherehe za kuazimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.
 
Waziri Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maazimisho hayo alibainisha kuwa mabadiliko ya Tabia Nchi yameendelea kuwa tishio kubwa kwa binadamu katika siku za leo duniani kote.
 
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliitisha mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23, mwaka huu ambapo watu, nchi, mabara na wafanyabiashara walitoa tamko la kuungana pamoja kwa kila mmoja kuinusuru dunia.
 
Prof. Tibaijuka alisema kuwa akiwakilisha bara la Afrika, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliwasilisha mpango unaoonyesha juhudi za pamoja zinazofanywa na bara hilo kukabiliana na mabadiliko hayo.
 
“Katika mkutano huo, Tanzania imeahidi kuimarisha juhudi zake katika kutunza misitu na matumizi ya nishati kama upepo, sola na gesi asilia,” Waziri Tibaijuka alisema.
 
Hivyo Prof. Tibaijuka alihimisa nchi wahisani kutimiza ahadi zao kwa wakati hususani kutoa fedha kiasi cha dola za Kimarekani billion 100 kila mwaka hadi 2020 zitakazosaidia katika juhudi za kupambana na changamotio hizo.
 
Waziri aliwaambia wageni waalikwa katika sherehe hizo pia kuwa Tanzania inaendelea kutekeleza malengo ya changamoto za mileniamu na kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuimarisha amani, utawala wa sheria na kudimisha haki za binadamu.

President Xi Jinping Welcomes President Kikwete in Beijing

D92A8190China’s President Xi Jinping welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the Great Hall of the People in Beijing this evening during the official formal reception at the climax of the State visit at the invitation of the Chinese leader. D92A8192 D92A8213President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph with their host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan shortly after they arrived for an official formal reception at the Great Hall of the People in Beijing this evening(photos by Freddy Maro) D92A8224

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MKE WA RAIS WA CHINA MAMA PENG LINYUAN

IMG_4094Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na mwenyeji wake Mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakielekea kwenye chumba maalum kilichoko kwenye ukumbi wa The Great Hall of China kwa ajili ya kufanya mazungumzo. Mama Salma yupo nchini China akifuatana na Mume wake Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwenye ziara nchini humo. IMG_4135Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mama Peng Linyuan, Mke wa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kwenye jumba la mikutano la The Great Hall of China jijini Beijing tarehe 24.10.2014
IMG_4141Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mama Peng Linyuan, Mke wa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kwenye jumba la mikutano la The Great Hall of China jijini Beijing tarehe 24.10.2014
 PICHA NA JOHN  LUKUWI
=================================================================

Prof. Tibaijuka: Magonjwa ya Mlipuko yatekelezwe Kimataifa

Picha-na-3
Na Anita Jonas-MAELEZO
Umoja wa Mataifa umeshauri  kuchukua  hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya milipuko ya magonjwa hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya Kidunia kwani yanaathiri mifumo yote ya kimaendeleo.
“Mataifa yaliyoendelea yasingepuuzia mlipuko wa  ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza  Afrika  hali  isingekuwa  hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai yangu kwa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua  tahadhari wakati wote ”Alisema Prof. Tibaijuka.
Aidha, Prof. Tibaijuka alisema kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio miongoni mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo hawanabudi kusaidia Mataifa mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa Kijani wa Hali ya hewa.
Akizungumzia kuhusu hatua ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000 kutoka Burundi, Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha ulimwengu kuwa suala la mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa kazi na kuwafanya wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.
Naye Mratibu muwakilishi wa makazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez alisema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine,  wamepanga kusaidia na kuboresha miundombinu ya kiusalama ili kuendeleza amani Duniani kwani bila amani maendeleo ni vigumu kupatikana.
Pia Bw. Rodriguez aliipongeza Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia katika sekta ya afya kwa ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya nchini vinatoa huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
Sherehe hizo zimebebwa na kauli mbiu ya “Leave no One Behind” ikiwa na mlengo wa kuleta maendeleo yenye usawa duniani.
===============================================================

Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kuanza katikati mwa Mwezi Novemba.

IMG_8833
Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
…………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo,Maelezo
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema kwamba  zoezi la majaribio ya  Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linatarajia kuanza rasmi katikati mwa mwezi  Novemba mwaka huu.
Aidha  NEC imefafanu kwamba zoezi hilo, litafanyika kwa kutumia mfumo mpya wa ‘Biometric Voter Registration’(BVR) katika majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Kilombero, Halimashauri ya Mji wa Kilombero na Mlele, Halimashauri ya Mlele, ambapo vituo vya uandikishaji vimewekwa katika kata zilizomo katika majimbo husika.
Hayo yalisemwa  na Makamu Mwenyekiti wa NEC  pia  na Jaji  Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud  Hamid,wakati  akisoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam.
“Tume tayari imekwishapokea baadhi ya vifaa muhimu vya uandikishaji zikiwemo fomu za unadikishaji, hivyo kinachosubiriwa ni kupokea BVR kits 250 zinazotarajiwa kupokelewa wakati wowote kuanzia leo. Zoezi la Uandikishaji litakapoanza, vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni, vyama vya siasa vinaruhusiwa  kuweka mawakala wao katika kituo ili kushuhudia jinsi uandikishaji utakavyokuwa unafanyika,” alisema  Hamid.
 Makamu Mwenyekiti huyo alisema baada ya zoezi hilo kukamilika zoezi hilo litaanza katika maeneo mengine.
“ Tunatarajia Uboreshaji  wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa yote nchini isipokuwa mkoa wa Dares Salaam na Zanzibar.Uandikishaji katika mikao ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika baada ya uandikishaji katika mikoa yote utakapokamilika.Muda wa uandikishaji  utakuwa ni siku saba katika kila kituo,” alisema.
Aliongeza kwamba uandikishaji katika mikoa yote umepangwa kufanyika kuanzia mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu hadi katikati ya   Februari mwaka huu, wakati katika mikoa ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
 Alisema uandikishaji katika mikoa yote utafanyika katika awamu nne kwenye kila halimashauri ili kutoa fursa ya kuhamisha vifaa vya uandikishaji   kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.
“Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utahusisha  wapiga kura wote wapya na wa zamani. Wapiga kura wa zamani yaani wale ambao walikuwa wamejiandikisha katika Daftari la Zamani, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha vilivyoko karibu na maeneo wanayoishi ili kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole, picha na saini zao kuiongizwa katika mfumo Biometric Voter Registration na hatimaye watapewa vitambulisho vipya.” Alisisitiza.
Alisema wapiga kura ambao watakuwa na kadi zao za kupiga kura za zamani watatakiwa kwenda na kadi zao katika kituo cha kujiandikisha ili kurahisisha zoezi la kuhamisha taarifa zao za awali katika mfumo mpya wa BVR.
 Aidha alifafanua kwamba  kwa wapiga kura waliopoteza kadi au wale ambao kadi zao zimeharibika watatakiwa kwenta kituoni ili kujiandikisha na kupewa kadi mpya.
 Hamid alisema kwa wapiga kura wenye vitambulisho vya taifa Dares Salaam na Zanzibar watakuja na kadi zao ambazo ni taarifa zao zitasomwa na vifaa maalum ili kupunguza muda utakaotumika katika zoezi hilo, pia watapewa kadi mpya ya mpiga kura.
 Alisema kwa wapiga kura wanaoishi na ulemavu na wale ambao hawajui kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda kituoni na mtu mmoja katika familia wanayemuamini ili kusaidia katika uandikishaji.
“Uboreshaji huu unahusisha pia kuandikisha wapiga kura wote waliotimiza umri wa miaka 18 au zaidi na wale ambao ifikapo siku ya upigaji  kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 watakuwa wametimiza umri wa miaka 18. Pia wale wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuwahi kujiandikisha katika Daftari la  Kudumu  la Wapiga Kura katika mazoezi yote uandikishaji yaliyopita,” alisisitiza.
Hivyo jumla ya watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi wapatao milioni 23.09 wanatarajiwa kujiandikisha.
Hamid aliongeza kwamba mpiga kura atakayejiandikisha katika daftari hilo la sasa pekee na kupewa kadi ndiye atakayeruhusiwa kupiga kura.
“Wakati wa uandikishaji, kipaumbele kitatolewa  kwa watu wanaoishi na ulemavu, wazee, wagonjwa wakinamama wajawazito na wenye watoto wachanga. Hivyo hawatalazimika kusimama kwenye mstari.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka  NEC, Julias Malaba alisema tayari kiasi cha fedha cha Sh. bilioni 15 zimeshatolewa kwa ajili ya zoezi hilo.Huku Makamu Mwenyekiti wa NEC  akisema bajeti halisi litafafanuliwa baadae.
Kwa upande wake, Sisti  Cariah ambaye ni Mkuu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Naibu Katibu NEC, alisema daftari hilo litakamilika  Aprili 14,mwaka huu na litawekwa  wazi   kwa muda wa siku tano katika maeneo husika  ili kumwezesha kila mtu aliyejiandikisha  aende  kukagua na kujiridhisha kwa taarifa zake zimeandikwa  kwa usahihi.
 Tume hiyo inatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza kwa wingi katika vituo vyote vya uandikishaji kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari hilo.
Akizungumzia  kuhusu mfumo wa BVR alisema unasaidia kupunguza ujiandikisha mara mbili na kuwa na taarifa sahihi.
==============================================================

Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala latoa tamko.

 IMG_5529
Na Beatrice Lyimo- Maelezo-Dsm.
 
BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala latoa tamko kuhusu vipindi na matangazo yote  ya tiba asilia na tiba mbadala yanayoonyeshwa kwenye vyombo vya habari hapa nchini kuwa ni batili yenye kupotosha na yasiyo na vibali.
Akizungumza na waandishi leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Rogassian Mahunnah alisema kuwa, baraza hilo linawashauri wananchi kutoamini huduma zinazotangazwa na watu hao kuhusu tiba wanazozitoa.
Amesema kuwa, kwa mujibu wa Sheria shughuli zote zinazohusu tiba asilia na tiba mbadala ni budi zisajiliwe na kupewa kibali kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala.
“Kanuni za maadili, miiko na mienendo ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala, imeweka utararibu wa kufuatiliwa pale mganga wa tiba asili na tiba mbadala anapotangaza shughuli zake kupitia vyombo vya habari na mabango kwa jamii” alisema Profesa Mahunnah.
Kwa mujibu wa taarifa za Mwenyekiti huyo zinasema kuwa, kumekuwa na uwepo wa Maafisa feki wakijitambulisha kama Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na kutoa vibali bandia kwa njia ya simu kuhusu urushwaji wa vipindi katika vyombo vya habari.
Naye kaimu Msajili wa Baraza hilo, Bi. Mboni Bakari ameongeza kuwa, kumekuwepo pia na matumizi ya mashine ya Quantum na za kuondoa sumu mwilini kwa baadhi ya waganga ambao hawana elimu ya kutosha juu ya kutafsiri majibu na kujua matumizi sahihi ya vifaa hivyo.
“kutokana na kutosajiliwa kwa mashine hizi na TFDA, ufanisi na usahihi wa mashine ya kuondoa sumu mwilini hautambiliki na hauna uhakika” aliongeza Bi. Mboni.
Aidha, Baraza hilo linawasisitizia waganga kuendelea kufanya usajili kwenye ofisi za waratibu wa tiba asilia na tiba mbadala katika Wilaya na Halmashauri zao na kutoa huduma katika sehemu walizosajiliwa.
===============================================================

NGUMI KUPIGWA KESHO OKTOBER 25 FRENDS CORNER MANZESE

 
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana na George Dimoso mpambano wa raundi nane picha na SUPER D BLOG
 
Bondia Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG
…………………………………………………………………… Mwandishi Wetu Jumamosi ya October 25 katika ukumbi wa friends Corner Manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa ‘Moto wa Gesi’ na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki ‘Manny Chuga’ na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali